• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Mahakama yaamuru madiwani watano kulipa Chadema Sh15 milioni

nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,869
Points
1,225
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,869 1,225
Siasa
Chadema wakiwa katika maandamano.
Na Mussa Juma

Posted Alhamisi,Novemba22 2012 saa 10:39 AM

Kwa ufupi
Madiwani hao ni Estomih Mallah (aliyekuwa Naibu Meya ya Manispaa ya Arusha kipindi hicho), John Bayo aliyekuwa Diwani wa Elerai, Reuben Ngowi (Themi), Charles Mpanda (Kaloleni) na Rehema Mohamed aliyekuwa Diwani wa Viti Maalumu.


SHARE THIS STORY

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, imewaamuru madiwani watano waliotimuliwa Chadema kulipa gharama za kesi waliyokuwa wamefungua kupinga kufukuzwa uanachama, vinginevyo watapelekwa magereza.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Charles Magesa alitoa hukumu hiyo jana baada ya Chadema kushinda kesi hiyo.
Hakimu Magesa alisema madiwani hao wanapaswa kulipa Sh15 milioni ndani ya miezi miwili, wakishindwa watapelekwa gerezani.
Madiwani hao ni Estomih Mallah (aliyekuwa Naibu Meya ya Manispaa ya Arusha kipindi hicho), John Bayo aliyekuwa Diwani wa Elerai, Reuben Ngowi (Themi), Charles Mpanda (Kaloleni) na Rehema Mohamed aliyekuwa Diwani wa Viti Maalumu.
Pia, katika kesi hiyo ya madai Chadema walikuwa wakiwakilishwa na Wakili Method Kimomogoro, wakati wadaiwa hao walikuwa wakijitetea wenyewe baada ya aliyekuwa wakili wao kujitoa.
Akisoma uamuzi huo, Hakimu Magesa alisema baada ya mahakama kupitia hoja za pande zote, imeona wadaiwa hao wanapaswa kulipa zaidi ya Sh15.1 milioni, kila mmoja anatakiwa kulipa zaidi ya Sh3.2 milioni katika kipindi kisichozidi miezi miwili.
Awali, kulikuwa na mvutano kati ya wadaiwa hao jambo lililosababisha kesi hiyo kusikilizwa kwa kipindi kirefu ambapo walitakiwa kueleza mahakama hiyo sababu ya kutokupelekwa gerezani, huku kila mmoja akitamka kiwango cha fedha ambacho angeweza kulipa kwa mwezi.
Kwa upande wake, Ngowi alisema ana uwezo wa kulipa Sh25,000 kwa mwezi, Mpanda Sh20,000, Mallah Sh20,000, Rehema Sh15,000 na Bayo Sh15,000 kwa mwezi bila kuonyesha mchanganuo wa kipato chao, jambo lililopingwa vikali na Wakili Kimomogoro kwamba kiwango hicho ni kidogo.
Hakimu Magesa alisema kisheria mtu akishinda kesi ana uwezo wa kuchagua hukumu ya kulipwa kwa kuchukua mali za mdaiwa au mlalamikiwa kupelekwa kifungoni.
“Kimsingi mtu anaposhinda kesi lazima alipwe gharama aliyotumia na iwapo mahakama itaridhia alipwe kwa kiwango hicho, itachukua muda mrefu kati ya miaka 10 na 16 kumaliza deni hilo, jambo litakalosababisha aliyeshinda kushindwa kuona matunda ya ushindi wake,” alisema Magesa.
Alisema fedha hizo wanapaswa kuzilipa mara mbili, awamu ya kwanza inatakiwa kila mmoja kulipa zaidi ya Sh1.5 milioni na wawe wamemaliza kwa miezi miwili na kwamba, iwapo watashindwa mdai anaweza kupeleka mchanganuo wa gharama za kumtunza mfungwa na mahakama kuupitia na baadaye kutoa amri wapelekwe gerezani. 
idawa

idawa

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Messages
23,167
Points
2,000
idawa

idawa

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2012
23,167 2,000
duh.! Ama kweli sheria ni msumeno, Pinda yuko wapi awasaidie kulipa hizo gharama maana ndie aliewashawishi kwenda mahakamani.!
 
Mungi

Mungi

JF Gold Member
Joined
Sep 23, 2010
Messages
16,981
Points
1,500
Mungi

Mungi

JF Gold Member
Joined Sep 23, 2010
16,981 1,500
Waende kwa Pinda wampigie magoti wakalipiwe.
 
Lekakui

Lekakui

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
1,448
Points
1,225
Lekakui

Lekakui

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2012
1,448 1,225
Chadema ni chama makini na nadhani kwa hili watawasemehe hao madiwani ili iwe fundisho kwa wengine watakaoleta mambo ya utani in future
 
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,810
Points
2,000
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,810 2,000
ama kwa hakika hii ndiyo people's power ya kludharau wapigakura wa Arusha na ........
 

Forum statistics

Threads 1,402,803
Members 530,989
Posts 34,405,361
Top