Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Moshi. Mlalamikaji wa kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa Jimbo la Vunjo, Augustino Mrema wa TLP, jana alikwaa kisiki mahakamani baada ya vielelezo vyake viwili kukataliwa.
Mrema ambaye anapinga ushindi wa Mbunge, James Mbatia wa NCCR-Mageuzi katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika nchini Oktoba 25, mwaka jana ndiye shahidi wa kwanza katika kesi hiyo iliyoanza kusikilizwa jana.
Vielelezo vilivyokataliwa kupokelewa na Jaji Lugano Mwandambo baada ya mawakili wa utetezi kuweka pingamizi ni pamoja na karatasi ya mfano wa kura iliyodurufiwa na karatasi ya mfano wa kura.
Akitoa uamuzi huo mdogo mbele ya Wakili Mkuu wa Serikali, Mark Muluambo akisaidiana na Lilian Machange, Jaji Mwandambo alisema vielelezo hivyo siyo nakala halisi kama alivyosema kwenye hati ya kiapo chake.
Alisema sababu zilizotolewa na upande wa mawakili wa upande wa mlalakiwa wa kwanza, wa pili na wa tatu kwamba vielelezo hivyo havina mashiko kisheria ni sahihi kwa sababu siyo hati halisi.
Jaji alisema vielelezo hivyo pia havikuwa na muhuri wa kisheria kama vielelezo vilivyokuwa katika maombi yao ya awali, jambo lililosababisha kushindwa kupokelewa kama kielelezo mahakamani hapo. Mlalamikiwa wa kwanza, anatetewa na Wakili Mohamed Tibanyendera akisaidiana na Youngsavier Msuya na Fey Sadala, huku Wakili January Mkobogho akimtetea Mrema.
Kesi ya Wenje kuendelea leo
Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Jimbo la Nyamagana, itaendelea kusikilizwa leo kwa upande wa utetezi kujibu hoja za upande wa mdai za kuomba Mahakama iwaruhusu mashahidi wake watumie fomu namba 21 B wakati wa kutoa ushahidi wao.
Shauri namba tatu la 2015 la kupinga matokeo ya uchaguzi lilifunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo Chadema, Ezekiah Wenje akipinga ushindi wa Stanslaus Mabula wa CCM katika Uchaguzi Mkuu.
Akiwasilisha hoja hiyo mbele ya Jaji wa Kanda ya Sumbawanga, Kakusilo Sambo anayesikiliza shauri hilo katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Wakili wa mleta maombi, Deya Outa, jana alidai kuwa alikuwa na kielelezo cha fomu 21B 646, lakini fomu moja ilikataliwa wakati shahidi wa tatu (Wenje) alipokuwa akitoa ushahidi wake na kubakia na fomu namba 645 ambayo haiwezi kutumika pasipo kibali maalumu cha Mahakama.
Alidai licha ya Mahakama kukataa kuzipokea fomu hizo kwasababu zilichelewa, lakini alikuwa ameshawapatia wajibu maombi tangu Januari 29 na Machi 11, mwaka huu ili wakazipitie.
“Tunaomba fomu hizo ziruhusiwe kutumika kwa sababu watakuja mashahidi wenyewe, wataulizwa maswali kuhusu fomu hizo,” alidai.
Wakili wa mjibu maombi wa kwanza, Constantine Mutalemwa aliiomba Mahakama kupewa siku mbili za kupitia vifungu mbalimbali vya sheria ili waweze kujibu maombi hayo kwa ufasaha.
Hata hivyo, licha ya Jaji Sambo kukubaliana na ombi la wajibu maombi kupewa muda wa kujiandaa kujibu hoja hizo, aliwakatalia kutumia siku mbili akisema hakuna kitu kipya kwenye kesi hiyo na wote wanafahamu kinachoendelea.