Mahakama ya Rufaa yabatilisha uamuzi wa Mahakama Kuu kesi ya dhamana ya makosa makubwa

Majaji wanatamka mtu aliyetenda makosa makubwa?

Majaji wanajua vipi pasi na shaka mtuhumiwa wa makosa makubwa kweli ametenda kosa bila huyo mtuhumiwa kufikishwa mahakamani na kisha kupatikana na hatia kupitia mchakato wa kesi kusikilizwa na kuhukumiwa kuwa alitenda kosa kubwa analotuhumiwa nalo !
 
Tangu asubuhi nilitegemea uamuzi wa aina hii. Maana siku hiza wana andikiwa wasome tuu
 
6 August 2020
LIVE: WAKILI MKUU AZUNGUMZIA Walivyoshinda MAHAKAMA YA RUFAA Dhidi ya DHAMANA Kwa MAKOSA MAKUBWA


Wakili Mkuu wa Serikali, Bwana Gabriel Malata, amezungumza na wanahabari na kufafanua kuhusu hoja walizotumia na kushinda kesi Mahakama ya Rufaa dhidi ya wakili wa kujitegemea Bwana Dickson Paulo Sanga aliyeshinda kesi Mahakama Kuu ya Tanzania akitaka watuhumiwa wa makosa ya uhujumu uchumi, mauaji na ubakaji, nao wawe wanapewa dhamana kwani ni haki yao kikatiba. Amesema kwa kuzingatia hayo, Mahakama ya Rufaa imefuta hukumu ya Mahakama Kuu na kueleza kuwa Kifungu cha 148 (5) (a) (i), (ii), (iii), (b), (c), (d) na (e) Sheria ya Mwenendo wa Jinai Sura ya 20 ya Sheria za Tanzania hakikinzani na Ibara ya 13 (3) na 15(1) na (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania badala yake kinalenga katika kuwezesha utekelezaji mzuri wa Ibara ya 30 (2) inayolenga katika kuhakiksha kwamba haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma haviathiriwi na matumizi mabaya ya uhuru na haki za watu binafsi na pia kuhakikisha ulinzi, usalama wa jamii, amani katika jamii, maadili ya jamii, afya ya jamii na utekelezaji mzuri wa mipango ya maendeleo ya jamii.


Source : Global TV online
 
Mahakama na Majaji hawanatofauti na wajumbe wa ccm, akili kidogo ubabaishaji mwingi. We have a hopeless court , a typical qualified Kangaroo Court.
 
20 Jul 2019
JAJI MKUU : SASA MAKOSA YOTE KUWA NA DHAMANA KAMA KENYA, ASIKITIKA WATUHUMIWA KUKAMATWA KABLA YA UPELELEZI KUKAMILIKA

20 Jul 2019
Jaji Mkuu wa Tanzania Ibrahim Juma ameitaka serikali kupitia upya sheria inayowafanya Mahabusu kujazana katika magereza kwa kisingizio cha kutokamilika kwa uchunguzi

Source : Global TV online
 
Kwahiyo kwa mujibu wa Majaji mtuhumiwa anakuwa ni mkosaji kwa hoja yao ya kulinda usalama na uhai wa wengine?
haki za binadamu zote zinalindwa na masharti mawili makubwa; kutokumia haki hizo kuvunja shera za nchi, na vile vile kutokutumia haki hizo kuvunja haki za binadamu wengine.
 
JAJI MKUU APENDEKEZA MAKOSA YOTE KUWA NA DHAMANA
26-07-2019 0



Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amependekeza makosa yote kuwa na dhamana kwa kuwa hatua hiyo itasaidia kuondoa msongamano wa Mahabusu kwenye Magereza mbalimbali nchini.

Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kuwakubali na kuwaapisha wanasheria waliomaliza mafunzo ya Sheria kwa vitendo kuwa Mawakili, jijini Dar es salaam Julai 19, 2019, Jaji Mkuu ameyataja baadhi ya mapendekezo ya Mahakama yatakayosaidia kuondoa msongamano magerezani kuwa ni pamoja na upelelezi wa kesi kumalizika mapema.

Jaji Mkuu alisema Mahakama imekuwa ikilaumiwa kwa kuchelewesha kesi mahakamani lakini kinachosababisha kuchelewa kwa mashauri hayo ni upelelezi kutokukamilika kwa wakati.

“Kuchelewa kumalizika kwa shauri Mahakamani wa kulaumiwa ni wapelelezi na siyo Mahakama”, alisema Jaji Mkuu.

Alisema pendekezo jingine ni sheria kutamka wazi muda wa kufanya upelelezi yaani ikifika muda fulani upelelezi haujakamilika basi shauri hilo lifutwe mahakamani.

Alisema sheria zimeegemea zaidi kwenye adhabu kubwa huku akitolea mfano wa mashauri ya mauaji, matumizi ya dawa za kulevya, Uhujumu uchumi na ubakaji. Aliongeza kuwa mashauri haya yana adhabu kubwa na upelelezi wake huchukua muda mrefu.

Alisema ili kutatua changamoto ya msongamano wa mahabusu magerezani, Mahakama ya Tanzania pia inapendekeza masharti ya dhamana kulegezwa na kushauri kutumiwa kwa vitambulisho vya Taifa kwenye dhamana.

“Hivi sasa wananchi wengi wana vitambulisho vya Taifa ambavyo vinaweza kutumika kama dhamana bila ya kumtaka mwananchi aonyeshe mali”, alisema Prof. Juma.

Jaji Mkuu alitoa mapendekezo hayo ya Mahakama alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na waandishi wa habari waliotaka kufahamu Mamlaka ya kutoa Mahabusu gerezani. Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, Mahakama ndiyo yenye Mamlaka.

Hivi karibuni, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliagiza kufanyika kwa uhakiki ili kubaini mahabusu na wafungwa waliobambikiwa kesi hatimaye kuachiwa huru. Watakaonufaika na matokeo ya uhakiki huo ni mahabusu wenye kesi ndogondogo na wafungwa watoto, wazee, na makundi mengine yenye mahitaji maalum.



Jumla ya wanasheria 720 wamekubaliwa na kuapishwa kuwa Mawakili wakiwemo Majaji nane wa Mahakama ya Rufani, Majaji saba wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Majaji wastaafu watatu, Manaibu Wasajili kadhaa, Mahakimu pamoja na wanasheria wengine.

Hii ni mara ya 60 kwa Mahakama ya Tanzania kuwakubali na kuwaapisha Mawakili wapya. Kwa mara ya kwanza Mahakama ya Tanzania iliwakubali na kuwaapisha Mawakili wapya mwaka 1986.

Source : JAJI MKUU APENDEKEZA MAKOSA YOTE KUWA NA DHAMANA
 
Mimi nashangaa huku Mh. Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Hamis Juma mawazo yake yanapingana na bench la Majaji 5 wa Mahakama ya Rufaa Tanzania.

Ningeelewa kama katika rufaa iliyowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa serikali katika shauri hili la Wakili msomi Dickson Paul Sanga, basi katika Majaji 5 angalau au Jaji mmoja au wawili wangekubaliana na Maamuzi ya Mahakama Kuu na hivyo uamuzi ukawa 3 : 2 na siyo 5:0 ambapo majaji wote wa Mahakama ya Rufani wanapingana na mawazo ya Mahakama Kuu na mawazo ya Jaji Mkuu kuwa dhamana ni haki ya msingi ikiwa mazingira mfano kesi ya uhujumu uchumi upelelezi haujakamilika.
 
Mahakama ya Rufaa ni hovyo kabisa, imejaa walamba viatu wa CCM

Hao majaji wa Mahakama ya rufaa kila wakati wanafuta maamuzi ya mahakama kuu yenye mrengo wa kulinda haki za wananchi.

Nahisi Lissu alikuwa sahihi , Tuna baadhi ya majaji vilaza, wamejazana kwenye mfumo wa mahakama nchini.

Hii mahakama ya Rufaa hopeless kabisa.

Hii mahakama ya rufaa imeshindwa kuona kuwa kuna makosa kama ya uhujumu uchumi ambayo yanatumika kisiasa kuumiza watu

Majaji wa Mahakama ya rufaa wachunguzwe uwezo wao wa akili, naona kama Upeo wao ni mdogo sana Au la basi watakuwa na Kadi za CCM kimyakimya kama aliyokuwa nayo Jaji Augustino Ramadhani
 
Back
Top Bottom