Mahakama ya Mwanzo Kariakoo yadaiwa kukosa wino kwa ajili ya ku-print Hukumu. Ni zaidi ya mwezi sasa

activist

Senior Member
Jan 3, 2014
123
225
Kwa muda wa mwezi mmoja sasa Mahakama ya Mwanzo Kariakoo iliyopo Upanga imeshindwa kuwapatia wananchi nakala ya hukumu kwa kisingizio kuwa hawajatumiwa fungu kwa ajili ya kununua WINO wa printa.

Tunaomba serikali na idara ya mahakama kumulika changamoto hii isije kuwa ni namna ya kumuhujumu Rais.

Wananchi wanacheleweshewa haki zao ikiwepo kukata rufaa bila sababu za msingi
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
47,262
2,000
Kwa muda wa mwezi mmoja sasa mahakama ya mwanzo kariakoo iliyopo upanga imeshindwa kuwapatia wananchi nakala ya hukumu kwa kisingizio kuwa hawajatumiwa fungu kwa ajili ya kununua WINO wa printa...
Zile pesa za faini wanapeleka wapi?
 

activist

Senior Member
Jan 3, 2014
123
225
Yaani ni aibu sana. Mimi hukumu imetoka zaidi ya mwezi uliopita lakini ukienda naambiwa bado hawajatumiwa fungu ili wanunue wino.
 

GwaB

JF-Expert Member
Mar 19, 2014
1,894
2,000
Mbona Iko hivyo kwenye mahakama zetu tangu zamani ?. Ingia mfukoni ugharamie wino wakuchapie Makala yako ya hukumu kama kuna mahali inahitajika, vinginevyo itakula kwako!.
Uzoefu; .... Nilikuwa nadhani kuwa watendaji wa mahakama zetu hawaombi rushwa, nilikosea wanaomba kwa uangalifu sana kupitia mtu wa tatu au vipi watachelewesha zoezi.
 

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
3,250
2,000
Kwa muda wa mwezi mmoja sasa mahakama ya mwanzo kariakoo iliyopo upanga imeshindwa kuwapatia wananchi nakala ya hukumu kwa kisingizio kuwa hawajatumiwa fungu kwa ajili ya kununua WINO wa printa.

Tunaomba serikali na idara ya mahakama kumulika changamoto hii isije kuwa ni namna ya kumuhujumu Rais.

Wananchi wanacheleweshewa haki zao ikiwepo kukata rufaa bila sababu za msingi
kwa nini umekosa uvumilivu wakati umepewa jibu lilo wazi tu!
huu sasa ni uchonganishi au tunaweza kuyaita Majungu.
ungekuwa umeombwa Rushwa hapo sawa mara moja angekamatwa.
kama unaona ulicho ambiwa sio kweli fanya uchunguzi au toa ripoti
 

Msingida

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
7,772
2,000
Hali dhaifu sana kwa watafsiri sheria wetu.
Wajiongeze walao watoe hukumu hata kwa soft copy!
 

CONTROLA

JF-Expert Member
Sep 15, 2019
5,600
2,000
Wino si sababu kuna sababu nyingine msizozijua,nchi ina siri sana hiiii halafu siri za ajabu ajabu kijanja janjaaaa...
 

Elli M

Verified Member
Mar 17, 2008
42,351
2,000
Yaani ni aibu sana. Mimi hukumu imetoka zaidi ya mwezi uliopita lakini ukienda naambiwa bado hawajatumiwa fungu ili wanunue wino.
Hahahaha unakosea sana, yaani hapo ukimpa buku kumi tu utashangaa wino unapatikana na hukumu inaprintiwa na wanakukaribisha tena
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom