Mahakama yaamuru Diwani aliyefukuzwa CHADEMA na kujiunga na Chama cha Wananchi (CUF) akamatwe!

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,000
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Arusha, imetoa hati ya kukamatwa mmoja wa madiwani waliofukuzwa na Chama cha Demokrasia na Mendeleo (CHADEMA), John Bayo baada ya kushindwa kutekeleza amri iliyotolewa na mahakama hiyo.
Hati hiyo iliyosainiwa na hakimu mkazi mfawidhi, Charles Magesa ilitolewa juzi baada ya Bayo kushindwa kutoa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 1.5 ikiwa ni sehemu ya kulipa gharama za shauri lao la madai lililotupwa, ambalo walilifungua kwenye mahakama hiyo dhidi ya CHADEMA na Mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe.
Hati hiyo ambayo Tanzania Daima inayo nakala yake, inamuagiza Mkuu wa Polisi wilayani Arusha kuhakikisha anamkamata na anamfikisha Bayo mbele ya mahakama hiyo mapema iwezekanavyo vinginevyo alipe kiasi hicho cha fedha kilichoamriwa na mahakama pamoja na gharama nyingine zitakazojitokeza katika zoezi la kumkamata.
Hata hivyo juhudi za kumpata Bayo ambaye tayari ameshajiunga na Chama cha Wananchi (CUF) kupitia simu yake ya kiganjani ziligonga mwamba kutokana na kuwa imezimwa muda wote.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CHADEMA wilayani hapa, Ephata Nanyaro, alisema kuwa ni kweli chama hicho kupitia wakili wao, Method Kimomogoro walilazimika kutoa taarifa mahakamani juu ya ukiukwaji huo wa amri ya mahakama baada ya kuona kipindi kilichotolewa na mahakama kwa ajili ya kutekeleza agizo hilo kikiwa kimekwisha huku Bayo akiwa hatekelezi amri hiyo wala kutoa taarifa yoyote.
Mapema Novemba 21, mwaka huu mahakama hiyo iliwaamuru waliokuwa madiwani watano wa CHADEMA kulipa gharama zilizotumika kuendesha shauri lao lililotupwa na mahakama ya mkoa kiasi cha shilingi milioni 15.1 kwa awamu mbili vinginevyo watapelekwa gerezani.
Aidha, kila mdaiwa anapaswa kulipa kiasi cha shilingi milioni 3.2 ambapo awamu ya kwanza ya shilingi milioni 1.51 walitakiwa kutoa mara baada ya uamuzi huo kutolewa na kiasi kilichobaki wanatakiwa wawe wamelipa ndani ya kipindi cha miezi miwili toka jana.
Wajibu maombi wengine katika shauri hilo la kudai gharama waliotimiza sharti hilo ni Reuben Ngowi, Charles Mpanda, Rehema Mohamed na Estomii Mallah.
Awali, Agosti 10 mwaka jana mahakama ya hakimu mkazi mkoa iliyokaa chini ya hakimu Hawa Mguruta, ilitupilia mbali shauri la madai lililofunguliwa na madiwani hao dhidi ya Mbowe na CHADEMA baada ya kubaini kuwa kulikuwa na upungufu wa kisheria.
Madiwani watano walikuwa wakipinga kuvuliwa uanachama wa CHADEMA, baada ya kufikia muafaka wa uchaguzi wa umeya wa Jiji la Arusha bila kupata baraka za chama.
 

Ronal Reagan

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,890
2,000
Nadhani hao waliokuwa madiwani wa CHADEMA Arusha wanajutia usaliti wao sasa. Lakini si walishikishwa mshiko na magamba? Watumie hizo hizo kujikwamua vingenevyo wapelekwe magereza
 

ZionGate

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
5,896
2,000
Alihamia cuf akizan watamchangia den hahahahaaaaaaaa,nenda magogon kwa mfazil wenu akupige tag
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
17,736
2,000
Hivi unaweza kufukuzwa Chadema ukajiunga na CUF kweli? Akili matope? Ukifukuzwa Chadema the best you can do ni kutulia ukaishi kama raia mwema vinginevyo unajitia aibu mbele ya jamii.

Inanikumbusha yule Charles Mwera mrithi wa Chacha Wangwe kule Tarime sijui naye aliishia wapi baada ya "kuikomoa" Chadema kwa kujiunga CUF.

 

Ukwaju

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
13,302
2,000
Habari hii niliileta hapa tangu juzi..
Ni kweli Crashwise ulichosema kimetimia tulikuwa hatuamini mpaka tumekuwa Tomaso, sasa waende tu hakuna ujanja km Diwani mstaafu anakosa 1.5m hata za kuchangiwa basi ...
 
Last edited by a moderator:

Safety last

JF-Expert Member
Mar 24, 2011
4,230
2,000
Hivi
unaweza kufukuzwa Chadema ukajiunga na CUF kweli? Akili matope?
Ukifukuzwa Chadema the best you can do ni kutulia ukaishi kama raia
mwema vinginevyo unajitia aibu mbele ya jamii.

Inanikumbusha yule Charles Mwera mrithi wa Chacha Wangwe kule Tarime
sijui naye aliishia wapi baada ya "kuikomoa" Chadema kwa kujiunga CUF.


yule jamaa wa mara hovyo sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom