Mahakama yamtaka Zitto kueleza sababu za kutofika Mahakamani jana

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imemtaka Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, anayekabiliwa na kesi ya uchochezi pamoja na wadhamini wake, kufika mahakamani kujieleza kwa nini hawakufika kwenye kesi jana.

Kadhalika Mahakama imemwonya shahidi wa kwanza Mrakibu Msaidizi (ASP) Shamila Mkoma, kufika mahakamani hapo Aprili 9, mwaka huu, kutoa ushahidi dhidi ya mshtakiwa huyo.
Amri hiyo ilitolewa jana na mahakama hiyo iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.
Wakili wa Serikali Wankyo Simon, alidai kuwa kesi hiyo ilipangwa kuanza kusikilizwa ushahidi na Jamhuri imeita shahidi mmoja, ASP Mkoma. Hata hivyo, alidai kuwa mshtakiwa hayupo mahakamani.

Wakili wa utetezi, Steven Mwakibolwa, alidai kuwa amepata taarifa kutoka kwa shemeji wa mshtakiwa, Vicent Kasala, kwamba Zitto ni mgonjwa lakini hafahamu mahali alipo.

"Kasala amenieleza kwamba mkewe Zitto kampigia kumfahamisha kwamba ni mgonjwa, lakini hajui yuko wapi," alidai Mwakibolwa.
Hakimu alihoji wakili amepewa taarifa kwamba mshtakiwa ni mgonjwa lakini hana uhakika.
"Umepewa taarifa kwamba mshtakiwa anaumwa, lakini huna uhakika. Tusitafutane maneno hapa, siku ya kesi wadhamini na mshtakiwa waje hapa mahakamani kujieleza kwa nini hawakufika mahakamani," alisema Hakimu Shaidi.

Alisema kesi hiyo itaanza kusikilizwa ushahidi wa Jamhuri Aprili 9, mwaka huu na shahidi afike siku hiyo. Awali, upande wa Jamhuri ulidai kuwa unatarajia kuita mashahidi 15 na kuwasilisha vielelezo vitatu kuthibitisha kesi yao dhidi ya Zitto.

Katika kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa Oktoba 28, mwaka jana, akiwa katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Makao Mkuu ya ofisi za Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto alitoa maneno ya uchochezi yenye kuleta hisia ya hofu na chuki.

Ilidaiwa kuwa Zitto alinukuliwa kuwa: "Watu ambao walikuwa majeruni katika tukio la mapambano baina ya wananchi na polisi wakiwa wamekwenda hospitalini kupata matibabu katika kituo cha afya Nguruka, polisi wakapata taarifa kuwa kuna watu wanne wamekwenda hospitali kituo cha afya Nguruka kupata matibabu wakawafuata kule wakawaua."

Upande wa Jamhuri ulidai kuwa mshtakiwa alizidi kunukuliwa kuwa: "Lakini tumefuatilia kwa kina jambo hili, taarifa ambazo tumezipata kutoka kijijini Mpeta, Nguruka Uvinza ni mbaya. Ni taarifa ambazo zinaonyesha wananchi wengi sana wameuawa na Jeshi la Polisi, pamoja na kwamba Afande Sirro amekwenda kule, halijatoa taarifa yoyote kuhusu wananchi. Kama hawa Wanyantuzu walivamia eneo la ranchi, kuna taratibu za kisheria za kuchukua na si kuwaua, wananchi wengi sana wamekufa."

Ilidaiwa kuwa, Zitto aliendelea kuwahimiza wananchi kwa kusema: "Tumekuwa tukifuatilia kwa kina yanayojiri yote huko Uvinza tunasikitika kusema kuwa taarifa tunazozipata kutoka Uvinza zinaogofya mno kwa kuwa tunaambiwa kuwa wananchi zaidi ya 100 wa kabila la Wanyantuzu wamepoteza maisha kwa kupigwa risasi na polisi, wengine wakisemwa kuuawa hata wakiwa kwenye matibabu hospitalini baada ya kujeruhiwa kwenye purukushani na Jeshi la Polisi."

Wankyo alidai kuwa maneno hayo si tu yalichochea chuki bali pia yalitengeneza uhasama kwenye mamlaka halali na kusababisha mijadala miongoni mwa makundi mbalimbali katika jamii na kwenye mitandao na vyombo vya habari kwa ujumla.

Pia alidai kuwa maneno hayo yaliwafanya watu wafikirie kuwa serikali haiwajali raia wake.
Zitto aliposomewa mashtaka yake alikana na yuko nje kwa dhamana.

IPP
 
Ndugu zangu,

Siku ya jana jumatatu tarehe 10-03-2019 Zitto Kabwe alitakiwa kufika mahakamani kuhudhuria kesi kama alivyoagizwa na mahakama.

Ajizi nyumba ya njaa badala ya kutoa sababu zenye mashiko baada ya Mh.Hakimu kuuliza alipo Zitto wakili wake alimwelekeza shemeji wa Zitto kutoa sababu za kutohudhuria.

Shemeji wa Zitto aliieleza mahakama kwamba ''nimepigiwa simu na dada nije mahakamani kueleza kuwa shemeji Zitto anaumwa ila sijui anaumwa nini?"

Bila shaka Zitto anatamani kunyimwa dhamana ili akaishi rumande pande za Segerea.

Tafiti chache zilizofanyika zimeonesha kitendo cha wanasiasa kukaa lupango hakijawasaidia kupata umaarufu zaidi ya kupuuzwa na wananchi.

Nimalize tu kwa kusema "mtoto akililia wembe apewe".

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmeisha anza jitokeza kuchochea moto sijui mahakimu aina ya mashauri bado wapo kisutu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu zangu,

Siku ya jana jumatatu tarehe 10-03-2019 Zitto Kabwe alitakiwa kufika mahakamani kuhudhuria kesi kama alivyoagizwa na mahakama.

Ajizi nyumba ya njaa badala ya kutoa sababu zenye mashiko baada ya Mh.Hakimu kuuliza alipo Zitto wakili wake alimwelekeza shemeji wa Zitto kutoa sababu za kutohudhuria.

Shemeji wa Zitto aliieleza mahakama kwamba ''nimepigiwa simu na dada nije mahakamani kueleza kuwa shemeji Zitto anaumwa ila sijui anaumwa nini?"

Bila shaka Zitto anatamani kunyimwa dhamana ili akaishi rumande pande za Segerea.

Tafiti chache zilizofanyika zimeonesha kitendo cha wanasiasa kukaa lupango hakijawasaidia kupata umaarufu zaidi ya kupuuzwa na wananchi.

Nimalize tu kwa kusema "mtoto akililia wembe apewe".

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa wewe ndio hakimu au ndio msemaji wa mahakama wacha ulimbukeni .
 
Kuna Hakimu pale Kisutu amelalamika kesi ya watuhumiwa wa uhujumu uchumi inamtesa coz kila siku mawakili wa Serikali wanadai upepelezi haujakamilika ila vielelezo vinaonesha upelelezi ulikamilika mwaka 2017.

Kesi ya maana zinawashinda mnakomaa na wapinzani tu.
KONOIKE washawaliza huko Ng'ambo.
Tuna mawakili wa ajabu sana. kesi wanazojua hawawezi kushinda wanang'ang'ania upelelezi kutokamilika au kuomba washtakiwa wanyimwe dhamana ili wasote.

nchi inaendesha kwa ubabe wakizamani sana aisee.
 
Hivi mahaba yako kwa Zitto hayajaisha tu??
nakukumbuka Shonza toka enzi zile za ile story ya kutembea na sumu mfukoni.
 
kuna hakimu pale Kisutu amelelemika kesi ya watuhumiwa wa uhujumu uchumi inamtesa coz kila siku mawakili wa Serikali wanadai upepelezi haujakamilika ila vielelezo vinaonesha upelelezi ulikamilika mwaka 2017.

Kesi ya maana zinawashinda mnakomaa na wapinzani tu.
KONOIKE washawaliza huko Ng'ambo.
Tuna mawakili wa ajabu sana. kesi wanazojua hawawezi kushinda wanang'ang'ania upelelezi kutokamilika au kuomba washtakiwa wanyimwe dhamana ili wasote.

nchi inaendesha kwa ubabe wakizamani sana aisee.
Soma tena kisha urejee kwenye hoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwenyewe nimeliona hili,Anapita mulemule alimopita Mbowe. Uzuri wa utawala huu hakuna anayeweza kuwa juu ya serikali.

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
Ndugu zangu,

Siku ya jana jumatatu tarehe 10-03-2019 Zitto Kabwe alitakiwa kufika mahakamani kuhudhuria kesi kama alivyoagizwa na mahakama.

Ajizi nyumba ya njaa badala ya kutoa sababu zenye mashiko baada ya Mh.Hakimu kuuliza alipo Zitto wakili wake alimwelekeza shemeji wa Zitto kutoa sababu za kutohudhuria.

Shemeji wa Zitto aliieleza mahakama kwamba ''nimepigiwa simu na dada nije mahakamani kueleza kuwa shemeji Zitto anaumwa ila sijui anaumwa nini?"

Bila shaka Zitto anatamani kunyimwa dhamana ili akaishi rumande pande za Segerea.

Tafiti chache zilizofanyika zimeonesha kitendo cha wanasiasa kukaa lupango hakijawasaidia kupata umaarufu zaidi ya kupuuzwa na wananchi.

Nimalize tu kwa kusema "mtoto akililia wembe apewe".

Sent using Jamii Forums mobile app
Ugonjwa Ni Siri ya mgonjwa na daktari

TAFITI AMEFANYA NANI? MATOKEO YALITOKA LINI ?

SEMA "MANENO YA MTAANI YANAONEASHANKUKAA LUPANGO WAPINZANI HAKUJAWAHI KUWASAIDI" NA SIO TAFITI.
 
Mfutieni dhamana viwanda viongezeke ,dola ipande thamani na hali ya maisha iboreke au vipi kijani .
 
Back
Top Bottom