Mahakama yaamuru Cyprian Musiba kulipa faini ya Tsh. bilioni 6 kwa kumchafua Bernard Membe

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemuamuru mwanahabari anayejitambulisha kama mwanaharakati huru, Cyprian Musiba kumlipa fidia ya Sh6 bilioni aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika Serikali ya Awamu ya Nne, Bernard Membe.
Hapo hata akiuza mali zake zote, auze familia na ukoo wake wote ajiuze na yeye mwenyewe hatoboi
 
Ndio faida ya kutumikia watu wajinga,amekubali kutumika kama tambara la deki kwa kudanganywa na vijisenti vichache masikini.
 
Kwa hiyo huyu mwamba kwa sasa ana madeni yapatayo 13bilion! Manake kule kuna shangazi Fatuma alipata tuzo ya 7b na huku Membe 6b. Nadhani sasa Musiba ni raia anayedaiwa madeni makubwa kuliko raia yeyote hapa nchini na anastahili sifa ya Highly Indebted Poor Person (HIPC).
Kwa lugha ya mtaani hakopesheki hata vikoba.
 
Hapo hata akiuza mali zake zote, auze familia na ukoo wake wote ajiuze na yeye mwenyewe hatoboi
IMG-20211028-WA0012.jpg
 
1. Atapewa muda wa kulipa cash.

2. Kama pesa hana, mali zake za kampuni (gazeti la Tanzanite) zitakuwa attached kisheria na kuuzwa kwa mnada halali publicly kwa order ya Mahakama, ili kulipa pesa yote husika.

3. Kama hana mali yoyote ya kukamata, ama mali zake husika hazitoshi kulipa dai lote, basi hapo mdai anakuwa na utashi (discretion) wa aina mbili: Kupokea pesa iliyopatikana (pungufu) na kumaliza kesi, ama kuridhia mdaiwa apelekwe jela kwa gharama za mdai mwenyewe. Civil prisoner. Yaani mfano mdaiwa akafungwa jela (civil prisoner) kwa miaka mitatu. Yule mdai atalipia gharama zote za mfungwa kwa miaka hiyo mitatu. Yaani mdai utalipia ili mdaiwa wako apelekwe gerezani kwasababu hana mali yoyote ya kulipa. Afisa magereza anaitaarifu Mahakama kuwa mfungwa mmoja anatumia gharama shilingi ngapi kwa siku kuwa gherezani. Kisha wanapiga calculation, mdai unalipia na risiti ya serikali unapewa, kisha mdaiwa wako anapelekwa 'ngome'.

-Kaveli-
Ahsante kwa maelezo mazuri. Kwahiyo mdai akimpeleka mdaiwa magereza mdai ndio anapata hasara tena kwa maana hiyo. Sheria ni ngumu sana
 
Mahakama kuu ya Tanzania imetoa hukumu ya kesi ya kuchafuliwa jina iliyokuwa ikimkabili mkurugenzi mkuu wa gazeti la Tanzanite na mwanaharakati huru, ndugu Musiba dhidi ya aliyekuwa Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na mgombea Urais kupitia ACT-Wazalendo, ndugu Bernard Membe. Mahakama hiyo imemtaka Musiba kulipa kiasi hicho cha pesa.

==========

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemuamuru mwanahabari anayejitambulisha kama mwanaharakati huru, Cyprian Musiba kumlipa fidia ya Sh6 bilioni aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika Serikali ya Awamu ya Nne, Bernard Membe.

Hukumu hiyo imetolewa leo Alhamisi Oktoba 28,2021 na Jaji Joacquine De Mello aliyeisikiliza kesi hiyo.

Katika hukumu hiyo Musiba ametakiwa kumlipa Membe kiasi hicho cha fedha pamoja na gharama zote za uendeshaji wa kesi kwa zaidi ya miaka miwili.

Pia imeweka zuio la kudumu kwa Musiba la kutokumkashifu Membe au kusema uongo dhidi yake.

Mwananchi

Pia, soma=> Benard Membe: Musiba hasimami tena na kujifanya yeye ni Mungu Mtu. Huko uliko naomba hela zangu

Si anyongwe tu mambo yaishe.
 
Hu

Huyu mwanaharakati mpumbavu alitakiwa atutetee sisiwavuvi tulioharibiwa malizetu halali kwa kuonewa kabisa aliendaelea kumsifu tu sasa alipe bila deni sema nchi yeti haina sheria ndoa za jinsia moja angeolewa deni likaisha
 
Back
Top Bottom