Mahakama yamuengua mjane wa Bilionea Erasto Msuya kusimamia Mirathi ya Mumewe

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Mahakama kuu Kanda ya Arusha, imemtengua msimamizi wa mirathi za marehemu Bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita aliyekuwa Mke wa Marehemu baada ya kushindwa kugawa Mali za marehemu Kwa wakati.

Bilionea Msuya, aliuawa Kwa kupigwa risasi zaidi ya 20 miaka tisa iliyopita katika eneo la Mijohoroni, wilayani ya Hai mkoani Kilimanjaro.

Akisoma hukumu hiyo Jana iliyokuwa ikionyeshwa kwa njia ya Video jaji wa Mahakama hiyo, Devota Kamzola alisema kuwa mahakama hiyo baada ya kupitia hoja za pande zote mbili imejiridhisha pasipo shaka kwamba mali za marehemu hazikuwahi kukusanywa ,kutolewa taarifa na kugawanywa Kwa wanufaika katika kipindi Cha miaka 9 tangu msimamizi wa mirathi ateuliwe.

Aidha mahakama hiyo imewateua watoto wawili wa marehemu Msuya, Glory Msuya na Simon Kelvin Msuya kuwa wasimamizi wa mirathi na kuagiza ndani ya miezi Sita wawe wamekusanya ,kuhakiki Madeni ,kugawanya Mali Kwa wanufaika na kutoa Taarifa mahakamani .

Shauri la kupinga msimamizi wa mirathi namba 66/2019 lilifunguliwa na Ndeshukulwa Msuya Mama wa marehemu Erasto dhidi ya mkwe wake Miriamu Msuya ambaye aliteuliwa na mahakama novemba 2013 kuwa msimamizi wa mirathi kupitia shauri la mirathi namba 8/2013.

Ndeshukulwa kupitia mawakili wake,Ismail Sharua na Fadhili Nangawe waliiomba mahakama hiyo imtengue Miriamu Mrita kuwa usimamizi wa mirathi ya mwanaye Kwa madai kwamba tangu ateuliwe hakuwahi kukusanya, kufunga na kugawanya Mali Kwa wakati.

Hoja zingine zilizowasilishwa na mawakili hao ni kwamba Miriamu Mrita anakabiliwa na kesi ya mauaji namba 5/2017 mahakamani isiyo na dhamana, pia alishindwa kumjali Kwa matumizi Mtoto wa marehemu mumewe Glory Msuya aliyekuwa nje ya nchi Kwa kumpatia fedha za ada, nauli ya kurejea nchini pamoja na matumizi binafsi.

Wakati hukumu hiyo ikisomwa na Jaji Kamzola mjibu maombi, Miriam Mrita alikuwa akiona na kusikilizwa kupitia mtandao wa mahakama(Video Conference) wakati akiwa katika Gereza la Segerea jijini Dar es salamu.

Akiongea mara baada ya kutolewa Kwa uamuzi huo, Familia ya Msuya kupitia Ndeshukulwa Msuya alishukuru mahakama hiyo Kwa kutenda haki Kwa kuwa lengo lao ni kuhakikisha watoto wa marehemu wanakuwa na haki ya kusimamia na kunufaika na Mali za baba Yao na sio mtu mwingie yoyote.

"Mimi sikuhitaji Mali yoyote ya mwanangu nilichotaka Mali zote zosimakiqe na watoto na sio mtu mwingine yeyote, tumepokea Kwa Furaha hukumu ya mahakama na haki imetendeka"alisema Msuya

Akiongea Kwa niaba ya Miriamu Mrita, Steven Mrita ambaye alikuwa msimamizi wa Mali za marehemu ikiwemo hoteli ya kitalii ya Sg baada ya kukabidhiwa na dada yake (Miriamu )alisema kwa upande wao wameridhika na uamuzi wa mahakama na hawàtakuwa na pingamizi lolote.

"Sisi tumeridhika Kwa moyo mweupe na uamuzi wa mahakama na hatutakuwa na pingamizi" alisema Mrita.

Ends

images%20(16).jpg
2287545_IMG-20200128-WA0006.jpg
---
VIDEO: Mauaji ya Erasto Msuya, Aneth Msuya na hukumu ya Miriam Mrita
Soma Sakata la Kifo cha Bilionea Msuya


MWENENDO WA KESI MAUAJI YA BILIONEA ERASTO MSUYA

Septemba 17, 2013 watuhumiwa wakiwa kwa mganga wakijizindika wasikamatwe

Soma Waliomua Bilionea Erasto Msuya wakutwa kwa sangoma

Juni 12, 2014, Mahakama yaelezwa jinsi Erasto Msuya alivyouawa
Soma Mahakama yaelezwa bilionea wa madini Erasto Msuya alivyouawa

Oktoba 27, 2017, Shahidi adai kuahidiwa Tsh 17m kutekeleza mauaji
Soma Shahidi aelezea walivyoahidiwa kulipwa Sh 17 milioni kila mmoja kumuua bilionea Msuya

Mei 11, 2018, Shahidi alidai kuwa Mfanyabiasha wa Madini, Chusa ndiye alipanga mauaji
Soma SHAHIDI: Chusa alipanga mauaji ya Bilionea Msuya

Mei 14, 2018 Mahakama iliwakuta na kesi ya kujibu washtakiwa 6
- Kesi ya bilionea Msuya: Sita wana kesi ya kujibu huku mmoja akiachiwa huru

Julai 23, 2018 washtakiwa wahukumiwa kunyongwa hadi kufa
soma Washtakiwa watano mauaji ya bilionea Msuya wahukumiwa na Mahakama Kuu adhabu ya kunyongwa hadi kufa

Agosti 18, 2018 waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa wakata rufani
Soma Waliohukumiwa kwa mauaji ya Bilionea Msuya wapinga kunyongwa

Jaji aliyetoa hukumu atishiwa kifo
Soma Jaji aliyesikiliza kesi ya mauaji ya Bilionea Msuya na kutoa hukumu ya kifo atishiwa kuuawa

Pia soma Aliyeachiwa kesi ya mauaji ya Bilionea Msuya aeleza mazito


MAUJI YA ANETH MSUYA NA MWENENDO WA KESI YA MAUAJI YAKE

Aneth Msuya aliuawa kinyama akiwa nyumbani kwake Kibada
Soma Aneth Msuya ambaye ni dada wa bilionea Erasto Msuya auawa kinyama Dar

AUG 23, 2016 Mirima Mrita alipandishwa kizimbani kwa tuhuma za mauji ya Aneth Msuya
Soma Mjane wa Erasto Msuya apandishwa Kizimbani Kisutu

SEPT 18, 2023 Mahakama ilimkuta Miriam Mrita na kesi ya kujibu Mauji ya Aneth Msuya
Soma Dar: Mke wa Bilionea Msuya akutwa na Kesi ya Kujibu mauaji ya wifi yake

FEB 23, 2024 Mahakama Kuu ilimuachia huru Miriam Mrita
Soma Mjane wa bilionea Msuya aachiwa huru, Mahakama haijamkuta na hatia mauaji ya Aneth Msuya


UGOMVI WA MALI ZILIZOACHA NA ERASTO MSUYA
Familia ilishindwa kuelewana suala la mirathi na kupelekea Serikali kuingilia kati
Soma Mali za Marehemu Bilionea Erasto Msuya, ndugu ngumi mkononi

Mama Mzazi wa Erasto Msuya adai kuwa mjane alikomba mali kabla ya mazishi
Soma Mama wa Bilionea Msuya: Mke alikomba mali kabla ya kumzika mwanangu

Wadau wahoji uhalali wa ndugu wa Miriam Mrita kusimamia mali za Erasto Msuya
Soma Mama wa Bilionea Msuya: Mke alikomba mali kabla ya kumzika mwanangu

Mama Mzazi wa Msuya akubali kuondoa shauri Mahakamani ili kulimaliza kifamilia
soma Mama wa Bilionea Msuya akubali kuondoa kesi kwa Muda Mahakamani

Mahakama yataka pande mbili za familia kukaa meza moja na kuondoa tofauti
Soma Ugomvi wa Mali za Marehemu Bilionea Msuya, Mahakama yanena

2021, Mahakama ilifikia uamuzi wa kumuondoa Miriam Mrita kuwa msimamizi wa Mali
Soma Mahakama yamuengua mjane wa Bilionea Erasto Msuya kusimamia Mirathi ya Mumewe
 
Ila kwa hiyo miaka tisa mali nyingi zitakuwa zimepotea, zimeshaliwa au hata kuharibika.
 
Ila kwa hiyo miaka tisa mali nyingi ziyakuwa zimepotea, zimeshaliwa au hata kuharibika.
Mali walianza kuzihamisha mara tu baada ya msiba wa Msuya, mama yake Msuya akashtuka na kukimbilia mahakamani, kutahamaki warangi wamebakiza magofu tu, mali nyingi walishauza, Miriam alikuwa na ndugu maboya boya tu halafu nyie akawaamini na kuwakabidhi mali za mumewe pasipo hata kuihusisha familia ya mumewe.
 
Alafu huyo jamaa yupo pamoja na hao watoto wa marehemu kama ulifuatilia hilo sakata na hao watoto wa marehemu wanamkubali mjomba wao kuliko hata bibi yao ndio mana huyo mrita hiyo hukumu kaipokea kwa mikono miwili, ila huyo bibi alitaka yeye ndo awe msimamizi
kumbe!!! ,ma bibi hawafai kuwa wasimamizi huwa wanapelekeshwa na mashangazi
mi nimejiuliza jamaa kama muda wote huo amesimamia Hotel na hajalalamikiwa basi atakuwa ni mtu asiye na shida
 
Kiuhalisia bado upande wa Mke(Mritas) wananguvu katika mali kuliko huo upande wa wazazi, hapo mjomba ataendelea kula kuku kwa mrija
 
Kiuhalisia bado upande wa Mke(Mritas) wananguvu katika mali kuliko huo upande wa wazazi, hapo mjomba ataendelea kula kuku kwa mrija
Inavyooneka huyo Glory Msuya cyo mtoto wa kumzaa huyo Mama Mrita ndio maana imesemwa kwamba hakutumiwa pesa ya matumizi wala nauli za kurudi nchini.Bibi atakula kupitia huyo Glory,na inaoneka bibi alifight ili Glory akubaliwe ale kupitia yeye.
 
Wanasheria KESI za matajiri kama hizi hawatakagi ziishe,ndo zinawatoaga Maisha.
Tegemea wapigiane simu wawashawishi wateja KESI irudi mahakamani.


Ila KESI ya maskini hukumu ikipita mwaka shukuru
 
Back
Top Bottom