Mahakama yaiamuru Serikali kurekebisha kifungu Sheria ya Mtandao

Petro E. Mselewa

Verified Member
Dec 27, 2012
9,474
2,000
Mahakama Kuu ya Tanzania iliyokuwa chini ya jopo la Majaji watatu (Profesa John Ruhangisa,Winfrida Korosso na Lugano Mwandambo) imemwondolea Mkurugenzi wa Mashtaka nchini mamlaka ya kutoa adhabu isiyokatiwa rufaa kwa mshtakiwa anayekiri makosa ya kimtandao.

Kutokana na uamuzi huo uliobatilisha kifungu cha 50 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao, Mahakama imeipa Serikali miezi 12 kukifanyia marekebisho kifungu hicho. Hatahivyo, Mahakama Kuu ya Tanzania imehalalisha vifungu vingine vyote vya Sheria hiyo ambavyo pia vimekuwa vikilalamikiwa na wadau wa matumizi ya mitandao na teknolojia ya habari.

Uamuzi huo wa Mahakama Kuu ya Tanzania umetolewa kwenye kesi ya kikatiba nambari 32 ya 2015 iliyofunguliwa na Wakili wa Kujitegemea Jebra Kambole. Wakili Msomi Kambole alikuwa akipinga vifungu vya 4,5,6,7,8,9,10,11,14,19,21,22,31,33,34,35,37,38 na 50 vilivuodaiwa kukiuka haki ya mtu kuwasiliana na haki ya mtu kusikilizwa zinazotolewa na Katiba ya nchi. Shauri hilo lilikuwa dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Chanzo: Mwananchi la leo, uk. 1 &3.

JAMII LEO

======

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ameondolewa mamlaka ya kutoa adhabu isiyokatiwa rufaa kwa mshtakiwa anayekiri makosa ya kimtandao.

Uamuzi huo umetolewa na Mahakama Kuu,umeipa Serikali miezi 12 kukifanyia marekebisho kifungu cha 50 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao kilichobatilishwa.

Hata hivyo, mahakama hiyo imehalalisha vifungu vingine vyote vya sheria hiyo, ambavyo pia vimekuwa vikilalamikiwa na wadau wa matumizi ya mitandao na teknolojia ya habari.

Uamuzi huo umetokana na kesi ya kikatiba, iliyofunguliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)na mashirika mengine.

Katika hukumu iliyotolewa na majaji Profesa John Ruhangisa, Winfrida Korosso na Lugano Mwandambo, Mahakama ilibatilisha Kifungu cha 50 cha sheria hiyo, lakini ikaridhia vingine kuwa ni halali.

Chanzo: Mwananchi
 

lukindo

JF-Expert Member
Mar 20, 2010
8,481
2,000
A thousand miles journey begins with a step! Walau umepatikana mwanzo, bidii zaidi inatakiwa ili kushinda game lote!
 

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
7,589
2,000
Petro hizi mahakama za ajabu kidogo, mbona vifungu vingine vinaonekana kuwa problematic even for a first year law student wameviacha? Nawakumbuka akina Mwalusanya, Lugakingira, Katiti! waliondoka na uhuru wa mahakama na sheria.
Ni "uhuru na haki" pia mtu kuwajibika kwa maneno na vitendo vyake, iwepo au isiwepo sheria. Huo ndio ubinadamu unaotutofautisha na wanyama.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom