Mahakama ya Rufani yaamuru Kesi ya Wasira na Bulaya isikilizwe upya

Bukanga

JF-Expert Member
Dec 13, 2010
2,857
1,934
Wafuasi wa aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Bunda Mjini, Steven Wassira wamembwaga mahakamani mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Ester Bulaya wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika rufaa yao ya kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu kutupilia mbali kesi yao.

Wafuasi hao, Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Escietik Malagila walifungua kesi ya uchaguzi kupinga ushindi wa Bulaya katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, wakijitambulisha kama wapigakura.

Hata hivyo, Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, katika uamuzi wake uliotolewa na Jaji Mohamed Gwae ilitupilia mbali kesi yao baada ya kukubaliana na pingamizi la wakili wa Bulaya, Tundu Lissu kuwa hawakuwa na haki ya kisheria kufungua kesi hiyo.

Chanzo: Mwananchi
 
Huyo Mzee Stephen Wasira anatakiwa apumzike tu.

Hawa wazee wa aina ya Wasira wanaziba mpaka nafasi za wajuu wao kuwa wabunge.

Yaani yeye toka uhuru wa Tanzania yupo tu kwenye siasa.

Tunahitaji fikra mpya.

Kung'ang'ania madaraka kwa njia hii ni aina fulani ya ufisadi ambayo inatakiwa bunge litunge sheria ya kikomo cha ubunge kwa mtu akifikisha miaka 70.
 
Huyo Mzee Stephen Wasira anatakiwa apumzike tu.

Hawa wazee wa aina ya Wasira wanaziba mpaka nafasi za wajuu wao kuwa wabunge.

Yaani yeye toka uhuru wa Tanzania yupo tu kwenye siasa.

Tunahitaji fikra mpya.

Kung'ang'ania madaraka kwa njia hii ni aina fulani ya ufisadi ambayo inatakiwa bunge litunge sheria ya kikomo cha ubunge.
Kabisa
Hivi yule mbunge wa Moshi mjini NdesaPesa yeye alifanya je?
 
Mzee NdesaPesa ameamua kuwaachia wajukuu zake ubunge. Kitendo cha Mzee NdesaPesa kustaafu ubunge ni heshima kubwa sana.

Mzee NdesaPesa ameondoka kwenye siasa akiwa na heshima zake, lakini huyu Wasira anataka kuondoka kwenye siasa baada ya kukosa heshima.

Mzee Wasira anadhani ubunge wa Bunda Mjini ni mali yake na atautoa kwa mapenzi yake.
 
Huyo Mzee Stephen Wasira anatakiwa apumzike tu.

Hawa wazee wa aina ya Wasira wanaziba mpaka nafasi za wajuu wao kuwa wabunge.

Yaani yeye toka uhuru wa Tanzania yupo tu kwenye siasa.

Tunahitaji fikra mpya.

Kung'ang'ania madaraka kwa njia hii ni aina fulani ya ufisadi ambayo inatakiwa bunge litunge sheria ya kikomo cha ubunge.
Hawa watu walilelewa kizembe kubebwa bebwa na hakujiandaa kwa maisha mengine baada ya siasa, JPM kaja analimisha watu kwa meno ndio wanakumbuka shuka asubuhi

Huku ni kupoteza muda na fedha za walipa kodi kwani hajui kuwa his time is up?
 
Mzee NdesaPesa ameamua kuwaachia wajukuu zake ubunge. Kitendo cha Mzee NdesaPesa kustaafu ubunge ni heshima kubwa sana.

Mzee NdesaPesa ameondoka kwenye siasa akiwa na heshima zake, lakini huyu Wasira anataka kuondoka kwenye siasa baada ya kukosa heshima.

Mzee Wasira anadhani ubunge wa Bunda Mjini ni mali yake na atautoa kwa mapenzi yake.
Hamuoni Lyatonga alivyobadili gia ghafla na kuamua kukubali yaishe?
 
kesi ikirudi mahakamani wassira anashinda asubuhi.. na baada ya hapo ni sehemu zote walizoshinda upinzani lazima wakatiwe rufaa.....
 
Hawa watu walilelewa kizembe kubebwa bebwa na hakujiandaa kwa maisha mengine baada ya siasa, JPM kaja analimisha watu kwa meno ndio wanakumbuka shuka asubuhi

Huku ni kupoteza muda na fedha za walipa kodi kwani hajui kuwa his time is up?
Hatukatai Mzee Wasira kugombea Ubunge kwa sababu ni haki yake kisheria.

Tunachokataa ni kutumia haki yake ya kugombea ubinge bila busara.

Mzee Wasira anatakiwa awape wajukuu zake hiyo fursa ya kulitumikia Jimbo la Bunda Mjini.
 
Hivi wale wazungu wa amerca hawapo huko bunda wamtungue hyo bichwa lake? hii nchi kaila sana lakini haliridhiki
 
wazee Kama wasira ni hazina waende vyuoni kutoa mihadhara Au kufundisha wasingangania siasa hata historia ije iwakumbuke .
 
Siasa ni noma mkuu, unakuta watu na taaluma zao kama vile DR,Professors, wanakimbilia siasa!!!!
 
Back
Top Bottom