Mahakama yakerwa kesi kuahirishwa mara kwa mara

Konaball

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
2,950
2,000
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, imeelezea kukerwa na tabia ya kuahirisha mara kwa mara kwa kesi ya madai inayowahusisha wafanyabiashara maarufu jijini Reginald Mengi na Yusuf Manji.
Kesi hiyo namba 91 ya mwaka 2006 iliyofunguliwa na Mengi ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP na imekuwa ikiahirishwa mara kwa mara.Kuahirishwa huko kunadaiwa kufanywa na Manji ambaye ni mlalamikiwa katika kesi hiyo, kufuatia kile kilichoeleza kuwa ni kubadilisha mawakili.

Hadi sasa Manji ameshabadili mawakili mara sita, lakini safari hii amekuja na nguvu ya ajabu baada ya kuajiri jopo la mawakili watano ambao wote isipokuwa mmoja, ni mawakili maarufu na wenye majina makubwa nchini.
Lakini wakati Manji akiwa na nguvu kubwa kiasi hicho cha kuajiri jopo la mawakili wazito kama hao, Mengi kwa upande wake anawakilishwa na wakili mmoja tu.
Kitendo hicho cha Manji kubadili mawakili kila mara kimekuwa kikikwamisha kuendelea kwa kesi hiyo kwa kuwa kila wakili mpya anapopewa kuendesha kesi hiyo, amekuwa akiomba iahirishwe ili apate muda wa kutosha kupitia jalada la kesi.

Akizungumzia kitendo cha mawakili wa upande wa mdaiwa kubadilishwa mara kwa mara nje ya mahakama, Wakili wa Mengi, Michael Ngalo, alisema hiyo ni mbinu ya mlalamikiwa kuchelewesha kesi.
Hali si tu kwamba ilionekana kero kwa upande wa mlalamikaji lakini pia kwa upande wa mahakama kiasi kwamba Jaji John Utamwa, anayeisikiliza kesi hiyo jana alilazimika kuizungumzia hali hiyo na kutoa tahadhari za kuendelea kwa kitendo hicho.
Wakati kesi hiyo ilipofika mbele ya Jaji Utamwa kwa ajili ya usikilizwa, mtaalam huyo wa sheria, alitoa mtiririko kuhusu namna kesi hiyo inavyoahirishwa mara kwa mara na sababu kubwa ikiwa ni kubadilishwa kwa mawakili wa upande wa mlalamikiwa.

Manji alianza na wakili mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Rattansi, na kufuatiwa na Rutashoborwa na baadaye Jamal.
Jamal alifuatia Yuda Tadei na Rattansi ambao hata hivyo hawakudumu na kisha kubadilishwa na jukumu hilo kukabidhiwa kwa Marando na wenzake wanne.
Pamoja na Marando, mawakili wengine ni Richard Rweyongeza ambaye alikodishwa na serikali katika kesi dhidi ya Mbunge wa Bariadi Magharibi Andrew Chenge.

Anakumbukwa pia katika kesi ya mgombea Binafsi.
Hali kadhalika, Dk. Ringo Tenga ambaye pia ni Mhadhiri wa Sheria katia Chuo Kikuu cha Dar es Salaa, ndugu yake Curthbet Tenga na Tausi Abdallaha ambao wote wanatoka kampuni ya Law Associates Advocates.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom