Mahakama yampinga diwani wa TLP aliyeshinda

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,187
671
Mahakama yampinga diwani wa TLP aliyeshinda

2007-10-14 09:39:47
Na Thobias Mwanakatwe, PST, Mbeya


Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Mbeya imetoa amri ya kutaka diwani wa Kata ya Nankupwe kupitia Chama cha TLP, aliyetangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwa amepita bila kupingwa asipewe madaraka yo yote ya udiwani katika kata hiyo.

Aidha mahakama hiyo pia imetoa amri ya kuzuia kufanyika kitu cho chote kinachohusu uchaguzi katika kata hiyo hadi shauri la msingi lililofunguliwa na mgombea wa CCM katika kata hiyo, Bw. Bosco Saines litakapotolewa ufumbuzi na mahakama.

Hukumu hiyo ilitolewa na mahakama hiyo juzi ambapo mgombea wa TLP, Bw. Lucas Tula aliyepita bila kupingwa ameamriwa asipewe madaraka ya uongozi katika kata hiyo mpaka shauri la msingi lililofunguliwa na mgombea wa CCM, Bw. Saines Nyembe litakapomalizika.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, Bw. M. M. Siyani akitoa uamuzi huo juzi, alidai mahakama imeamua kutoa hukumu hiyo kufuatia mgombea wa CCM kuomba amri ya mahakama isimamishe shughuli zozote za uchaguzi katika kata hiyo kutokana na uchaguzi huo kugubikwa na utata.

Hatua ya mgombea wa CCM kuamua kufungua kesi hiyo inafuatia kubainika kuwa fomu za mgombea wa TLP zilikuwa na mapungufu kwa sababu hakuwa na wadhamini wa kutosha kama taratibu za uchaguzi zinavyoelekeza.

Katika kesi hiyo ya madai namba 36/2007 ambayo mlalamikiwa namba moja ni mgombea wa TLP, mgombea huyo wa CCM pia amemshitaki Msimamizi wa Uchaguzi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Chunya pamoja na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Ofisa Mtendaji kata ya Nankupwe.

Taarifa ambazo PST imezipata kutoka Tume ya Uchaguzi inadaiwa kuwa kati ya wadhamini 25 waliojitokeza kumdhamini mgombea wa TLP asilimia kubwa ya wadhamini hao wameweka sahihi za kidole gumba hatua ambayo pia imeleta mashaka kwa tume hiyo.

Uchaguzi huo mdogo uliofanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani wa CCM, umekumbwa na utata mkubwa ambapo inadaiwa Msimamizi wa Uchaguzi aliamua kumtangaza mgombea wa TLP kwamba amepita bila kupingwa hatua iliyopingwa na mgombea wa CCM ambaye aliamua kwenda mahakamani kuomba amri ya mahakama ya kumzuia diwani huyo kufanya kazi zake hadi hapo kesi ya msingi itakapomalizika.

Utata katika uchaguzi huo unafuatia Msimamizi Msaidizi wa uchaguzi ambaye ni Ofisa Mtendaji kata ya Nankupwe kudaiwa kumpa tarehe tofauti ya kurejesha fomu za uteuzi mgombea wa CCM kwamba siku ya kurudisha fomu ni Oktoba 3 wakati tarehe ya kurudisha iliyokuwa imepangwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni Oktoba 2 mwaka huu.

SOURCE: Nipashe
 
Hukumu hiyo ilitolewa na mahakama hiyo juzi ambapo mgombea wa TLP, Bw. Lucas Tula aliyepita bila kupingwa ameamriwa asipewe madaraka ya uongozi katika kata hiyo mpaka shauri la msingi lililofunguliwa na mgombea wa CCM, Bw. Saines Nyembe litakapomalizika.


Kumbe sio kura zilizopigwa, haya!
maana makelele yaushindi tulioyaona hapa ndio hivyo tena!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom