Mahakama ya Mwanzo Ukonga imekataa ombi la Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga kumtaliki mkewe

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Mahakama ya Mwanzo Ukonga leo imekataa ombi la Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga kumtaliki mkewe, Ruth Osoro aliyefunga naye ndoa Serikalini Februari 21, 2010 na kupata cheti cha ndoa B no 0979341

Katika kesi hiyo, Odunga ambaye ni mdai alitoa ushahidi mwenyewe huku mkewe akitoa ushahidi wake na mashahidi wawili akiwepo dada yake na mke mwenza wa ndoa ya Kikristo na Odunga

Odunga alilalamikiwa na mkewe Ruth kwa kutokutoa mafunzo ya mtoto wao wa kiume (4) kwa kipindi cha miaka mitatu

Licha ya malalamiko hayo Ruth aliomba Mahakama isivunje ndoa yake kwa kuwa bado anampenda mume wake huku Odunga akitaka ndoa ivunjwe na apewe ridhaa ya kumlea mtoto huyo
 
Licha ya malalamiko hayo Ruth aliomba Mahakama isivunje ndoa yake kwa kuwa bado anampenda mume wake huku Odunga akitaka ndoa ivunjwe na apewe ridhaa ya kumlea mtoto huyo patamu hapa
 
Dah! Hawa mabinti wa kileo ukimzaba kofi moja anarudi kwao, wajifunze kwa huyu mwanamke...
Mwanamke anampendea huo ukuu wa wilaya.

Kapuku aige ajifanye anataka talaka aone atakavyoachiwa manyoya huku analia hadi anapenga kamasi.
 
Licha ya malalamiko hayo Ruth aliomba Mahakama isivunje ndoa yake kwa kuwa bado anampenda mume wake huku Odunga akitaka ndoa ivunjwe na apewe ridhaa ya kumlea mtoto huyo patamu hapa
Hapo kweli ngoma inogile๐Ÿ™†๐Ÿฝโ€โ™‚๏ธ๐Ÿ™†๐Ÿฝโ€โ™‚๏ธ
 
Hili litathibitishwaje mahakamani endapo litatokea?
๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜
Mahakama inatuma Polisi waje kukukamata. Mnapelekwa kwenye ofisi hapo mahakamani mnafungiwa, unaambiwa umshughulikie mwenzako at a gun point hadi aridhike... Mwenzako anaulizwa umeridhika? Akisema tayari ndio unaachiwa hadi baada ya wiki unakamatwa tena...Natania.
 
Dar es Salaam. Mahakama ya Mwanzo ya Ukonga, Dar es Salaam nchini Tanzania imekataa ombi la Mkuu wa Wilaya ya Chemba (DC) mkoani Dodoma, Simon Odunga kumtaliki Ruth Osoro.

Hakimu Elia Mrema ametoa hukumu hiyo leo Ijumaa Agosti 23,2019 baada ya kusikiliza ushahidi uliotolewa na mashahidi wa pande zote.Mbali na kukataa ombi la talaka, imemuamuru Odunga kutoa Sh250,000 za matunzo ya mtoto kila mwezi, kuanza sasa hadi atakapofikisha umri wa miaka 18.

Mtoto huyo hivi sasa ana umri wa miaka minne. Odunga pia ametakiwa kugharamia matibabu na masomo ya mwanaye.
Akitoa hukumu hiyo, hakimu Mrema amesema Mahakama ilijiuliza endapo kuna ndoa halali baina ya Odunga na Ruth.
Alifafanua tafsiri ya ndoa ni muungano wa hiari kati ya mume na mke kwa kusudi la kuishi pamoja katika siku zote za maisha yao.

Amebainisha katika sheria ya ndoa, kuna ndoa ya mke mmoja na ndoa ya mke zaidi ya mmoja.
Habari zinazohusiana na hii

Hakimu Mrema amesema kulingana na cheti cha ndoa iliyofungwa bomani kati ya Odunga na Ruth inaonyesha mkuu huyo wa wilaya hajawahi kuoa wala mdaiwa hajawahi kuolewa.

Lakini kabla ya kuhitimisha cheti hicho cha ndoa, Mahakama ilikilinganisha na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na Odunga ambao haukuwa na uwazi kuwa wakati anamuoa Ruth mwaka 2010, mwanamke huyo alikuwa akitambua kuwa anaishi na mwanamke mwingine na akaridhia.

Kwa habari zaidi soma gazeti la Mwananchi kesho Jumamosi Agosti 24,2019
 
Licha ya malalamiko hayo Ruth aliomba Mahakama isivunje ndoa yake kwa kuwa bado anampenda mume wake huku Odunga akitaka ndoa ivunjwe na apewe ridhaa ya kumlea mtoto huyo patamu hapa
Hapa ndipo ulipo ujinga wa mahakama, sasa mwanaume ashasema hamtaki yeye analazimisha kuwa anampenda anategemea nini na tayari anajua ana mke mwingine si ulofa huo.
.
Hilo janamke linataka hela tu halina lolote la kuchoma mkaa
 
Kiufupi zitamtoka 42mil kama matumizi ya mtoto kwa hiyo miaka 14 iliyobakia
Mshahara kabisa
 
Back
Top Bottom