Mahakama yamtangaza Jumanne Kishimba mshindi jimbo la Kahama, James Lembeli atoa machozi

Dr.adams faida

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
1,874
3,306
Ile kesi iliyokuwa ikimkabili mbunge wa jimbo la Kahama Mjini mheshimiwa Kishimba imefikia mwisho leo baada ya kesi hiyo kuamuliwa leo asubuhi na kuwa Lembeli ametoa ushahidi ambao hauna ukweli na kuonekana ameidanganya mahakama.

Hata hivyo Lembeli alishindwa kujizuia pale machozi yalipomdondoka mbele ya mahakama baada ya kesi yake kutupiliwa mbali na kumtangaza rasmi ndg Jumanne Kibera Kishimba kuwa ndiye mbuge halali wa jimbo la Kahama mjini.
 
mzee kama yule akikulilia si unaokota makopo kweli,daaaah hizi kazi nyingine hazifai kabisa
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Daaa Babu weee!! CCM sio mama yako unalia nini Babu? Kubali yaishe! Ile kile kiburi hapana kama chama lazima wakufanyizie namna ile usirudi bungeni kamwe! Jumanne hakuwa anataka ubunge lakini aliombwa apambane na wewe ili ile jeuri yako iishe! Pole san babu jipange tu na ukawa!
 
  • Thanks
Reactions: R.B
Ile kesi iliyokuwa ikimkabili mbunge wa jimbo la kahama mjini mheshimiwa Kishimba imefikia mwisho leo baada ya kesi hiyo kuamuliwa leo asubuhi na kuwa lembeli ametoa ushahidi ambao hauna ukweli nakuonekana ameidanganya mahakama...
Hata hivyo lembeli alishindwa kujizuia pale machozi yalipomdondoka mbele ya mahakama baada ya kesi yake kutupiliwa mbali na kumtangaza rasmi ndg jumanne kibera kishimba kuwa ndiye mbuge halali wa jumbo la kahama..
KATA RUFANI HIGH COURT JUDGES SI WA KUWAAMINI SANA. HASA MAJAJI WA UPE ALIOWAWEKA JK. KATA RUFANI HUKO JUU KUNA COMPETENT JUDGES
 
Inawezekana Lembeli mahakama haijamtendea haki ama hajaridhika na maamuzi. Lakini ni lazima uwe kiongozi ndio maisha yasonge mbele? Ni kipi alichosahau kwenye siasa mpaka amwage chozi kwa kukosa ubunge safari hii?
 
Ile kesi iliyokuwa ikimkabili mbunge wa jimbo la kahama mjini mheshimiwa Kishimba imefikia mwisho leo baada ya kesi hiyo kuamuliwa leo asubuhi na kuwa lembeli ametoa ushahidi ambao hauna ukweli nakuonekana ameidanganya mahakama...
Hata hivyo lembeli alishindwa kujizuia pale machozi yalipomdondoka mbele ya mahakama baada ya kesi yake kutupiliwa mbali na kumtangaza rasmi ndg jumanne kibera kishimba kuwa ndiye mbuge halali wa jumbo la kahama..
Lembeli apinga matokeo Mahakamani
 
wanasheria wa chadema tunawaomba mkate rufaa , hapa kuna kitu kichafu sana kinaendelea .
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Hata hivyo lembeli alishindwa kujizuia pale machozi yalipomdondoka mbele ya mahakama baada ya kesi yake kutupiliwa mbali na kumtangaza rasmi ndg jumanne kibera kishimba kuwa ndiye mbuge halali wa jumbo la kahama..

Jamani wekeni picha ikimwonyesha Lembeli akilia.Hizo picha nazipenda ninayo moja hii hapa Tundu LISU akilia

upload_2016-3-31_14-25-47.jpeg
 
wanasheria wa chadema tunawaomba mkate rufaa , hapa kuna kitu kichafu sana kinaendelea .
Wanasheria karibia wote wa chadema nguvu nyingi waliziweka kwa upande wa wenje na kafurila mi naona huku lembeli alikuwa hana wa kumsimamia..
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Back
Top Bottom