Mahakama yadhibitisha Thamani ya MTANZANIA NI tsh.25 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahakama yadhibitisha Thamani ya MTANZANIA NI tsh.25

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Alfu Lela Ulela, Jan 11, 2011.

 1. A

  Alfu Lela Ulela JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jamani liko wapi soko la hisa za watanzania? Nataka nikaulize kama thamani ya mTZ imeongezeka au iko palepale.

  Mzee wa vijisent aliua akina dada wawili (mmoja mwenye umri wa miaka 38) na mahakama ikampiga faini ya tsh.700,000.

  Hii ina maana kila mmoja (kati ya wale waliouawa) thamani yake ni tsh.350,000.

  Sasa ukitaka kujua thamani ya Mtanzania mwenye umri wa mwaka mmoja chukua 350,000 then gawanya kwa miaka 38 aliyoishi yule dada mmoja utapata 9210.

  Kwa hiyo thamani ya mTANZANIA mwenye mwaka mmoja ni tsh.9210.

  Ukitaka kujua thamani halisi ya Mtanzania mwenye umri wa siku moja chukua 9210 then gawanya kwa siku 365 ambazo ni mwaka mmoja utapata 25.243.

  Kwa hiyo kumbe thamani ya Mtanzania ni tsh.25!! Mahakama imedhibitisha.
   
 2. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Toa utahira wako hapa.
  kesi ilivyohukumiwa si hicho unachoeleza, tunajua kuwa hukumu ya chenge ina maswali mengi lakini kosa la kuua hukumu yake si hicho unachoeleza. kwa nini usiulize kama hujui? humu kuna wanasheria wengi.
   
 3. d

  dotto JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kwani ni chenge ndiye aliyeua!!?? Tafadhali!!
   
Loading...