Mahakama yaingilia Bunge kuzuia suala la Escrow lisijadiliwe!

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,985
20,263
Asubuhi niliwaeleza kuwa serikali ya CCM kupitia Mwanasheria mkuu na Waziri mkuu wapo kwenye mchakato mkubwa wakuzuia ripoti ya wizi wa Escrow isijadiliwe na bunge.

Sasa, jioni hii baada tu ya kuahirishwa bunge kiutatanishi, na kikao cha UKAWA kuisha, Katibu mkuu kiongozi Ombeni Sefue amewasilisha rasmi barua ya mahakama inayozuia mjadala wowote wa Esrow account katika bunge hili,

Ujio wa Sefue Bungeni na barua hii umetafsiriwa kuwa ofisi kuu nchini inatambua na kwa mamlaka iliyonayo imeinjinia kile kinachoitwa zuio la mahakama dhidi ya wizi huu unaotikisa nchi.

UPDATE:
- Ndugu James Lembeli amesema taasisi zinazoaminika hapa nchini ni BUNGE na JESHI la wananchi tuu.

Kwa maneno haya CCM wanakubali kuwa taasisi ya urais haiaminiki TENA. kumbuka LEMBELI ni kigogo wa CCM, na pia rais ni mojawapo ya taasisi hapa nchini

- Lissu ametaka kama Barua ipo, iletwe na Jaji aliyeandika barua hiyo ajadiliwe Bungeni.

- Zitto anasema kuwa Suala hili linachora mstari wa uvumilivu wa watanzania kwa Serikali
- Zitto anasema jambo hili (kuzuia Bunge lisifanye kazi yake) linaweza kutokea kwenye nchi isiyokuwa na Dola
- Zitto anasema umefanywa kila ubabe, kila aina ya maneno/matusi kuhakikisha suala hili halijadiliwi Bungeni lakini njia pekee ya kulimaliza hili ni kuwa na mjadala wa wazi Bungeni.
- Zitto anasema PAC ipo tayari wakati wowote watapohitajika kuwasilisha ripoti Bungeni watapohitajika. Anataka wanaotaka kupinga suala hili wasubiri ziletwe facts
- Waziri Mkuu, Mizengo Pinda anasema Mihimili Mitatu yote ipo kwa mujibu wa Katiba. Anasema ameogopa kuona Bunge likidai Mahakama inajaribu kuficha uozo
- Pinda anasema lazima busara kubwa itumike kuhakikisha maamuzi yanayofanywa na Bunge yasionekane kuingilia Mhimili mwingine (Mahakama) hivyo ni jukumu la Spika kutumia busara kila Mhimili unatekeleza jukumu lake inavyotakiwa (ANAZOMEWA)
- Ndugai anasema wao Wabunge kama viongozi hawawezi kuwa na umoja katika kutetea maovu. Anasema hekima itatumika
- Ndugai anasema haki itatendwa na Bunge, ushauri wa Pinda umepokelewa

James-Mbatia-November20-2014.jpg

Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), James Mbatia (kulia) akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana kuhusu madai kuwa Mahakama Kuu ya Tanzania imeandika barua ya kuzuia wabunge kujadili kashfa ya ITPL. Kushoto ni Mshauri wa Masuala ya Kisheria wa umoja huo, Tundu Lissu.Picha/ Omar Fungo

Mkanganyiko mkubwa umeibuka mjini hapa kwamba serikali inafanya kila njia kuzuia taarifa ya sakata la IPTL la uchotwaji wa zaidi ya Sh. bilioni 300 katika akaunti ya Escrow iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kujadiliwa bungeni.

Habari za mkakati huo zilitangazwa jana na wabunge watatu wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), James Mbatia (NCCR-Mageuzi), Tundu Lissu (Chadema) na Mohamed Habib Mnyaa (Cuf), walipozungumza na waandishi wa habari wakidai kuwa Mahakama Kuu ya Tanzania imeandika barua kwenda ofisi za Bunge ikizuia mjadala wa sakata hilo.

Wabunge wa Ukawa waliionya Mahakama Kuu ya Tanzania, kutotumika kuzuia Bunge kujadili ufisadi kwenye akaunti ya Escrow.

Mbatia ambaye pia ni Mbunge wa Kuteuliwa na Rais, aliwaambia waandishi wa habari kuwa wamebaini mbinu za kuchelewesha au kuzuia Bunge kujadili kashfa hiyo.

Alisema hata danadana zinazoendelea katika ratiba ya shughuli za kila siku za Bunge, ikiwamo kuahirishwa kikao cha jana, kuwa ni moja ya njama za kupoteza muda ili mwishoni isemekane muda hautoshi.

Kwa msingi huo wanataka kila Mbunge apewe nakala ya ripoti hiyo, angalau kati ya siku tatu hadi nne, kabla ya Jumatano ijayo, suala hilo litakapopelekwa bungeni na PAC.

Mbatia alisema hatua hiyo itatoa nafasi kwa wabunge, kuisoma na kuielewa ili kuijadili kwa upana na kutoa uamuzi utakaofaa kwa maslahi ya taifa.

"Hii kashfa inahusisha viongozi waandamizi serikalini na tumepata taarifa za uhakika, kuna kila aina ya mbinu zinafanywa kuhujumu Bunge lisisimamie serikali katika kudhibiti matumizi ya kodi hizi za wananchi," alieleza Mbatia.

Alisema kwa uchunguzi uliyofanyika mpaka sasa, wabunge hao wameazimia kila atakayethibitika kuhusika kisiasa, kisheria au kimaadili, achukuliwe hatua stahiki sambamba na kurejesha fedha alizochukua.

Alitaka umma kufahamu kuwa kashfa hiyo iliibuliwa bungeni kabla haijaondolewa kwa ahadi iliyotolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kwamba ingerudishwa baada ya kuchunguzwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Taasisi ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Mbatia alisisitiza kuwa pamoja na ripoti ya uchunguzi kuelezea fedha zilizochotwa kwenye akaunti ya Escrow kuwa zilizotokana na kodi za wananchi, kuna zaidi ya Sh. bilioni 21 ambazo zilitakiwa zilipwe serikalini kama kodi, lakini hazikulipwa.

"Hata Katibu Mkuu Kiongozi (Balozi Ombeni Sefue) mlimsikia akikemea Bunge lisishughulikie suala hili, akituita wanasiasa, tunasema hii ni kodi ya wananchi ni lazima tuhakikishe inatumika sawasawa, ndilo jukumu letu hilo," alieleza.

Kwa mujibu wa Mbatia, watuhumiwa hao katika kashfa ya Escrow wamefika mbali zaidi kwa kufikia hatua ya kuingiza mahakama ili kuitumia kama kigingi cha kuzuia au kucheleweza mjadala huo usifanyike kama ilivyopangwa.

Aliwaonya wahusika hao, akiwataka kusoma alama za nyakati kwamba kwa sasa utulivu umekosekana bungeni, nje ya Bunge na hata serikalini na hivyo waone umuhimu wa kuacha kashfa hiyo ijadiliwe ili hatima yake ijulikane.

"Hauwezi kuacha watu kati ya watatu hadi saba hivi, wakatesa vichwa vya watu na walipa kodi wa Tanzania, hakuna uwezekano wa mahakama kuingilia mchakato wa kazi za kibunge dhidi ya kashifa ya IPTL," alieleza Mbatia.

Pia alisema kwamba wanazo taarifa kuwa serikali inajaribu kusema haina fedha, ili muda wa Bunge ufupishwe kashifa hiyo ijadiliwe kwenye vikao vya Bunge vijavyo na kwamba Ukawa haiko tayari kwa hilo kutokea.

Lengo la mpango huo lilielezwa na Mbatia kuwa ni kutaka kuchakachua ripoti hizo zilizotokana na uchunguzi wa vyombo viwili vya serikali.

"Ukawa hatuna haja ya kumkandamiza mtu, tunachotaka ni haki itendeke kwa pande zote, waliohusika kuiba na walioaibisha taifa kwa kashfa hizi wawajibike kwa mujibu wa sheria, lakini pia fedha za walipa kodi zirudishwe," alisema.

Naye Mbunge wa Iramba (Mashariki- Chadema) ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya kisheria wa Ukawa, Tundu Lissu, alisema hakuna kipengele cha sheria yoyote anayoifahamu kinachoruhusu mahakama kuingilia shughuli za Bunge na kwamba, kesi ya wizi huo katika akaunti ya Escrow ilikwisha kufanyiwa uamuzi katika Mahakama Kuu, Saa 6:00 usiku.

Alitaka mahakama ikiwa bado ina hata chembe ya kuhitaji kusitiri hadhi yake, isikubali kutumika mithili ya karatasi ya chooni.

Alisema kashfa hiyo ni kubwa na pengine kuliko ya Richmond, ambayo ilijadiliwa bungeni na uamuzi ukafikiwa kabla ya waliohusika kwa namna tofauti kuwajibika tena bungeni.

"Tumesikia kuna barua imetoka mahakamani, kwa Jaji Mkuu au Jaji Kiongozi, hatujapata hakika, lakini tumeambiwa kwamba, kuna barua imekuja kutoka mahakama ya Tanzania ikisema jambo hili liko mahakamani na kwa sababu hiyo lisijadiliwe na Bunge," alisema Lissu.

Alisema kwa mujibu wa kanuni za Bunge, hakuna mahakama au jaji, au kiongozi yeyote wa mahakama mwenye mamlaka ya kuliandikia Bunge barua, kulipangia kitu gani kifanyike au kisifanyike.

Vilevile Lissu alisema utaratibu wa aina hiyo haupo hata kwa mujibu wa Katiba ya nchi wala sheria yoyote anayoifahamu, iliyowahi kutungwa na Bunge na kwamba itawashangaza ikitokea barua ya aina hiyo iingizwe kwenye ukumbi wa Bunge kama inavyosemekana imekusudiwa.

Alitoa wito kwa wabunge wa CCM wanaochukia maovu, kushirikiana nao dhidi ya vikwazo vinavyoundwa kuzuia mkakati wa kushughulikia wezi bungeni kutekelezwa.

Hata hivyo, Lissu alisema ikitokea wakafanikiwa kuzima jitihada hizo bungeni, wana hakika hawatafaulu kuzizuia nje ya Bunge kwa kuwa dunia ni pana, watatembea kwa lengo la kuhakikisha kodi ya Watanzania inatendewa haki.

Naye Mbunge wa Mkanyageni (CUF), Mohammed Habib Mnyaa, alisema pamoja na maelezo ya Mbatia, mwenendo wa serikali unaoshuhudiwa kwa sasa, ukiwamo kuunganisha vikao viwili vya Bunge; cha 16 na 17 ni dhahiri haina nia njema ya kuridhia kashfa ya Escrow kujadiliwa bungeni.

"Tulitakiwa kukaa kwenye kamati wiki nne, tumekaa wiki mbili ikisema haina fedha tuahirishe Bunge kwa ajili hiyo, basi ni dhahiri serikali hii imeshindwa kujiendesha, kiasi cha kukosa uwezo wa kuhudumia muhimili wake wa Bunge," alieleza Mnyaa.

Msemaji wa Mahakama ya Tanzania, Mery Gwela, alipoulizwa kuhusiana na barua hiyo, alisema hana taarifa na kwa wakati huo yupo nyumbani na kushauri aulizwe Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Amir Msumi, ambaye naye hakupatikana baada ya simu yake ya kiganjani kuita bila kupokelewa. Nao viongozi wakuu wa Bunge hawakupatikana kuthibitisha kama wameipokea barua hiyo.

Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashillilah, alipotafutwa simu yake haikupokelewa kwa maelezo kutoka Kitengo cha Habari cha Bunge kuwa alikuwa kwenye kikao sambamba na Ndugai.

Hata walipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi (sms) hawakujibu hadi tunakwenda mitamboni.

Chanzo:Nipashe
 
Kwani siku hizi Executive imegeuka kuwa Judiciary? Kwa kutoa stop order kwa muhimili mwingine unaodaiwa kuwa huru kimfumo na ki uendeshaji?
Unavyosema Ikulu una maanisha taasisi au mtu?
 
Asubuhi niliwaeleza kuwa serikali ya ccm kupitia Mwanasheria mkuu na Waziri mkuu wapo kwenye mchakatp mkubwa wakuzuia ripoti ya wizi wa escrow isijadiliwe na bunge, Sasa jioni hii baada tu ya kuahirishwa bunge kiutatanishi, na kikao cha UKAWA kuisha, Katibu mkuu kiongozi Ombeni Sefue amewasilisha rasmi barua ya mahakama inayozuia mjadala wowote wa Esrow account katika bunge hili,

Ujio wa Sefue Bungeni na barua hii
umetafsiriwa kuwa ofisi kuu nchini inatambua na kwa mamlaka iliyonayo imeinjinia kile kinachoitwa zuio la mahakama dhidi ya wizi huu unaotikisa nchi.


Nimepepesa macho mpaka basi sioni barua.
Anyway lisemwaalo lipo au laja.Hivi Prof.JK kasharudi magogoni kufanya maamuzi magumu?
 
Safi sana,

Kikwete is grown up now, now He is acting like a real president.
 
UKAWA hawawezi kudeal na hii ishu kwa dhati kwa sababu kuna viongozi wawili wa upinzani wanahusishwa na ufisadi wa Escrow
 
Asubuhi niliwaeleza kuwa serikali ya ccm kupitia Mwanasheria mkuu na Waziri mkuu wapo kwenye mchakatp mkubwa wakuzuia ripoti ya wizi wa escrow isijadiliwe na bunge, Sasa jioni hii baada tu ya kuahirishwa bunge kiutatanishi, na kikao cha UKAWA kuisha, Katibu mkuu kiongozi Ombeni Sefue amewasilisha rasmi barua ya mahakama inayozuia mjadala wowote wa Esrow account katika bunge hili,

Ujio wa Sefue Bungeni na barua hii umetafsiriwa kuwa ofisi kuu nchini inatambua na kwa mamlaka iliyonayo imeinjinia kile kinachoitwa zuio la mahakama dhidi ya wizi huu unaotikisa nchi.

hizi taarifa je zimewafikia wakubwa (TUNAISHI KWA HISANI YA WAHISANI) wanaotulisha kila mwaka na mwaka huu wamesema hawatoi kitu mpaka wajue nani kabugia huo mshiko?
@:CC: CHABRUMA
 
Asubuhi niliwaeleza kuwa serikali ya ccm kupitia Mwanasheria mkuu na Waziri mkuu wapo kwenye mchakatp mkubwa wakuzuia ripoti ya wizi wa escrow isijadiliwe na bunge, Sasa jioni hii baada tu ya kuahirishwa bunge kiutatanishi, na kikao cha UKAWA kuisha, Katibu mkuu kiongozi Ombeni Sefue amewasilisha rasmi barua ya mahakama inayozuia mjadala wowote wa Esrow account katika bunge hili,

Ujio wa Sefue Bungeni na barua hii umetafsiriwa kuwa ofisi kuu nchini inatambua na kwa mamlaka iliyonayo imeinjinia kile kinachoitwa zuio la mahakama dhidi ya wizi huu unaotikisa nchi.

Mahakama haina mamlaka ya kulizuia bunge kufanya shughuli zake ikiwa ni pamoja na kujadili report ya uchunguzi wa wizi wa Escrow. Isitoshe barua ya mahakama haiwezi kupelekwa na katibu mkuu kiongozi kwani si mtendaji wa mahakama wala mtumishi wa bunge.

Kuna vitu havijakaa sawa kwenye taarifa yako kaka.
 
Kwani siku hizi Executive imegeuka kuwa Judiciary? Kwa kutoa stop order kwa muhimili mwingine unaodaiwa kuwa huru kimfumo na ki uendeshaji?
Unavyosema Ikulu una maanisha taasisi au mtu?

Aiseee hii ni shida mbona tutashaa.
 
Mtazamo wangu mahakama wako sahihi kwamba jambo hili walikuwa wameliamua wao tena mahakama kuu iweje leo bunge wajadili maamuzi ya mahakama?
 
Back
Top Bottom