Mahakama yamwachia huru Mtikila katika kesi ya uchochezi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahakama yamwachia huru Mtikila katika kesi ya uchochezi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sokomoko, Sep 12, 2008.

 1. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mahakama yamwachia huru Mtikila katika kesi ya uchochezi
  Na Tausi Ally

  MAHAKAMA ya hakimu mkazi wa Kisutu jijini Dar es Salaam, imemuachia huru mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya kutoa maneno ya uchochezi dhidi ya viongozi wa serikali ya awamu ya tatu.


  Mchungaji Mtikila aliachiwa huru jana baada ya mawakili wa serikali, Irene Resulia na Prosper Mwangasila kushindwa kuithibitishia mahakama kama mchungaji huyo ana kesi ya msingi ya kujibu.


  Hakimu Msongo alisema amemuachia huru Mtikila kutokana na upande wa mashitaka kushindwa kuithibitishia mahakama kuwa ana kesi ya msingi ya kujibu dhidi ya shitaka namba 425 ya mwaka 2002.


  Mara ya mwisho katika mahakama hiyo, mwendesha mashitaka wa Polisi, Nassoro Sisiwaya aliiomba mahakama kufunga ushahidi wa kesi hiyo baada ya mashahidi watatu wa upande wa mashitaka kumaliza kutoa ushahidi.


  Kutokana na ombi hilo, Hakimu Msongo aliahidi kutoa uamuzi dhidi ya shauri la awali kama Mchungaji Mtikila ana kesi ya kujibu au la, uamuzi ambao umetolewa leo kwa Mchungaji huyo kuachiwa huru.


  Katika shtaka dhidi yake lililosomwa mahakamani, Mtikila anadaiwa kutoa maneno hayo Julai 27, 2002 kwenye viwanja vya Jangwani. Ilidaiwa kuwa maneno hayo ni ya uchochezi na ambayo yangeweza kusababisha kuvunjika kwa amani.


  Pia alidai kuwa rais wa awamu ya tatu, Benjamin W. Mkapa hakuwa raia wa Tanzania bali ni wa Msumbiji na kwamba hana uchungu na nchi hii kwa kuruhusu makontena ya mchanga wa dhahabu kupelekwa nje ya nchi.


  Ilidaiwa kuwa pia alitoa maneno mengine ya uchochezi kuwa kuwa waziri mkuu wa wakati huo, Fredric Sumaye ni gabachori na mwizi mkubwa.

  Source Mwananchi.
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Huyo Mtikila ni pandikizi la CCM , linatumika kivyakevyake ,sasa chukulia kama maneno hayo angeyasema Seif Sharif , saa ingine lazima watu wa duzaini za Mtikila mzisitukie ,anatumiliwa tu na CCM na serikali zake.
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,318
  Likes Received: 5,610
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama pandikizi la CCm huyu bwana ni mropokaji hasa anaejua anafanya nini....wakumbuka ameshakwenda jela miezi 9 sababu ya uchochezi..huyu ni mtambo kwelii sio mchezo....anaweza ropoka lolote
   
 4. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kumbe mlitegemea nini? kwamba ashindwe kesi apelekwe jela wakti tayali alisha andaliwa kwa kazi ya kuua upinzani TARIME???

  Ila nimesikitika sana kwamba Mtikila naye anaweza nunulika kirahisi namna hiyo!
   
Loading...