Mahakama Yamkuta "Scorpion" Na Kesi Ya Kujibu

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,251
scorpion.jpg

Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemkuta mshtakiwa Salum Njwete, maarufu kwa jina la ‘Scorpion’ anayekabiliwa na shtaka la unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi ana kesi ya kujibu na anatarajiwa kuanza kujitetea, Novemba 14, mwaka huu.

Uamuzi huo umetolewa leo Oktoba 31/2017 na Hakimu Mkazi Flora Haule wa mahakama hiyo baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na zaidi ya mashahidi kumi walioletwa mahakamani pale na upande wa Mashtaka.

Kabla ya kutolewa uamuzi huo, Hakimu Haule alimkumbushia mshtakiwa mashtaka yake.

Baada ya uamuzi huo kutolewa, mshtakiwa Scorpion amedai kuwa atajitetea kwa kiapo na pia atakuwa na mashahidi wawili ambao walitoa ushahidi upande wa mashtaka.

Hata hivyo, upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili Ester Kyala ulipinga hoja hiyo na kudai kuwa mshtakiwa huyo hawezi kutumia mashahidi ambao wamekwisha toa ushahidi wao kwa upande wa Jamhuri na kama anaweza atafute mashahidi wengine.

Kutokana na pingamizi hilo Scorpion amedai atajitetea mwenyewe na pia akaomba mahakama itumie pia ushahidi wa wale mashahidi wawili.

Kufuatia hayo kesi hiyo imeahirishwa hadi November 14 mwaka huu. Mshtakiwa amerudishwa rumande kwa kuwa makosa anayoshtakiwa nayo hayana dhamana.

Katika kesi hiyo, Njwete anakabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni unyang’anyi wa kutumia silaha na kumjeruhi Said Mrisho kwa kumchoma kisu sehemu mbalimbali za mwili zikiwemo, tumboni na mabegani na kisha kumtoboa macho kitendo anachodaiwa kutenda Septemba 6, mwaka jana katika eneo la Buguruni Sheli, jijini Dar es Salaam.

Pia, anadaiwa kumwibia mali yenye thamani ya Sh 476,000/-.


Chanzo: Mpekuzi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom