Mahakama yaamua kuwa ukahaba si uhalifu Nigeria

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
1576830714698.png

Mahakama kuu jijini Abuja imetangaza kwamba ukahaba sio uhalifu nchini Nigeria.

Uamuzi huo umejiri katika kesi iliyokuwa inashirikisha wanawake 16 waliokamatwa kwa kufanya ukahaba.

Ni mara ya kwanza kwa mahakama ya Nigeria kuamuru kuhusu uhalali wa biashara hiyo ambayo inazidi kuonekana kuwa uhalifu mkubwa miongoni mwa mataifa mengi Afrika.

Jaji Binta Nyako wa mahakama kuu ya Abuja alisema kwamba hakuna sheria inayoharamisha ukahaba nchini humo.

Kesi hiyo iliowasilishwa 2017 ilifuatia kukamatwa kwa baadhi ya wanawake mjini Abuja kwa madai ya kushiriki katika biashara hiyo.

Licha ya serikali ya taifa hilo kudai kwamba wanawake hao ni wahalifu mahakama ilipinga hilo na badala yake kuagizia kwamba walipwe fidia.

Wakili mmoja aliyekuwa akiwawakilisha wanawake hao Babatunde Jacob aliambia BBC kwamba mahakama iliamuru kwamba vyombo vya usalama vilikiuka haki za wateja wake wakati walipovunja na kuingia katika nyumba zao na kudai kwamba wanawake hao walikuwa makahaba.

Wataalam wa sheria wanaamini kwamba uamuzi huo utakuwa na athari kubwa kwa taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika.

Kukamatwa kwa makahaba na vyombo vya serikali ni kitu cha kawaida. Katika msako mmoja mnamo mwezi Mei mwaka huu, zaidi ya wanawake 60 walikamatwa mjini Abuja kwa kudaiwa kushiriki katika bishara hiyo.

Wanawake hao walidai kwamba , walinyanyaswa, kupokonywa fedha zao kwa nguvu na kuaibishwa hadharani.

BBC Swahili
 
NIGERIA: Mahakama Kuu imeamuru kuwa ukahaba si kosa kwa kuwa hakuna sheria yoyote nchini humo inayozuia kitendo hicho. Uamuzi huo umetolewa Desemba 19 na Jaji Binta Nyako wa Mahakama Kuu jijini Abuja na kuamini wanawake 16 waliokamatwa mwaka 2017 kwa kufanya ukahaba walipwe fidia .
IMG_20191220_123032.jpeg
 
Kuna majimbo yanaendeshwa kwa Sheria za Kiislam na sio Nigeria yote mkuu, mbona majibu yenu ovyo sana kiivyo
Acha uongo mtoa mada, la sivyo ambatanisha na source, Ile nchi ina Waislam wengi zaidi ya milioni 100, tena wenye misimamo mikali, baadhi ya maeneo hawaruhusu kula mchana kipindi cha Ramadhani, wangelipua mahakama kuu kwa huu uamuzi
Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
, Ile nchi ina Waislam wengi zaidi ya milioni 100, tena wenye misimamo mikali, baadhi ya maeneo hawaruhusu kula mchana kipindi cha Ramadhani, hawatalipua mahakama kuu kwa huu uamuzi?
Sent using Jamii Forums mobile app
Wakishalipua kuna watu humu, akiwemo mama moja, watadai hao waliolipua sio waislamu na kuwa muislamu hawezi kufanya vitendo kama hivyo na wakati huo huo walipuaji watadai wamefanya kwa jina la allah........ What a paradox.
 
Mahakama za Tanzania ziige mfano huu mzuri, kwanza tumeambiwa tufyatue watoto wengi elimu ni bure
MAHAKAMA ZETU SIO ZA KUIGA TUU!! VP WEWE!!!???
KWA HIYO WEWE ULITAKA HATA SIKU NIGERIA IKISEMA WANAUME 'WACHAPANE' MAHAKAMA ZETU PIA ZIIGE???!!

HUO NI UKIMWI WA UBONGO WAKO WENYE CANCER YA MAWAZO.

AKILI ZISIZO NA AKILI NI CHANGAMOTO KWENYE JAMII.

HAYO MAMBO YA KUHALALISHA UKAHABA YATAISHIA HUKO HUKO NIGERIA KWETU HAPA NO!. NO. NO HII NI NCHI YA WATU WASTAARABU MZEE. WACHA KUIGAIGA TU KILA UJINGA UTAIGA MENGI YASIOFAA.
 
Back
Top Bottom