Zapa RadioFm
Senior Member
- Feb 12, 2016
- 112
- 171
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Pwani imetengua rasmi matokeo ya uchaguzi ya Kata ya Misugusugu, Jimbo la Kibaha Mjini yaliyompa ushindi wa kiti cha Udiwani mgombea wa CCM, Adhudadi Mkomambo katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana.
Hukumu hiyo imetokana na kesi ya kupinga ushindi huo iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa kiti hicho kupitia Chadema, Gasper Ndakidemi.
Katika kesi hiyo, Ndakidemi alikuwa akidai kuwa mgombea huyo wa CCM alitumia kura zisizo zake kujipatia ushindi.
Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Pwani, Elizabeth Nyembele baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa walalamikaji.
Hakimu Nyembele alisema katika uchaguzi huo, mgombea wa nafasi ya udiwani katika Kata ya Misugususugu kupitia Chadema, Ndakidemi, alipata kura nyingi dhidi ya Mkomambo.
Lakini makosa yalifanyika wakati wa kumtangaza mshindi na kwamba, ushindi ulikwenda kwa Mkomambo isivyo halali.
“Mgombea wa Chadema alipata kura nyingi lakini kulitokea makosa wakati wa majumuisho, baada ya Mahakama kujiridhisha na ushahidi, natengua rasmi matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Mkomambo na uchaguzi katika kata hiyo itabidi urudiwe,” alisema Hakimu Nyembele.
Alisema katika uchaguzi huo, Ndakidemi alipata kura 1,525 dhidi ya Mkomambo aliyepata kura 1,515, lakini matokeo yalitangazwa kwa kumpa ushindi mgombea huyo wa CCM kwa kura 1,545.
Aliyekuwa mlalamikaji, Ndakidemi alisema baada ya kubaini ukiukwaji huo wa makusudi uliofanywa na msimamizi wa uchaguzi huo, chama chake kililazimika kwenda mahakamani kupinga matokeo.
“Katika matokeo ya uchaguzi huo, mimi nilipata kura nyingi tofauti na mwenzangu, lakini leo (Juzi) Mahakama imetenda haki kwa kutengua matokeo hayo, naishukuru kwani imeenda haki,” alisema Ndakidemi.
Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Kibaha Mjini, Bumija Senkondo alisema hatua inayofuata kwa sasa ni kufuatilia kwa wanasheria nakala ya mwenendo wa kesi na hukumu na baadaye kusikiliza ushauri wao kwani chama kipo tayari kwa jambo lolote, ikiwa ni kurudia uchaguzi au kukata rufaa huku akiwataka wanachama kujiweka tayari.