Mahakama yaamru serikali kumlipa mfanyabiashara Sh15bilioni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahakama yaamru serikali kumlipa mfanyabiashara Sh15bilioni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Oct 16, 2007.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 16, 2007
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 55,662
  Likes Received: 20,260
  Trophy Points: 280
  Posted Date::10/16/2007
  Mahakama yaamru serikali kumlipa mfanyabiashara Sh15bilioni
  Na Frederick Katulanda, Mwanza
  Mwananchi

  MAHAKAMA imeiamuru Serikali kuilipa kampuni ya Mansoor Oil Industries Ltd (MOIL) ya jijini Mwanza jumla ya Sh14.7bilioni

  kutokana na uamuzi uliotolewa na Waziri wa Ujenzi wakati huo John Pombe Magufuli wa kuvunja kituo cha mafuta cha kampuni hiyo.

  Uamuzi huo umetolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza katika kesi ya madai namba 2 ya mwaka 2002 ambapo

  kampuni hiyo ilikuwa ikiwashitaki Waziri Magufuli, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (wakati

  huo) Brigedia Hassani Ngwilizi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Andrew Chenge pamoja na Halmashauri ya Jiji la Mwanza.

  Katika kesi hiyo madai ya kampuni hiyo ya MOIL kwa serikali yalikuwa jumla ya Sh.18bilioni kutokana na kuvunjiwa kituo hicho cha mafuta kilichokuwa kimejengwa katika kiwanja namba 178 Kitalu ‘A’ eneo la Kirumba kando ya barabara ya Makongoro.

  Katika madai hayo, kampuni hiyo iliomba kulipwa kiasi cha Sh 593milioni kama thamani ya jengo ambalo lilibomolewa kwa amri ya Waziri Magufuli, Sh13.4 bilioni ikiwa ni kiasi cha faida ambacho ingekipata katika kipindi cha miaka 33 ambacho ilitarajiwa kufanya biashara na Sh 4 bilioni kama hasara ya jumla ya mradi huo.

  Katika hukumu hiyo iliyotolewa Agosti 30, mwaka huu na Hakimu Mfawidhi H. Mushi kwa niaba ya Jaji Lawrence Mchome, mahakama ilisema baada ya kusikiliza pande zote ikiwa ni pamoja na kupitia vielelezo na ushahidi mbalimbali iliridhika na hivyo kutoa uamuzi kuwa mlalamikaji anapaswa kulipwa fidia katika madai yake.

  Katika hukumu hiyo, Mahakama imesema kwamba mdai alikuwa na vibali halali vinavyoruhusu kuendesha shughuli zake katika eneo hilo, na kwa mujibu wa sheria, Rais ndiye alikuwa na uwezo wa kubatilisha vibali hivyo na si waziri.

  “Mahakama iliamuru Serikali Kuu kwa niaba ya washitakiwa watatu ambao ni Waziri Magufuli, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (wakati huo) Brigedia Hassani Ngwilizi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Andrew Chenge kulipa fidia kama ifuatavyo.

  Kuilipa kampuni hiyo kiasi cha fidia ya Sh 490 milioni badala ya Sh 593 milioni alizoomba, kumlipa Sh13.4 bilioni kama fidia ya faida ambayo angepata katika kipindi cha miaka 33 na kumlipa kiasi cha Sh 730 milioni ambacho ni sehemu ya Sh 4 bilioni, aliyoomba kama hasara ya jumla katika mradi huo wa kituo cha mafuta.

  Katika hukumu hiyo, mahakama imemwondoa mlalamikiwa mmoja ambaye ni Halamshauri ya Jiji la Mwanza kwa kuwa

  hakuhusika na uvunjaji wa kituo hicho.

  Pia mahakama imeamuru serikali kumlipa mdai huyo kiasi cha asiliamia 17 ya madai yake ya hasara ya

  jumla ya Sh730 milioni kwa mwaka tangu siku jengo hilo lilipobomolewa Juni 21, 2001 hadi siku ya hukumu ilipotolewa.

  Makahama imeamuru kulipwa kwa mdai huyo tena kiasi cha asiliamia hizo 17 ya Sh13.4 bilioni kwa mwaka ambayo ni madai yake ya hasara kutoka siku jengo lilipobomolewa hadi siku ya hukumu.

  Kituo hicho kilibomolewa wakati tayari kikiwa kimekaguliwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza na kutoa hati ya umiliki wa kiwanja hicho Na. 033005/167 ya muda wa miaka 33 pamoja na hati ya kuruhusu ujenzi wa kituo hicho na Na. 00785.

  Katika kesi hiyo MOIL ilikuwa ikitetewa na mawakili Salum Magongo na Paulin Rugaimukamu wote wa

  jijini Mwanza wakati serikali ilikuwa ikitetewa na mawakili Michael Kamba na Edwin Kakolaki.
   
 2. green29

  green29 JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2007
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 312
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Duh... kwani tokea amekuwa waziri Magufuli ameshazalisha shs ngapi maana hii hasara wanayoliingizia taifa kwa umbumbumbu wa sheria ni kubwa sana??? ukiachana na biashara ya kuuza nyumba za serikali!
   
 3. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2007
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 9,116
  Likes Received: 1,165
  Trophy Points: 280
  Ina maana hizi gharama zitalipwa kutokana na kodi zetu ama? Kwa sababu kosa kafaya Magufuli na wenzake. Kwa nini wasiwajibike wao wakosaji moja kwa moja?
  Naomba ufafanuzi
   
 4. S

  Semanao JF-Expert Member

  #4
  Oct 16, 2007
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 208
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Hiyo pesa ya walipa kodi sababu MAgufuli alikuwa ndo mwakilishi. Nafikiri kuna umuhimu wa mawaziri kupimwa IQ zao vinginevyo watakuja kufilisi taifa kwa maamuzi ya pupa. Tukianzia kwa LOwassa alifuta mkataba wa city water na sasa serikali iko kitanzini
   
 5. S

  Semanao JF-Expert Member

  #5
  Oct 16, 2007
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 208
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Hiyo pesa ya walipa kodi sababu MAgufuli alikuwa ndo mwakilishi. Nafikiri kuna umuhimu wa mawaziri kupimwa IQ zao vinginevyo watakuja kufilisi taifa kwa maamuzi ya pupa. Tukianzia kwa LOwassa alifuta mkataba wa city water na sasa serikali iko kitanzini
   
 6. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #6
  Oct 16, 2007
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Bwana Mkubwa Magufuli...hatua ile ilikuwa ya kipumbavu kabisa.MOIL walikuwa na kila documents za kuhalalisha kujenga pale lakini wewe ukiwa umelewa madaraka ulidhani una mamlaka ya kuvunja kile moil alikuwa akikijenga kwa jasho lake.sijui ulikuwa unamchukia kwa rangi yake au mafanikio yake ...nobody knows.Wewe ni mtu hatari sana kwa jamii.Kweli inafaa upimwe iq.Nadhani hata JK hatakuvumilia na atakupiga teke sasa hivi.
   
Loading...