Mahakama ya Uhujumu Uchumi: Mvutano mkali kesi ya Mbowe na wenzake. Hatma ya kesi kujulikana Septemba 6

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,323
217,344
Kesi ya Ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake watatu inaendelea kuunguruma kwenye Mahakama ya Uhujumu uchumi , Ambapo mvutano wa kisheria umekuwa mkali hasa baada ya Mapingamizi yaliyowekwa na Mawakili wa Mbowe kuwa ya moto .

Kesi imeahirishwa kwa muda ili kuiruhusu Mahakama kupitia mapingamizi hayo na ufafanuzi wa mawakili wa serikali

Leo_Sept._03,_2021_Mhe. @freemanmbowetz amefikishwa_Mahakama_Kuu_Division_ya_Uhujumu_Uchumi_na...jpg


------ Maelezo kwa hisani ya Martin M. M-----

Updates; Kesi imeanza saa 9:30 asubuhi kwa Jaji Luvanda kuingia chumba cha mahakama. Mawakili wa Freeman Mbowe wametambulishwa wakiongozwa na Peter Kibatala. Jumla ya Mawakili 9 waliopo na Wengine watakaoendelea kuingia wameombewa udhuru wa kuchelewa kuingia chumba cha mahakama.

Updates; Mawakili wa upande wa Jamhuri wamejitambulisha na wanaomba waendelee na kesi kwa kujibu hoja za upande wa utetezi (washtakiwa). Mawakili wa Jamhuri wanaomba kujibu hoja ya 2 na 3 na kisha ya 1 itakuwa ya mwisho katika mlolongo huo ambao wameomba mbele ya mahakama.

Sehemu ya pili ya pingamizi la 3 la upande wa utetezi kuwa hati ya mashtaka ni batili kwa sababu ya kujirudiarudia (duplicity) kwa mashtaka. Yanatokana na watu walewale, muda uleule lakini wameshtakiwa katika makosa mawili tofauti ya 1 na 4.

Updates; Mawakili wa upande wa Jamhuri Wlwanasema pingamizi la 3 lililogawanyika sehemu kuu 3, kwamba hati ya Mashtaka ni batili kwa sababu imeunganisha mashtaka ya kula njama za kutenda ugaidi na mambo madogo madogo ya kula hizo njama. 1/2

Updates; Wakili upande wa Jamhuri anaomba kuanza na hoja ya tatu sehemu ya kwanza, Mapungufu katika hati ya mashtaka. Upande wa Jamhuri unapinga hoja hiyo kwa kueleza Mahakama kwamba shtaka la kula njama za kupanga ugaidi na mpaka shtaka la 6 hakuna hata moja linalo jirudia

Updates; Wakili upande wa Jamhuri anaomba mahakama irejee hati ya mashtaka, maelezo ya kosa hili Yanajieleza Kuwa washtakiwa walikula njama, kutenda matendo ya kigaidi, kulipua vituo vya mafuta na kulipua mikusanyiko katika Jiji la DSM, Mwanza na Arusha na kutishia Jamhuri

Updates; Wakili wa Jamhuri anaeleza mahakama, njama hizi zilikuwa zilitegemewa kuwepo. Shtaka la msingi lilitakiwa kuwa kulipua vituo vya mafuta. Hakuna mashtaka yanayosema kuwa washtakiwa walilipua vituo vya kuuzia mafuta sehemu zilizo tajwa na hakuna kosa tulilowashtaki nalo.

Updates; Jamhuri inaeleza mahakama, mashtaka kuanzia 3 hadi 6 hakuna kosa la kusababisha majeraha. Kwa sababu hiyo ndiyo maana wameita ni njama. Mashtaka kuanzia 3 hadi 6 ni mashtaka yaliyokamilika kwa mujibu wa sheria. Ni makosa kwa mujibu wa sheria ya kuzuia ugaidi.

Updates; Mawakili wa Jamhuri bado wapo kwenye hoja ya 3, sasa wanaelezea kesi za mifano zilizotolewa na wakili Jeremiah Mtobesya ile ya Steven Salvatory Vs Republic na ile ya Magogo Njige na mwenzake Vs Republic kuwa zilikuwa kesi zilizoamuliwa mahakama ya rufani (Jinai).

Updates; Mawakili wa Jamhuri wanaeleza kwamba ni kweli mahakama ya rufani (kwa kurejea kesi hizo hapo juu) ilikataa utaratibu wa kurudia mashtaka ya kula njama na kushtaki kosa kuu hapo hapo katika hati moja ya mashtaka. (zingatia, hii ni hoja ya msingi upande wa utetezi)

Updates; Mawakili wa Jamhuri wanasema ndiyo maana (Jamhuri) wameshtaki kula njama za Kutenda ugaidi na hawajawashtaki watuhumiwa hao kwa kosa la ugaidi kwa hiyo hawaoni kuwa makosa yamejirudia kwa muktadha huo. Pia wanasema mawakili wa utetezi hawajaonyesha sheria au precedent

Updates; Mawakili wa Jamhuri kuhusu hoja ya 3 ya sehemu ya 2 ya utetezi, wanasema kifungu cha 5(a) cha sheria ya ugaidi kuwa mtu anatenda ugaidi kwa kupanga, kusaidia au kushiriki kikao chenye viashiria vya kutenda ugaidi. Mawakili hao wanasisitiza kwamba sio lazima ukae kikao

Updates; Mawakili wa Jamhuri wanatafsiri kifungu cha 27(c) cha sheria ya kuzuia ugaidi kwa kutumia kamusi ya "Black Law Dictionary" ukurasa wa 329. Wanatafsiri kula njama kuwa ni kukubaliana kiakili. Jaji anauliza "hiyo tafsiri ni yako?". Wakili anarudia tena kusoma dictionary

Updates; Jaji anamuuliza "hiyo tafsiri ni yako?" wakili wa Jamhuri anarudia kusoma upya.. Baada ya ukimya wa dakika 3, wakili anasema "njama ni makubaliano ya kutenda kosa". Anasema shtaka la 4 linasema walishiriki kwenye kikao cha kupanga kulipua.

Updates; wakili wa Jamhuri anasema "kuna kukubaliana kiakili na kuna plan" na anasisitiza kutokana na hayo matendo mawili tofauti, na hivyo hayo makosa ni tofauti na hawahitajiki kuthibitisha kukutana kwa washtakiwa bali wanachotakiwa kuthibitisha ni "Common intentions".

Updates; Wakili wa upande wa Jamhuri anahitimisha hoja zake kwamba hakuna kujirudia kwa makosa katika hati ya mashtaka kwa kuwa hayo ni makosa mawili tofauti na mtu anaweza kuishia kutenda kosa moja asifike kwenye kosa la pili.

Updates; Mawakili wa Jamhuri wanauliza mahakama kwamba kesi ya marejeo iliyotolewa na wakili upande wa utetezi, Jeremiah Mtobesya haipo katika walichonukuu, kwamba wametafuta hawajaiona. Mawakili wa utetezi wanaulizwa wanasema "Jamhuri wamekosea kunukuu au hawajaiona kweli"

Updates; Mawakili wa Jamhuri wanajibu hoja hoja ya kwamba hati ya Mlmashtaka ni batili kwa sababu haielezi ni wapi? Lini? Muda? Malengo? Mawakili wa Jamhuri wanasema kasoro hiyo haipo. Wanasema sheria inasema kwamba unatakiwa kujikita katika masuala yaliyoelezwa katika sheria tu

Updates; Mawakili wa Jamhuri wanaeleza mahakama kwamba haikuwepo sababu ya Jamhuri kuweka maelezo mengi kuhusu makosa ya kula njama za Kutenda ugaidi katika hati ya mashtaka. Sasa anaeleza kwanini sheria ya ugaidi Tanzania ni tofauti na ile ya Zambia, Uganda na Trindad & Tobago

Updates; Mawakili wa Jamhuri wanasema licha ya nchi tatu hizo kuwepo katika Jumuiya ya madola sheria zao za ugaidi ni tofauti, ingawa wanakiri mbele ya mahakama kwamba sheria ya ugaidi Tanzania ilitungwa kwa hitaji la Jumuiya za kimataifa mwaka 2004 (kasema 2004, tunzeni hii)

Updates; wakili wa Jamhuri anasema mazingira yanaweza kufanya sheria za ugaidi kutofautiana na nchi nyingine., wanasema paliletwa statutory provision for legislative kama sheria ya mfano kwa nchi zote lakini waliruhusu nchi hizo kuweka mambo mengine.

Updates; Mawakili wa upande wa Jamhuri wameingia hoja ya kwanza ya pingamizi kwamba kifungu namba 4 cha sheria kama ilivyonukuliwa kwenye mashtaka hakikuwa kimetoa tafsiri ya sheria ya Ugaidi, kwa maana hiyo hakuna kesi. Wanajibu "Hapana, mashtaka yapo wazi, wametengeneza kosa"

Updates; Wakili wa Jamhuri anasema kifungu 4(i) kimesema mtu yeyote atakayefanya matendo ya ugaidi atakuwa ametenda makosa na kifungu 4(ii) kinaeleza matendo gani ya ugaidi na 4(iii). Anasema hata sheria za kimataifa hawajajaribu hata kidogo kutafisiri neno 'TERRORISM INTENTION'

Updates; Wakili wa Jamhuri anaeleza kwamba sheria yetu ya ugaidi 4(ii) paragraph A,B na C zimeonyesha mtu akitenda vitendo hivi atakuwa ametenda matendo ya ugaidi. Anasisitiza kwamba unatakiwa kujikita kwenye sheria hiyo ili kupata maana ya ugaidi na kusudio la kutenda ugaidi.

Updates; Wakili wa Jamhuri anasema chapter one inatuongoza kupata tafsiri ya maneno yote ya sheria hii. Anamueleza Jaji "kutokuwepo kwa definition ya neno hilo haimaanishi kushindwa kuona intention of Terrorism" na hakuzui mahakama kutafsiri. Tools zipo nyingi za kutafsiri.

Updates; Wakili wa Jamhuri anaeleza mahakama, tools zipo nyingi za kutafsiri 'ugaidi na dhamira' hata kama sheria haina tafsiri hiyo. Anataja case laws, vitabu vya sheria. Anasisitiza kukosekana kwa neno haimaanishi mahakama itashindwa kupewa tafsiri ya "terrorism intentions"

Updates; Wakili wa upande wa Jamhuri anasisitiza kwamba kwa Maelezo hayo wame create makosa kwa kutumia sheria hiyo. Anamuomba radhi Jaji kama neno wamesahau kwa kupitiwa basi dhamira yao ya kupambana na vitendo na ugaidi kimataifa izingatiwe. Anarejea sheria ya ugaidi Sept 2002

Sisi (Mawakili wa Jamhuri) tunasema hoja yao haina mashiko kwa sababu sheria hii imejieleza kwenye majedwali, hatukutakiwa kwenda zaidi ya hapo. Wakili huyu anasisitiza kwamba mashtaka yote ni valid na yamezingatia sheria husika wakati wa kuandika hati ya mashtaka hayo.

Updates; Wakili wa upande wa Jamhuri anaendelea kueleza katika mwongozo huu na hati hii ya mashataka hatukuhitajika kutafsiri kuhusu hili. Mawakili wa Freeman Mbowe walikuwa wanasema kwa kuwa Terrorist intentions haijawa defined na kwa sababu hiyo mashtaka yatupiliwe mbali.

Updates; Hoja ya mwisho ya mawakili ya Jamhuri, wanasema mawakili wa Freeman Mbowe walikuwa wanasema tutumie exactly 4(3)(i). Wakili huyu wa Jamhuri anasema hawapaswi kutumia maneno yanayopendekezwa na mawakili wa Freeman Mbowe. Wametumia neno intended kwa kuwa ndiyo purpose, walikubaliana kuwa yana maana na walikwenda kupata maana kwenye Dictionary na hivyo hata kesi hii hata kama neno 'terrorist intentions' halijafafanuliwa lakini haliwezi kufanya lisiwe na maana kabisa. Terrorist intentions ndiyo pekee linalotofautisha na makosa mengine ya Jinai

Updates; Mawakili wa Jamhuri wanataka kesi ya Paul Dionizi Criminal appeal 271 ya 2018 katika mahakama ya rufaa ukurasa wa 10 ambapo palikuwa na malalamiko katika kesi ya ubakaji kwa maneno yaliyotumika. Majaji walikubaliana kuwa pamoja maneno hayajasemwa katika sheria 1/2

Updates; Wakili wa upande wa Jamhuri anasema makosa katika sheria nyingine yanatokana na kusoma vizuri vifungu katika kutekeleza makosa katika sheria hii, na huu ndiyo utofauti.. Katika kifungi 4(iv) paragraph A na B ime' exclude vitendo vitavyokuwa siyo vya kigaidi

Updates; Wakili wa upande wa Jamhuri anasema wenzetu (mawakili upande wa utetezi) walidai kuwa wasichukuliwe kama wanai' challenge sheria sisi tunaona wana' challemge sheria hii. Pia hati ya mashtaka haina makosa wanayodai. Pia wameleta muda wa kesi katika muda ambao siyo sahihi

Updates; Wakili wa upande wa Jamhuri anasema Mheshimiwa Jaji kutokana na tulichokieleza katika sheria zetu kutokana na hoja za wenzetu, tunaona hoja zao za mapingamizi ya kisheria zionekane hazina mashiko. Tunaomba mapingamizi uyakatae na uyatupilie mbali. Wamemaliza submissions

Updates; Mawakili upande wa utetezi wamesimama wakiongozwa na wakili Msomi Peter Kibatala. Anaomba mahakama imruhusu kujibu kwa mtindo ule wa 'shaghalabaghala' kwa kuanzia hoja ya mwisho kwenda ya kwanza. Jaji anasema "sawa, endelea".. Anasimama wakili Msomi Jeremiah Mtobesya

Updates; Wakili Jeremiah Mtobesya anajibu majibu ya mawakili wa upande wa Jamhuri. Mtobesya anasema hoja ilikuwa maelezo. Maelezo aina moja hayawezi kutoa mashtaka zaidi ua moja. Anasisitiza kwamba alitoa mfano wa kesi kwa maamuzi ya mahakama kuu na mahakama ya rufaa. Anaendelea

Updates; haiwezekani kushtaki kwa tuhuma za kula njama na ukashtaki kwa kosa lingine kama hilo katika shtaka moja. Kwanini Mahakama kuu imekataza kurudia mashtaka? Jibu ni rahisi mheshimiwa Jaji, njama ni moja ya mashtaka 3 ya aina Incoherent offences (yasiyo ya msingi)

Updates; Wakili msomi Jeremiah Mtobesya anasema Kwanini unafikiri mahakama kuu imeyeweka makosa haya katika kundi hili, ni kwa sababu ya kukwepa kuadhibu au kuzuia kusudi la kutaka kutaka kutenda kosa.. Huwezi kuita haya makosa, hizi ni hatua za kutaka kutenda kosa.

Updates; Wakili Mtobesya anaendelea kama watuhumiwa katika kesi hii wangelikuwa wametenda kosa la kula njama basi kosa lao la kula njama linakuwa kosa halisi (Actual Offence). Mtu ametekeleza, ni wazi hatua alizokuwa anachukua kutekeleza, Makosa yanaweza Kuthibitishwa mahakamani

Updates; Wakili Jeremiah Mtobesya anasema kwa namna hii tunasisitiza kuwa mashtaka na maelezo ya Jamhuri kuwa ni BATILI kwa namna hiyo yanatakiwa kutupiliwa mbali. Mh Jaji, Wakili wasomi wa serikali wameeleza kuwa mashtaka ya kula njama yanajitegemea katika hati ya mashtaka

Updates; Wakili Jeremiah Mtobesya anaendelea kusema, mawakili wa serikali wamekwenda mbali na kusema kuwa maelezo ya makosa katika mashtaka ni tofauti. Simu ya mwendesha mashtaka inaita. Mahakama inasimama kidogo. Jaji nae anakunywa maji kidogo pale, kisha Mtobesya anaendelea

kikao ni kitu kimoja. Ndiyo maana kwanini tunasema hivyo ni kinyume kabisa na kanuni ya siku nyingi inayofahamika na mahakama. Mawakili wa serikali wanasema hatukutoa rejea yoyote. Na akasema kwamba kujirudia siyo kujinakilisha. Hapo Mheshimiwa Jaji, kuna falsafa mbili za mawazo

Updates; Wakili Jeremiah Mtobesya anaendelea kusema Maelezo ya makosa katika mashtaka haya mawili ni kitu kimoja. Yameonekana katika 'mutatis-mutandis'. Maelezo katika shtaka la nne kutoka katika shtaka la kwanza. Muda, tarehe, maeneo na kwa wapanga njama kwa somo husika katika

#Updates; Wapo wanaosema multiplicity & D+duplicity ni kitu kimoja na yanaweza kutumika Interchangeably. Falasafa ya Pili ni wanaofikiri tofauti na hivi, iwe isiwe sisi tunasema hii haibadilishi ukweli kuwa maelezo yanajirudia katika mashtaka. Anasisitiza wakili Jeremiah Mtobesya

Updates; Wakili Mtobesya anaendelea; Maelezo yao mbele yako yanakumbana na UBATILI wa iwe kwa MULTIPLICITY au DUPLICITY kwa sababu sheria inakataa mtu kushtakiwa mara mbili kwa kosa moja. Pamoja na ukweli kwamba kunaweza kuwa na makosa mawili tofauti yanayoweza kuketi pamoja.

Na kwa hivyo ni wakilisho letu kuwa ili mahakama iendelee mbele ijiridhishe kuwa makosa hayo hayajarudiwa katika hiyo hati ya mashtaka iliyopo mbele yako, ma adhabu ya matendo haya yanapaswa kuwa faida ya mshtakiwa wakati wote mheshimiwa Jaji.

Wakili msomi Jeremiah Mtobesya anaendelea kueleza mahakama, ndiyo dhamira ya kifungu cha 70 cha sheria ya utafsiri mahakama, inakata kabisa kurudia mashtaka, na watungaji wa sheria katika kifungu hiki walifikiria kuhusu kumuonea mtu kwa kurudia mashtaka. Na mmoja anahitajika apate uthibitisho wakati wa kikao cha kula njama kinatendeka. Huwezi kuthibitisha kuwepo kwa njama pasipo kuwepo kwa kikao, kiwe kwa njia ya kimwili, kimtandao au byovyote vile. Hivyo ni Ombi letu kuwa kikao ni jambo muhimu katika kuthibitisha Kupangwa njama

Updates; Wakili Mtobesya; Mheshimiwa Jaji niliwasilisha kula njama ni lazima kuwepo na viashiria vya mkutano, lakini mawakili wa serikali wamekataa hivyo wao wanasema mkiwa na mawazo yanayofanana ni kikao tayari. Sisi tunaona wamejipotisha. Kuna Utofauti katika kula njama.

Wakili Mtobesya ananukuu kesi Freeman Mbowe Vs Republic Criminal Appeal No. 76 ya 2020 ukurasa 18 Patagraph ya kwanza. Mahakama ilitafsiri kuwa kuthibitisha njama ni lazima pawe na mtu aliyeshiriki kikao cha njama kwa mmojawapo kushirki kimwili au mtandao katika kutenda kosa hilo

Updates; Wakili Jeremiah Mtobesya anaendelea Kwa maana hiyo tunaendelea kukumbusha na kukuomba kuwa pingamizi yote yaonekane kuwa na mantiki mbele yako. Mwisho nimalizie kesi waliyosema kuwa hawajaiona ya Ahamada Ntimba. Kesi iliyoripotiwa' katika TLR ya 1998. Ukurasa 268.

Updates; Kesi imesimama kwa nusu saa (dakika 30) baada ya Adhana kusikika, kupisha waumini wa kiislam wa mahakama kufanya ibada. Mahakama itarejea baada ya dakika hizo kupita. Tuendelee kusubiri.

Wakati tukiendelea kusubiri mahakama irejee, tuendelee tulipoishia.. Tujadili kidogo, hadi sasa, umebaini nini? Umegundua uwezo wa mawakili wa Freeman na wenzake? Uwezo wa mawakili wa serikali? Uwezo wa Jamhuri kuandaa hati ya mashtaka ya kubumba ambayo inawapa shida sana?

Updates; Kesi imerejea saa 7:47 mchana huu. Jaji anasalimia na anamkaribisha wakili Msomi Peter Kibatala. Na wakili Peter Kibatala anaomba rejea ya kesi ya Steven Salvatory and Magabu Majige Vs Republic nakala ifunguliwe ili aweze kutoa ufafanuzi wake.

Updates; Wakili Kibatala anasema moja ya Jambo la msingi katika kuanzisha kesi ni fact za kisheria na siyo 'individual facsts'. Hoja ya msingi ni kuwa kesi mbili tofuati haziwezi kushtakiwa kwa pamoja kama zina ufanano...Hiyo haikuwa Hoja yetu kwa kweli. Wamechanganya.

Ilikuwa kughushi nyaraka feki siyo kupanga njama na kutengeneza nyaraka feki. Hiyo ndiyo kesi ya Morgan Marick. Tunashukuru mawakili wa serikali kwa kuturejesha kwenye shtaka la 3,5 na 6. Mashtaka ya 4,5 na 6 yote yana uwezo kuwa sehemu moja ya kula njama, kwa kilichoitwa ugaidi.

Updates; Hoja yetu mheshimiwa Jaji ni kuwa huwezi kushtaki kupanga njama na shtaka lingine kwa mkono mwingine kama hilo. Kesi Morgan Marick iliamualiwa kwa kuwepo kwa kesi mbili tofauti kinyume na kupanga njama na kosa lilitendwa mbeleni. Anaeleza Kibatala

Updates; Wakili Kibatala anaendelea kueleza, Tunachokiwasilisha kwako ni kanuni ya msingi ya makosa ya kushtaki makosa ya njama. Kwamba Kama jambo la njama halijatendeka, katika sheria limezuiwa, basi shtaka haliwezi kusimama sehemu zote mbili. Hapa kuna suala la eneo.

Updates; Wakili Kibatala anasema, linapokuja suala la kula njama kwa tarehe fulani na kwa sehemu fulani zilizotajwa kwenye hati DSM, Arusha na Mwanza zinaonekana kwa kila shtaka. Na kutishia jamii ndani ya Jamhuri ya Tanzania, Maneno haya yanajirudia katika mashtaka yote 6.

Updates; Wakati hati inaonyesha makosa hayakuwa yametendeka bado, ukubali au usikubali kula njama na kikao ni kitu kimoja. Wanakwepa wakati kwenye hati ya mashtaka wameonyesha Eneo/mahali kwenye shtaka la 3 na tarehe katika shtaka la 4. Anaendelea kueleza wakili Peter Kibatala.

Updates; Wakili Peter kibatala anaeleza mahakama kwamba "tunaomba mahakama yako tukufu itupilie mbali shtaka la kwanza na la pili kuhusu watuhumiwa kula njama. Kwa ruhusa yako Mheshimiwa Jaji naomba kwenda sasa kwa hoja ya Kwanza."

Updates; Peter kibatala anasema "kwa kifupi wao wameeleza walikuwa na upekee wa mashtaka katika kuyaleta kwa sheria waliyotumia. Lakini sheria hizo zimetofautisha matendo ya kigaidi na matendo mengine yasiyo ya kigaidi na siyo kwa Tanzania bali hata kimataifa. Nitatoa mifano

Updates; Naomba nikupitishe sehemu ya 3 katika kichwa cha habari cha OFFENCES na kabla sijaenda katika yaliyomo naomba niwakumbushe mawakili wasomi wa serikali, kwanini wanao muundo huu ambao kwa maoni yetu sheria hii ina hadhi sawa na sheria zingine. anaeleza Peter Kibatala

Updates; wakili Peter Kibatala anachambua sheria mama ya kimataifa iliyotumika kuunda sheria ya ugaidi jinsi inavyokataza makosa ya kawaida kushtakiwa kama makosa ya kigaidi. Jinsi kesi za ugaidi zilivyo na upekee kushtaki. Jinsi sheria ya ugaidi isivyotumika kwa madhumuni OVU

Updates; Mheshimiwa Jaji naomba pia nitumie hoja ya hawa kaka zetu (mawakili wa serikali) kujichanganya (self contradictory). Ndugu zetu hawajasema kuwa sheria tatu za Uganda, Zambia na Trindad & Tobago zote zimetoka kwa mzazi mmoja (one source). Anaeleza Peter Kibatala.

Updates; Wakili Kibatala anasema, zimetoka kwa chanzo kimoja, kwa Maana hiyo tukiruhusiwa kuzifanyia ulinganisho sheria hizi zote kwa sababu zote zimeanzishwa na chanzo kimoja, kwa maana hiyo tukimjadili mzazi (chanzo cha sheria) tunaruhusiwa kuangalia na watoto wao hawa wanne.

Updates; Kibatala anaendelea, ninayoitumia siyo uamuzi wa mahakama bali mukhtasari wa mahakama. Tuangalie kesi ya Antony Gervas Mgesi, Maamuzi ya mahakama ya Rufaa hayakuangalia pekee mazingira ya kutunga sheria,sana mahakama ya Rufaa imekazia kuwa sheria zetu hazijitoshelezi

Updates; Wakili Peter Kibatala anaeleza Mahakama za Tanzania zimeruhisiwa kuchukua "inspirational quotes" kutoka kwa nchi za Jumuiya ya madola mnapofafana sheria. Ukurasa wa 33 mpaka 38. Mahakama za Tanzania hazijazuiwa na mahakama za Afrika Kusini kurejea jambo lolote.

Kibwagizo kifupi. Hapa Mahakamani, mawakili wa serikali wanatumia lugha ya kiswahili kuwasilisha hoja zao. Mawakili wa Freeman Mbowe na wenzake (upande wa utetezi) wanatumia lugha rasmi ya mahakama (Kiingereza) kuwasiliana na Jaji na kuweka mezani hoja zao. It's what it's....

Mawakili wa serikali wapo watano leo na mpangilio wao wa ukaaji ni 3 mbele na 2 nyuma yao. Wakati mfumo wa ukaaji mawakili wanaomtetea Freeman Mbowe wao 4 mbele, 9 nyuma, nyuma yao tena wapo 4 na nyuma kabisa wapo 2 jumla ya Mawakili wa Freeman ni mawakili wasomi 19.. Tuendelee

Updates; Kibatala anaendelea kusema, Bunge lilikuwa makini sana wakati wanatunga sheria ya ugaidi, uangalizi wa kuachia wigo mpana. Kuzuia Kila mkosaji kushtakiwa kwa makosa ya ugaidi. Kwa uangalifu huo sasa tulipaswa tuuone katika hati ya mashtaka. Hawajafanya huo umakini.

Updates; Kaka zetu wameamua leo hata wasizungumzie kesi ya ya Wilfred Lwakatare ambayo kwa uwazi kabisa imesisitiza yapi ya kushtakiwa kwa ugaidi. tangu Maamuzi ya Mahakama Kuu kutoka kesi ya Lwakatare tunaiomba Mahakama isiogope kutupilia mbali mashtaka haya. Anasema Kibatala

Updates; Bila kutoka nje ya uwezo wetu tunakuomba katika kesi ya Freeman Mbowe kwa umuhimu wake kama ulivyo katika kifungu cha 4(4) cha sheria PTA inaondoa matendo fukani kuwa siyo ugaidi. Mheshimiwa Jaji naomba kuwasilisha hoja ya kwanza.. anasema Wakili Peter Kibatala

Updates; Wakili Peter kibatala anasema, Hoja yetu ya pili, tumesikiliza kwa umakini uwasilishaji wa kaka zetu, hatujasikia kuwa kifungu 4(2) kuwa kinatoa kinga ya matendo yalitotajwa hapo kwamba makosa yote yanaangukia katika Ugaidi. Terrorist intentions was not Defined there.

Updates; Wakili Peter Kibatala anasema, SISI hatujaiomba mahakama kuibatilisha mahakama kama kaka zetu (mawakili wa serikali) walivyokuwa wanataka kusema. Hiyo ni AGENDA nyingine, siku nyingine na mahala Pengine. Hatujasema lolote kuhusu hilo, kaka zetu wasituongoze vibaya.

Updates; Tunachowasilisha ni, kwa kuwa Terrorist Intentions haijafafanuliwa kwenye hati ya mashtaka kwa upekee na kwa kuwa madhumuni ya Bunge hayo maneno yanatengeneza makosa ya ugaidi kukosa maelezo sahihi kwa muktadha huo. Je Mahakama hii inaweza kufanya nini? Anasema Kibatala

Updates; Mahakama hii inaweza kuweka rejea kama Bunge litahitaji. Mfano kesi ya Chiriko Haruni Vs Kangi Lugola & return Officer. Kilichotokea katika Kesi hiyo palikuwa na ukomo wa kusikiliza kesi kwa miezi 6. Wakati Bunge lilitaka kesi iwe imeisha kwa Miezi 6, anasema Kibatala.

Lakini anamkumbusha kinachoongelewa na dhumuni la Bunge kutunga sheria ya Ugaidi na muundo wa makosa yake. Anamuomba Jaji na atamsaidia kumpitisha tena, lakini kwa kuwa leo Ijumaa na saa hizi ni saa 9 amsaidie kwa kifupi sana.. Jaji Luvanda anasema Wakili Kibatala aendeleee.

Updates; Kibatala anaeleza mahakama Kuu ilichofanya haikuingilia mhimili mwingine bali ilijulisha Bunge nini kinatakiwa kufanywa Wakili wa Serikali amesimama na kuomba Kibatala asitunge jambo lolote ambalo hawakulileta awali. KIBATALA anasema huenda wakili wa serikali alisinzia

Wakili Kibatala analinganisha hati ya mashtaka na ule muundo wa makosa ya ugaidi wa Bunge. Mheshimiwa Jaji tunakurejesha kwenye kesi ya Rwakatale kuhusu usahihi wa mashtaka. Na kuhusu UBATILI WA MASHTAKA. Na Kumalizia kwa kesi ya Paul Dionizi iliyoletwa na mawakili wa serikali

Updates; Kibatala anasema Mheshimiwa Jaji unapotaka Kulinganisha hayo mambo mawili kwa neno kwa neno. Kitaalamu inaitwa Canal Knowledge. Kwa Mahakamani hatuendi hivyo. Sheria haziji ghafla. Sheria zinajitosheleza. Shida ipo kwa muandaaji wa MASHITAKA.

Updates; Kibatala anasema Muandaaji alikuwa na hila. Muandaji alikuwa anainajisi sheria. Mheshimiwa Jaji tunarudia tena Maombi yetu kuwa Hmhati ya Mashtaka ni BATILI kwa namna hiyo na tunaomba mashtaka yatupiliwe Mbali. Wakili Kibatala anakaa chini kwa UTULIVU.

Mawakili wa serikali wanaulizana hapa kama wajibu au wapotezee hizo mbanga. Jaji Elianaza Luvanda anasema uamuzi unatoka Jumatatu tarehe 6.9.2021.. Watu wote wanasimama. Jaji anatoka. Kesi imehairishwa.... Ahsante!

Updates; Wakili Jeremiah Mtobesya anasema na hapo ndipo tukaja na sheria za kesi zinazoungana na tulichokiwasilisha, kwamba huwezi kumshtaki mtu kwa makosa yasiyo halisi dhidi ya makosa halisi kwa mashtaka hayo hayo. Mheshimiwa Jaji ukiangalia shtaka la 5 & 6
 
Kesi ya Ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake watatu inaendelea kuunguruma kwenye Mahakama ya Uhujumu uchumi , Ambapo mvutano wa kisheria umekuwa mkali hasa baada ya Mapingamizi yaliyowekwa na Mawakili wa Mbowe kuwa ya moto .

Kesi imeahirishwa kwa muda ili kuiruhusu Mahakama kupitia mapingamizi hayo na ufafanuzi wa mawakili wa serikali
Mungu mbariki mbowe , mtetee, pia mtoe katika mikono ya watesi wake!
Daima uwe upande wake!
 
Back
Top Bottom