Mahakama yamtia hatiani Zitto Kabwe katika kesi yake ya Uchochezi. Atakiwa kutotoa matamshi ya Uchochezi kwa mwaka 1. Asema kukata Rufaa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,861
Leo ikiwa ni siku ya Hukumu ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Waandishi wenye Press Cards wamekataliwa kuingia kusikiliza hukumu ya Zitto kwa maelezo kwamba si waandishi wa Mahakama.

UPDATE

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Ndugu Zitto ameachiwa huru kwa sharti kwamba asitoe matamshi ya uchochezi katika kipindi cha mwaka mmoja.

Zitto.jpg

0F8839DA-9DB3-4573-8215-6B3C076345EF.jpeg

Zitto kukata Rufaa dhidi ya hukumu yake

Zitto2.jpg

TAARIFA KWA UMMA

Chama cha ACT Wazalendo kimepokea kwa mshtuko taarifa ya kutiwa hatiani kwa Kiongozi wa Chama Ndugu Zitto Zuberi Ruyagwa Kabwe ambaye alishitakiwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkaazi Kisutu na kukabiliwa na mashtaka matatu chini ya Sheria ya Vyombo vya Habari.

Kwa mujibu wa hukumu iliyosomwa leo na Hakimu Huruma Shaidi, Ndugu Zitto ametiwa hatiani kwenye makosa yote matatu na kuachiwa huru kwa sharti la kutotoa matamshi ya kichochezi katika kipindi cha mwaka mmoja.

Ndugu Wananchi na Wanachama wa ACT Wazalendo, kwa sasa itoshe tu kusema kuwa Chama cha ACT Wazalendo kinapokea na kuyaheshimu maamuzi ya Mahakama ya Hakimu Mkaazi Kisutu yaliyotolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi na kwamba kwa sasa Chama kinasubiri kupokea ushauri wa mawakili wa Ndugu Zitto Kabwe kuhusu tafsiri ya hukumu hiyo na hatua sahihi za kuchukua.

Muda mfupi uliopita, nimeongea na Kiongozi wetu na amenihakikishia kuwa yupo imara na kamwe hukumu hii haitamrudisha nyuma. Mapambano ya kuondoa mfumo kandamizi na uchumi goigoi lazima yaendelee. Aluta Continua!!

Wakati tukiendelea kusubiri tafsiri na ushauri wa wanasheria, nichukue fursa hii kwa niaba ya Chama kuwataka wanachama wote mtulie katika kipindi hiki huku mkisubiri taarifa mbali mbali zitakazotolewa na Chama kupitia viongozi wenu.

Tunachukua fursa hii pia kuwapongeza mawakili wote ambao wamefanya kazi kubwa sana tangu mwanzo hadi mwisho wa kesi hii. Mawakili hao ni Stephen Mwakibolwa, Bonifasia Mapunda, Peter Kibatala, Jebra Kambole na Jeremia Mtobesya.

Asanteni na nashukuru sana!

Dorothy J. Semu,
Makamu Mwenyekiti Bara,
ACT Wazalendo.
29 Mei 2020.
 
Kama haujui ni kwamba wapo waandishi wanaoreport taarifa za Mahakama zote tz, na wanakuwa wanatambuliwa na msajili wa mahakama kwamba ni waandishi wa habari za mahakama sio kila mwandishi anaweza kuandika habari za kimahakama, hapa USA kuna waandishi wanaitwa Judiciary Journalism.
Hapa Tanzania tunaye Godfrey Monyo wa ITV!
 
Hukumu ishajulikana. Hapo hawataki updates za kama ile hukumu ya kina Mbowe
 
Kama haujui ni kwamba wapo waandishi wanaoreport taarifa za Mahakama zote tz, na wanakuwa wanatambuliwa na msajili wa mahakama kwamba ni waandishi wa habari za mahakama sio kila mwandishi anaweza kuandika habari za kimahakama, hapa USA kuna waandishi wanaitwa Judiciary Journalism.
Mzee wa USA samahani kidogo, hivi waandishi wanaitwa Judiciary Journalism au Judiciary Journalists, samahani lakini kukuuliza maana nyie wenzetu mmeishi sana huko na ndio lugha zenu hizi. Sisi tunababia babia tu
 
Leo majira ya saa 2;30 Asubuhi inatarajiwa kusomwa hukumu ya kesi inayomkabili kiongozi wa ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma mjini ZITTO KABWE ambapo kwa wale ambao tumekuwa tukifuatilia kesi hiyo kwa karibu kuanzia kufunguliwa mashtaka usikilizwaji wa mashahidi hatuna budi kusema nafasi ya ZITTO kuchomoka ni asilimia 5 TU.

Ikumbukwe katika kesi hiyo ZITTO anashtakiwa kwa uchochezi kupitia kauli hii aliyoitoa kwenye mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu ugomvi kati ya jeshi la polisi na jamii ya wafugaji

"Watu ambao walikuwa ni majeruhi katika tukio la mapambano baina ya wananchi na Poilisi, wakiwa wamekwenda hospitali kupata matibabu katika kituo cha afya Nguruka, Polisi wakapata taarifa kuwa kuna watu wanne wamekwenda hospitali kituo cha afya Nguruka kupata matibabu wakawafuata kule wakawaua.

kwa nini sioni ZITTO AKICHOMOKA

Ugumu wa kuthibitisha kisayansi, kifo cha watu hao (wanne) kilisababishwa na Polis
i na sio Magonjwa mengine endapo ni kweli watu hao walikufa. Katika utetezi wake ZITTO alikuwa na mlima mkubwa sana wa kudhibitisha kwamba ni kweli hao watu waliuawa na Polisi,. Hapa ili awe salama alihitajika kuleta ushahidi wa kuthibitisha pasi na shaka ambao ni postmortem za maiti unaothibitisha kwamba waliuawa polisi.

ZITTO kwenye hili hana UJANJA zaidi ya KUIOMBA MAHAKAMA MSAMAHA kwamba kama binadamu alipotoka hivyo apunguziwe adhabu. Wapo wanaopenda ZITTO aendelee kubaki uraiani laikini HISIA hazina nafasi dhidi ya SHERIA.
 
Zito anapenda kuvunja sheria

Uwongo wake na upotoshaji ndio umemfikisha pale

Alikuwa anafurahisha watu mitandaoni amebaki peke yake
 
Ushauri wako umeutoa kwa kuchelewa.

Wakati huu wa Corona adhabu inayopendekezwa ni kulipa faini siyo kifungo!
 
Wacha ale mvua ili ajifunze kusema ukweli, mambo ya kutengeneza taifa la waongo ni hatari sana katika mustakabali wa taifa, Kuna mwingine juzi tu kasema eti aliongea uongo juu ya kinana, sasa kama tunatengeneza wanasiasa wa hivi si itakuwa hatari sana?

Aliwahi kutwambia dream liner kuwa ni terrible tins, mara ni nzee, bombadier pia ni nzee, lakini mpaka sasa hajasema tena kama ni terrible pia kama ni nzee au mpya

Mtu wa namna hii ni bora awe jera tu akajifunze ukweli.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom