Mahakama yamtia hatiani Zitto Kabwe katika kesi yake ya Uchochezi. Atakiwa kutotoa matamshi ya Uchochezi kwa mwaka 1. Asema kukata Rufaa

*TAARIFA KWA UMMA*
...
Muda mfupi uliopita, nimeongea na Kiongozi wetu na amenihakikishia kuwa yupo imara na kamwe hukumu hii haitamrudisha nyuma. Mapambano ya kuondoa mfumo kandamizi na uchumi goigoi lazima yaendelee. Aluta Continua!!
....
*Dorothy J. Semu,*
*Makamu Mwenyekiti Bara,*
*ACT Wazalendo.*
*29 Mei 2020.*

Tunasubiri maelezo ya kina na ushahidi usio na mashaka kuhusu mfumo kandamizi na uchumi goigoi ili kama ni kuwaunga mkono tufanye hivyo.
 
"Kiongozi wetu na amenihakikishia kuwa yupo imara na kamwe hukumu hii haitamrudisha nyuma. Mapambano ya kuondoa mfumo kandamizi na uchumi goigoi lazima yaendelee. Aluta Continua!!"

kwa hiyo ndio sababu inayomfanya atoe matamshi ya kichochezi?
Ndiyo maana alibeba saaana UDSM na kumaliza kwa taabu sana. Hawa wametumika mpaka wamesahau waongee kipi.
 
mbona mashavu yamefula au macho yangu yanahitaji mchicha kwa wingi? ukiongea sana uzushi mashavu hufula
 
*TAARIFA KWA UMMA*

Chama cha ACT Wazalendo kimepokea kwa mshtuko taarifa ya kutiwa hatiani kwa Kiongozi wa Chama Ndugu Zitto Zuberi Ruyagwa Kabwe ambaye alishitakiwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkaazi Kisutu na kukabiliwa na mashtaka matatu chini ya Sheria ya Vyombo vya Habari.

Kwa mujibu wa hukumu iliyosomwa leo na Hakimu Huruma Shaidi, Ndugu Zitto ametiwa hatiani kwenye makosa yote matatu na kuachiwa huru kwa sharti la kutotoa matamshi ya kichochezi katika kipindi cha mwaka mmoja.

Ndugu Wananchi na Wanachama wa ACT Wazalendo, kwa sasa itoshe tu kusema kuwa Chama cha ACT Wazalendo kinapokea na kuyaheshimu maamuzi ya Mahakama ya Hakimu Mkaazi Kisutu yaliyotolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi na kwamba kwa sasa Chama kinasubiri kupokea ushauri wa mawakili wa Ndugu Zitto Kabwe kuhusu tafsiri ya hukumu hiyo na hatua sahihi za kuchukua.

Muda mfupi uliopita, nimeongea na Kiongozi wetu na amenihakikishia kuwa yupo imara na kamwe hukumu hii haitamrudisha nyuma. Mapambano ya kuondoa mfumo kandamizi na uchumi goigoi lazima yaendelee. Aluta Continua!!

Wakati tukiendelea kusubiri tafsiri na ushauri wa wanasheria, nichukue fursa hii kwa niaba ya Chama kuwataka wanachama wote mtulie katika kipindi hiki huku mkisubiri taarifa mbali mbali zitakazotolewa na Chama kupitia viongozi wenu.

Tunachukua fursa hii pia kuwapongeza mawakili wote ambao wamefanya kazi kubwa sana tangu mwanzo hadi mwisho wa kesi hii. Mawakili hao ni Stephen Mwakibolwa, Bonifasia Mapunda, Peter Kibatala, Jebra Kambole na Jeremia Mtobesya.

Asanteni na nashukuru sana!

*Dorothy J. Semu,*
*Makamu Mwenyekiti Bara,*
*ACT Wazalendo.*
*29 Mei 2020.*
Hiyo hukumu ni ndogo mno....mshenzi huyo amefanya visa vingi sana....mahakama ingemgonga na faini

Zito amepotosha mengi
Zito amechonganisha sana
Zito anahujumu taifa
 
Hiyo hukumu ni ndogo mno....mshenzi huyo amefanya visa vingi sana....mahakama ingemgonga na faini

Zito amepotosha mengi
Zito amechonganisha sana
Zito anahujumu taifa
Iwapo mhukumiwa na wafuasi wake wataamini ni adhabu ndogo, watakuwa wanajidanganya. Kwa mtu aliyezoea kuropokaropoka, kama Zitto, adhabu hiyo ni kubwa sana.

Ni dhahiri hukumu hiyo imefungua ukurasa mpya nchini. Ni funzo tosha kuwa kila mtu anawajibika kupima uzito wa mawazo/maoni yake kabla ya kutamka. Kwamba uhuru wa mawazo una mipaka na haki uambatana na wajibu, kama inavyotakiwa katika Katiba ya JMT (1977).

Ibara ya 30(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.
 
Kwa mujibu wa hukumu iliyosomwa leo na Hakimu Huruma Shaidi, Ndugu Zitto ametiwa hatiani kwenye makosa yote matatu na kuachiwa huru kwa sharti la kutotoa matamshi ya kichochezi katika kipindi cha mwaka mmoja.
Mimi si mwanasheria lakini naona mtego hapo-kwani anae amua kuwa mtu amefanya uchochezi ni polisi, dpp na hakimu bahati uchochezi ni kama urembo,mrembo kwangu kwako anaweza kuwa si mrembo. Hivyo Zitto atafuatiliwa na wakiona inabidi basi ataambiwa mchochezi. Kazi moja ya upinzani ni kuibua udhaifu wa watawala na kwa Tanzania inaonekana ukiupiga utawala za uso unakuwa mchochezi.
 
Mkuu, hili ni kosa kubwa sana kwa hakimu. Kuna kupatikana na hatia au kutopatikana na hatia. Kama Zitto hakuwa na hatia ilikuwa inatosha kumwachia. Kosa lingine atalofanya Zitto halipaswi kuhusishwa kwa namna yoyote na shitaka hili ambalo hakukutwa na hatia.

Tuna au majaji wanasiasa au wanaotoa hukumu za hisia.
Mkuu kama haujui Mahakama wengi wa kisutu ni threat sana kwa regime hii.
 
Mimi si mwanasheria lakini naona mtego hapo-kwani anae amua kuwa mtu amefanya uchochezi ni polisi, dpp na hakimu bahati uchochezi ni kama urembo,mrembo kwangu kwako anaweza kuwa si mrembo. Hivyo Zitto atafuatiliwa na wakiona inabidi basi ataambiwa mchochezi. Kazi moja ya upinzani ni kuibua udhaifu wa watawala na kwa Tanzania inaonekana ukiupiga utawala za uso unakuwa mchochezi.

Tafsiri yako hiyo (maandishi mekundu) ni ya upotishaji. Wapo watu wengi wengi tu nchini, wa kila aina (elimu, jinsi, madaraka, kipato, imani ya dini, nk) wanaikosoa Serikali, ndani na nje, wanaendelea kufanya hivyo kwa uhuru kabisa. Mifano iko mingi. La msingi ni kuzingatia Ibara ya 30(1) ya Katiba ya JMT bila shurti.
 
Iwapo mhukumiwa na wafuasi wake wataamini ni adhabu ndogo, watakuwa wanajidanganya. Kwa mtu aliyezoea kuropokaropoka, kama Zitto, adhabu hiyo ni kubwa sana.

Ni dhahiri hukumu hiyo imefungua ukurasa mpya nchini. Ni funzo tosha kuwa kila mtu anawajibika kupima uzito wa mawazo/maoni yake kabla ya kutamka. Kwamba uhuru wa mawazo una mipaka na haki uambatana na wajibu, kama inavyotakiwa katika Katiba ya JMT (1977).

Ibara ya 30(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.

Hilo linajukikana, Zitto atachukua tahadhari. Lakini revolutionaries hawafikiri kama wewe. Wao wamejitoa kutetea jamii no matter what happens. Basically wako na falsafa ya Ernesto Che Guevara aliyesema;
"I would rather die standing up than to live life on my knees."

Na akaongeza;
"If you tremble with indignation at every injustice then you are a comrade of mine"

Nakuhakikishia huyo Zitto Kabwe hata bado ataendelea kufanya ukosoaji hivyo hivyo. Hata Tundu Lissu ni wa aina hiyo. Hao wamejitoa sadaka kupambana na uovu na hawajali kufa kwa ajili ya kupigania haki.

Kwani Nelson Mandelea hakufungwa jela miaka 27 kwa sheria ya kibaguzi? Na hatimaye akawakomboa wana wa Afrika Kusini kutoka utawala dhalimu wa kibaguzi.

Je Nyerere hakufunguliwa mashtaka ya uhaini kwenye Mahakama hiyo hiyo ya Kisutu na hatimaye akawa Rais wa kwanza wa Tanzania?

Utamfunga jela, utamuua lakini hata wauaji nao huwa wanakufa. Yuko wapi Iddi Amin? Yuko wapi Saddam Hussein?

Ninachoweza kuongeza ni kwamba hizi harakati za za akina Zitto Kabwe na wenzie zina nguvu sana dhidi ya watawala wadhalimu. Angalia mwenyewe mauaji yaliyofanywa na WATU WASIOJULIKANA kati ya 2016 na 2018 kama vifo vya akina Ben Saanane au Azory Gwanda ni nani waliokomaa kuvikemea kama siyo wanasiasa wa upinzani na wanaharakati wa haki za binadamu.

Na sasa hivi kumetulia hatusikii watu kutekwa na kuuliwa, haya ni matokeo ya kelele za akina Zitto Kabwe na wenzake. Hivyo vyombo rasmi vya habari vinaogopa na vinatishiwa kila leo na Dr Abbas na Mwakyembe kufutiwa leseni.

Nikuhakikishie kuwa hawa watawala wa awamu ya 5 ni waoga sana ndiyo maana wanatumia fedha nyingi kwenye security yao. Ila kumbuka kama Watanzania wote tunakuwa waoga namna hiyo hawa watu wataingia mpaka bedroom zetu wakabake wake zetu.

Tusiogope kukemea uovu kwa sababu eti watatukamata na kutuua, hata wao watakuta tu.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom