Mahakama yafuta hati ya kumkamata Mbowe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahakama yafuta hati ya kumkamata Mbowe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sir.JAPHET, Sep 21, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  [h=2] Mahakama yafuta hati ya kumkamata Mbowe [/h] Ijumaa, Septemba 21, 2012 06:16 Na Omary Mlekwa, Hai

  MAHAKAMA ya Wilaya ya Hai imefuta hati ya kukamatwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, iliyotolewa baada ya kushindwa kufika mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

  Mahakama hiyo ilimfutia Mbowe na mdhamini wake, Awadh Mussa, baada ya kupokea maelezo na vielezo.

  Akitoa vielezo na maelezo mahakamani hapo jana yaliyosababisha kushindwa kuhudhuria mahakamani hapo, mdhamini huyo alimueleza Hakimu Mfawidhi wa Wilaya hiyo, Dennis Mpelembwa, kwamba siku ya kesi alikuwa mgonjwa na alilazwa hospitali na kushindwa kufika.

  Alisema mtuhumiwa alishindwa kufika mahakamani hapo kutokana kuwa nje ya nchi kwa ajili ya shughuli za kiserikali akiwa kama kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni.

  Kutokana na sababu hizo, Hakimu Mpelembwa hakuwa na pingamizi na kufuta hati ya kumkamata na kutoa amri ya mtuhumiwa huyo kufika mahakamani tarehe itakayopangwa kwa ajili ya kuendelea na hatua ya usikilizaji.

  Awali ilidaiwa kuwa Mbowe anakabiliwa na mashitaka ya kufanya vurugu na kumjeruhi Msimamizi wa Uchaguzi, Nasri Othmani, siku ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 katika Kituo cha Lambo.

  Inadaiwa mshitakiwa huyo alimshambulia msimamizi huyo na kumsababishia maumivu makali mwilini.

  Mbowe ameshitakiwa kutokana na kuvunja kifungu cha sheria ya makosa ya jinai kifungu cha 240 sura ya 16 ya sheria za Tanzania, kutokana na kufanya shambulio hilo katika kijiji hicho saa 11 jioni.

  Pamoja na kufuta hati ya kumkamata Mbowe, kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa tena Oktoba 9, mwaka huu.

  [h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]
   
 2. f

  fergusonema Senior Member

  #2
  Sep 21, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sina maoni
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Hii kesi niliisahau ati........
   
 4. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Asente kwa taarifa, ila wangekuwa watoa hati hizo kwa viongozi wote, bila kujali vyama, nadhani hakimu alikuwa anajipendkeza kwa serikari ya CCM, maana anajua hata kama hana sifa iko siku atakuwa jaji, si wajua tena Tanzania
   
 5. Ston Merchant

  Ston Merchant JF-Expert Member

  #5
  Sep 21, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 395
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  shukran kwa taarifa.........
   
 6. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #6
  Sep 21, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Asante!
   
 7. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #7
  Sep 21, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kesi zote kwa viongozi wa vyama vya upinzani ni za kusingiziwa ili kudhoofisha vyama hivyo ikiwa ni janjaa ya CCM. Nawaambia majaji na CCM kwa ujumla kuwa , Kama vile Giza lisivyoweza kushinda nuru vivyo hivyo Dhuruma haitashinda haki Daima.

  Mapaambano yanaendelea. niamdikie quality.chality0@gmail.com
   
 8. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Udhaifu tupu uliochanganyika na rushwa.
   
 9. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #9
  Sep 21, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,645
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  wastage of time and resources
   
 10. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #10
  Sep 21, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hivi hizi kesi hawawezi kuzifanya online ..
   
 11. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #11
  Sep 21, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  labda kupokea ushahidi.
   
 12. TEMPOLALE

  TEMPOLALE JF-Expert Member

  #12
  Sep 21, 2012
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 303
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Na watawafanyia sana unafikiri maneno aliyotoa Tundu lisu dhidi ya uteuzi wanayapenda? sijui anataka wakose ujaji kisa tuu eti hawana sifa.
   
 13. Mkali Tozz

  Mkali Tozz JF-Expert Member

  #13
  Sep 21, 2012
  Joined: Aug 9, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  .. kuwalundikia wapinzani kesi nyingi, imeshakuwa ni utamaduni wa serikali nyingi za vyama tawala hasa bara la giza!
   
 14. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #14
  Sep 21, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  kuzifanya online vp jomba?
  Laba unamaanisha kuwa hukumu ZIPAtikane online.
   
Loading...