Mahakama ya Uingereza yahukumu Assange anaweza kurejeshwa nchini Marekani

Marekan hatetei haki za binadam dunian, hana ujinga huo! Kukiwa na chochote cha kufaidi katika nchi 'y', basi nchi hiyo itasingiziwa kwamba inakiuka haki za binadam
 
View attachment 2044736Hivi karibuni Marekani imeongoza “mkutano wa kimataifa wa demokrasia”, na kwenye mkutano huo nchi za Magharibi zimedai kutetea mambo ya demokrasia na haki za binadamu duniani. Kinachoshangaza ni kwamba wakati wa mkutano huo, Mahakama Kuu ya Uingereza imetoa uamuzi kwamba mwanzilishi wa kampuni ya WikiLeaks Bw. Julian Paul Assange, anaweza kupelekwa nchini Marekani, na kama akipelekwa anaweza kukabiliwa na adhabu ya kifungo cha miaka 175. Jambo hili linadhihirisha kwamba, nchi za magharibi zinafanya unafiki mkubwa katika mambo ya demokrasia na haki za binadamu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken hivi karibuni kwenye mtandao mmoja wa kijamii, alisema zaidi ya wanahabari 350 duniani wamefungwa kutokana na ripoti zao. “Lazima tufichue kwa uthabiti ukandamizaji kwa waandishi wa habari, na lazima tuhimize kuachiliwa kwa wanahabari wanaozuiliwa bila haki,” alisema. Lakini Bw. Blinken amemsahau Bw. Assange, ambaye ni mwanahabari mashuhuri zaidi wa kiraia atakayekabiliwa na kifungo cha maisha nchini Marekani. Kwani Assange amefanya uhalifu gani mbaya?

“Uhalifu” Assange ni kwamba alitumia uhuru na haki za binadamu ambavyo nchi za Magharibi zinatetea kwa nguvu zote, na kufichua uhalifu mwovu uliofanywa na Marekani, ikiwa ni pamoja na mauaji ya zaidi ya raia 15,000 nchini Iraq ambao hawakuripotiwa, kutesa wafungwa wenye miaka kati ya 14 na 89 huko Guantanamo, kufanya ujasusi dhidi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na wanadiplomasia wengine kwa njia haramu, kuanzisha mapinduzi ya kijeshi nchini Honduras, kufanya vita ya kisiri dhidi ya Yemen, na kusababisha vifo vya maelfu ya watu.

Baada ya kutangazwa kwa hukumu hiyo Bw. Edward Joseph Snowden ambaye ana uzoefu unaofanana na Assange, amesema Assange ni mmoja wa wafungwa wakubwa wa kisiasa katika nchi za Magharibi. Kila kesi dhidi yake imejaa rushwa na matumizi mabaya ya sheria. Bw. Snowden amekuwa akisakwa na serikali ya Marekani kwa kufichua mpango wa ujasusi wa “Prismgate”, na sasa amejificha nchini Russia.

Mbunge wa zamani wa Uingereza George Galloway amesema, kama Bw. Assange angekuwa mwanahabari wa China aliyefichua siri ya serikali, angepata Tuzo ya Nobel, na kuwa mtu anayefuatiliwa zaidi na nchi za magharibi katika “Siku ya Haki za binadamu”, picha yake kubwa ingeoneshwa kwenye mkutano wa demokrasia ulioitishwa na Rais Joe Biden wa Marekani, na pia angekuwa msemaji wa kususia Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing.

Kwenye mkutano wa demokrasia, Uingereza na Marekani zimedai jinsi zinavyojitahidi kutetea demokrasia na haki za binadamu duniani, na kusema nchi zao zimetekeleza demokrasia vizuri kuliko nchi nyingine. Hata hivyo, hukumu ya Mahakama Kuu ya London dhidi ya Bw. Assange imefichua unafiki wao. Kama Jarida la Time la Marekani lilivyosema, mkutano huu haukuwa na nia ya kutatua changamoto za kidemokrasia nchini Marekani, badala yake umelenga kuzipaka matope China na Russia, hivyo mkutano huu umekuwa “kilele cha unafiki”.
Walisikika wanaharakati tz "Marekani inajali uhuru wa kujieleza..........".
 
Hawa waingereza wanaagiza familia kutoa kubali cha kuua watoto wenye ulemavu na bado wanajinasibu wapigania haki za binadamu. Inashangaza kwa wale wanaowapelekea mashitaka ya haki za binadamu.

Jioneeni kadhaa yao

 
Back
Top Bottom