Mahakama yaruhusu kura ya siri ya kutokuwa na imani na Zuma

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,509
2,000
Mahakama ya juu zaidi nchini Afrika Kusini imeamuru kuwa kura ya kutokuwa na imani na Rais Jacob Zuma inaweza kufanywa kwa siri. Mahakama ya katiba ilisema kuwa spika wa bunge na haki ya kuamuru hatua kama hiyo. Awali alisema kuwa hakuwa na mamlaka kama hiyo.

Vyama vya upnzani vinaamini kuwa chini ya kura ya siri, wabunge kutokla chama cha Zuma cha ANC wanaweza kupiga kura ya kumpinga. Zuma aliponea kura za awaliaza kutokuwa na imani naye.

Bwana Zuma amekuwa chini ya shinikizo kufuatia shutuma nyingi ikiwemo madai ya ufisadi na mabadiliko kwa baraza la mawaziri yaliyokumbwa na utata.

Akitoa uamuzi huo Jaji mkuu Mgoeng Mgoeng, alisema kuwa spika wa bunge ana mamlaka ya kuamua ni njia gan kura hiyo itafanyika. Spika wa bunge Baleka Mbete ni afisa wa cheo cha wa ANC na alikuwa amedai kuwa sheria za bunge haziruhusu kufanyika kura ya siri,

Sasa tarehe mpya ya kura hiyo ya kutokuwa na imani itatangazwa.

chanzo. bbc swahili
 
Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
10,394
2,000
Hiyo kura ya siri ikitua pale mjengoni saa4 asubuhi tuu Sizonje out.
Nina uhakika huku kwenu tukifikia huko na mahakama ikarudisha mpira Bungeni na kusema Speaker na mamlaka ya kuamua aina gani ya kura ipigwe, huyu Ndugai wenu ataamua ipigwe ya wazi. Si kaambiwa ana mamlaka? Sizonje sio wa mchezomchezo na Ndugai hakohoi pale.

Hata huko SA, ushishangae pesa/vitisho/woga vikashinda na speaker "akatumia mamlaka yake" kuamua ipigwe ya wazi tu, afterall speaker ni kiongozi pia ndani ya chama cha ANC na alishaonyesha tangu mwanzo kupinga kura za siri. Africa bado sana.
 
Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
14,892

Kwanza kwa hapa hiyo kura ya siri itashindwa Mahakamani kabla ya kufika bungeni maana hakuna Jaji atakuwekuwa na guts za kuamua hivyo. Si unakumbuka yale ya mita200 wakati wa uchaguzi mkuu uliopita?

Sent from my Vodafone Smart Tab 3G using JamiiForums mobile app
 
Imeloa

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
7,319
2,000
Spika wa bunge la SA mwana mama Baleka Mbete kamwe hana ubavu wa kuamua ipigwe kura ya siri kwani hajitambui ni kibaraka wa Jacob Zuma.

Ni sawa tu na akina Ndugai na Ackson wa hapa kwetu. Ni aina ya watu wanaoamini kuwa rais ndiyo anawa-supply na oxygen wanayopumulia.
 
Yodoki II

JF-Expert Member
Oct 17, 2014
5,265
2,000
Nikiangalia kwa lugha ya kisheria, "anaweza" maana yake ni "may" kwa Kiingereza.Ukiidadavua "may" maana yake kuna option ya "may not". Either decision is discretal upon Mdm Speaker.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom