Mahakama ya Rufaa yasikiliza Rufaa ya Jamhuri dhidi ya Masheikh wa Uamusho

Sep 19, 2019
35
400
Bismillahir Rahmanir Rahiim

SHURA YA MAIMAMU TANZANIA

MAHAKAMA YA RUFAA YA SIKILIZA RUFAA YA JAMHURI DHIDI YA MASHEIKH

Leo tarehe 07/05/2021 Mahakama ya Rufaa chini ya Majaji watu imesikiliza Rufaa ya Jamhuri dhidi ya Masheikh inayo pinga Hukumu ya Mahakama Kuu iliyofuta mashitaka 14 kati ya mashitaka 25 yaliyo kuwa yakiwakabili Masheikh na waislaam.

Hukumu hiyo iliyo futa mashitaka hayo 14 ilitolewa na Jaji wa Mahakama Kuu tarehe 23/04/2021.

Katika rufaa hiyo iliyo sikilizwa leo, hoja za kisheria zimetolewa kutoka pande zote mbili za Mawakili. Upande wa Utetezi ulikuwa na Mawakili 9 wa kiongozwa na Wakili Juma Nasor. Na upande wa Jamuhuri ulikuwa na mawakili 11 wa kiongozwa na Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP).

Katika shauri hilo zito hoja za mahusiano na mgongano wa kisheria katika mambo ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zimejitokeza na kuchukua nafasi kubwa ya kujadiliwa. Huku mawakili wa masheikh wakionyesha nguvu na uwezo wa kisheria wa Mahakama Kuu ya Zanzibar kusikiliza shauri hilo la masheikh.

Shauri hilo lenye mguso mkubwa wa kijamii na kidini limesikilizwa na Majaji wa Mahakama ya Rufani, Mheshimiwa Stella Mugasha (J. A), Mheshimiwa Shaaban Lila (J. A), na Mheshimiwa Korsso (J. A).

Aidha shauri hilo limekamilika kusikilizwa leo katika Mahakama ya Rufani na pande hizo mbili zitaitwa tena hapo Mahakamini tarehe itakayopangwa kwaajili ya uamuzi.

Hukumu ya Mahakama ya Rufaa italirudisha shauri hilo Mahakama Kuu kuendelea chini ya hati yenye mashtaka 25, ya awali au ikubaliane na mawakili wa masheikh kuwa kesi iendelee na hati mpya yenye mashtaja 11 kama ilivyoamuliwa awali na mahakamakuu.

Aidha Shura ya Maimamu Tanzania inawaomba Watanzania kufuatili kwa karibu mashauri haya ya ugaidi dhidi ya Waislamu ili kubaini ukweli kwa maslahi ya umoja wa Watanzania na Taifa kwa jumla.

Ust. Ibrahim Z. Mkondo
Msemaji wa Shura.
0713118812
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom