Mahakama ya mafisadi ni ufujaji wa fedha zetu

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
20,385
38,655
Hivi ni jambo gani ambalo mashitaka yake hayawezi kusikilizwa kwenye hizi mahakama zetu zilizopo hivi sasa mpaka serikali itumie fedha kuanzisha mahakama itakayoitwa ya Mafisadi? Hiyo Mahakama itaendeshwa kwa kutumia sheria hizi hizi tulizonazo au itakuwa na sheria zake zinazojitegemea?

Mahakama hiyo ya Mafisadi ni takwa la Tawi la sheria (judiciary) au takwa la tawi la utawala (executive)? Faida yake ni ya kisiasa kwa ajili ya kuzifurahisha hisia binafsi (Adventure) za watawala au ni kwa faida ya jamii nzima ya watanzania kwa ajili ya kuliondoa tatizo la ufisadi liliota mizizi?

Waendesha mashitaka watakuwa chini ya DPP au watajitegemea, Upelelezi utafanywa na Polisi au kitaundwa chombo maalum cha kufanya kazi hiyo ya kupeleleza? Hao wasafi wa kuendesha mchakato wa Mahakama hiyo ni kina nani hasa.

Hivi mafisadi hawashtakiki kwa kuwa hawana mahakama yao na sheria zinazowabana au tatizo ni nini hasa? Tunamkubuka Sokoine kwa kupambana na Mafisadi enzi za miaka ya 80 yeye alitumia mahakama zipi na sheria zipi? Tunataka kusema kwamba mahakama na sheria zetu ni dhaifu kiasi kwamba haziwezi kuwabana mafisadi itakiwavyo?

Huu ni ufujaji wa fedha zetu usio na sababu!!
 
Wewe ndiyo hujui kitu tatizo lenu bavicha upeo mdongo kila mtu anataka mahakama ya mafisa wewe ndiyo unashangaa mwache Rais achape kazi.
Jibu hoja kwa hoja. Kuna sababu ya kuanzisha hiyo mahakama ya Mafisadi? Kwani mahakama zilizopo zimeshindwa kusikiliza kesi za ufisadi? Kina Mramba na mwenzake wamehukumiwa na mahakama zipi kama si hizi zilizopo?
 
Mahakama hiyo inaanzishwa kutokana na uhitaji na umuhimu. Hakuna tofauti na mahakama nyingine isipokuwa hiyo ni specialized na mahakimu ni hawa hawa waliopo, ndio maana kuna mahakama ya kazi, mahakama ya nyumba, ya biashara . hii itaharakisha maamuzi kwani inahusu maslahi ya nchi kiuchumi na kijamii hata kama kesi nyingine ni hivyo hivyo lakini swala la uhujumu ni sensitive. Hakutakuwa na gharama zaidi ya kuokoa muda bajeti ya mahakama ni hiyohiyo.
 
akiri kama hz ndo zinafanya CCM izidi kuwa dharau nyny wapnzan maana hamweleweki nn mnataka, mlilia mkwere kusafiri sana nje ya nchi huyu wa sasa hafanyi hvyo, bado tena mnalia, mlisema mkwere mpole amekuja huyu wa sasa ni mkali tena bado mnalia, kama watoto wadogo kwa jinsi mnavyolalamika tumewachoka aseeeh, haraf leo mkuu umeamkaje, maana nikihesabu huu ni uzi wa pili kuuanzisha YAANI SIAMINI KAMA NI WW!!!!?
 
Sijajua lengo hasa la kuanzishwa kwa hiyo kamahama ya mafisadi lakini kwa ufupi hakuna tija.
Wale watuhumiwa wa EPA walihukumiwa lakini mwisho wake wengi wako nje kwa kisingizio cha ushahidi au kushinda rufaa.
Hapo tatizo sio aina ya mahakama ila ni nia ya dhati ya kupambana na ufisadi.

Ilitakiwa uchunguzi/ utafiti na upembuzi ufanyike kujua kwanini kesi zote zinaendeshwa kwa kusuasua, tatizo hasa liko wapi? Ni utaalamu wa au rasilimali watu? Ikumbukwe tuna jeshi la polisi, wapelelezi, takukuru, wote hao wanamchango mkubwa sana kwenye uendeshaji wa kesi na wanatumia pesa yetu hiyo hiyo ambayo bado haitoshi kutimiza mahitaji yaliyopo.

Sasa unaposema unaanzisha mahakama ya mafisadi utatumia muundo au mbinu gani kuharakisha au kuendesha hizo kesi kwa ustadi na ubora zaidi kuliko sasa hivi kesi zinavyoendeshwa? Na kama kuna njia ambayo itatumika kwenye hizo mahakama, kwanini isitumike kwenye mahakama zilizopo ilikuharakisha ufumbuzi wa kesi za aina zote?

Mahama ya mafisadi hakuna cha maana zaid ya kufuja pesa za walipa kodi tu.
 
ndio maana kuna mahakama ya kazi, mahakama ya nyumba, ya biashara .
Unajua kwamba masuala ya Kazi, Ardhi na biashara matatizo yake ni mapana na ya kudumu sana na sheria zake nyingi zimetungwa kutokana na kuridhia mikataba mbalimbali ya kimataifa. Hata hivyo kwenye suala la Nyumba na Ardhi z yale ni Mabaraza yaliyoanzishwa na sheria yake na hayako chini ya mfumo wa Mahakama.

Lakini ufisadi ni jinai, na ndiyo maana hata huko kwenye Kazi, Ardhi na Nyumba au Biashara inapofanyika jinai kesi zake huwa hazipelekwi kwenye mahakama hizo bali hupelekwa kwenye mahakama za kawaida. Jee Jinai hii ina sababu gani ya kufunguliwa mahakama yake maalum? na hiyo mahakama itakuwa ni ya kudumu au ni ya muda maalum?
 
Mbona kesi za ubunge zinatumia ma billion ili kukidhi matakwa ya demokrasia?

Mahakama ya mafisadi ni muhimu ije ili wale wanaosema wanaonewa wasafishwe na mahakama hiyo.
 
akiri kama hz ndo zinafanya CCM izidi kuwa dharau nyny wapnzan maana hamweleweki nn mnataka, mlilia mkwere kusafiri sana nje ya nchi huyu wa sasa hafanyi hvyo, bado tena mnalia, mlisema mkwere mpole amekuja huyu wa sasa ni mkali tena bado mnalia, kama watoto wadogo kwa jinsi mnavyolalamika tumewachoka aseeeh, haraf leo mkuu umeamkaje, maana nikihesabu huu ni uzi wa pili kuuanzisha YAANI SIAMINI KAMA NI WW!!!!?
Ha! Ha! Ha! Ha! Ha! Ni mimi bwana na huwa sina tabia ya kumpa mke wangu pass word ya akaunti yangu kama anavyofanya Dr. Mihogo kwa "Mchumba" wake.

Turudi kwenye mada.Kuna wakati CHADEMA/UKAWA waliwahi kusema kuwa wakichaguliwa wataunda mahakama maalum ya kushughulika na Mafisadi?
 
Wewe ndiyo hujui kitu tatizo lenu bavicha upeo mdongo kila mtu anataka mahakama ya mafisa wewe ndiyo unashangaa mwache Rais achape kazi.
Hivi wewe, si kila kitu una ufahamu nacho. Vingine waachie wenye weledi watufafanulie. Huoni mleta uzi alivyoliweka suala hilo la mahakama ya kadhi kuwa linavunja katiba? Hakuna katika nchi yoyote rais anaanzisha mahakama. Jiulize mahakama hii itadumu kwa muda gani iwapo mafisadi wote watashtakiwa na kuisha? Kama watakuwa wametengenezewa miundo mbinu je, itafanyiwa kazi gani mbadala? Na huu ni ufujaji wa hiki kidogo kilichopo kwani ni gharama kubwa mno. Magufuli wananchi hawahitaji mahakama ya mafisadi bali uchumi imara. Kama ni lazima, tuundie na ya madawa ya kulevya.
 
Mahakama ya mafisadi imeanzishwa kutokana na mahitaji ya wakati. Tatizo la watu kuuhujumu uchumi wa nchi limekuwa kubwa sana. Enzi za Sokoine walikuwepo wahujumu wa uchumi lakini hawakuwa ni wale wa kiwango cha kuficha mabilioni kule uswisi. Hawakuwa ni wa kiwango cha EPA na ESCROW.

Dunia haikuwa na maendeleo makubwa sana ya teknolojia kama hivi leo, hata wanaohujumu uchumi na wao wamekuwa sophisticated katika wizi wao kadri miaka inavyozidi kupita. Wingi wa mafisadi, wingi wa kile wanachokiiba, madhara ya wizi wao katika ustawi wa nchi, vyote hivyo ni vigezo vilivyochangia katika uibukaji wa umuhimu wa kuuchukulia ufisadi kama tatizo linalohitaji idara maalum ya mahakama.

Tukumbuke kuwa bajeti zetu zinategemea fedha za wahisani, hivyo ipo pia presha kubwa kutoka kwa wahisani hao, ambao wanataka kuona Tanzania ikionyesha seriousness katika vita dhidi ya mafisadi. Haiwezekani wazungu ambao wanajibana ili kutusaidia sisi wawe na moyo wa kutuvumilia wakati wanaufahamu kwa undani ufisadi unaofanywa na viongozi wenye mamlaka makubwa serikalini.
 
kama wapinzani wanawategemea ninyi kwa mawazo yenu basi, ccm itatawala miaka 200, kwanza ninyi mmeshndwa kuusoma mchezo wa ccm wa kutoa tetes nyie mkaikosoa wakairekebisha, pili wewe allan unashindwa elewa kuwa hauna akili ya kutosha katika masuala yanayohusu tanzania, utajiita mpinzanio uongee upuuz wa namna hii?
 
Hivi ni jambo gani ambalo mashitaka yake hayawezi kusikilizwa kwenye hizi mahakama zetu zilizopo hivi sasa mpaka serikali itumie fedha kuanzisha mahakama itakayoitwa ya Mafisadi? Hiyo Mahakama itaendeshwa kwa kutumia sheria hizi hizi tulizonazo au itakuwa na sheria zake zinazojitegemea?

Mahakama hiyo ya Mafisadi ni takwa la Tawi la sheria (judiciary) au takwa la tawi la utawala (executive)? Faida yake ni ya kisiasa kwa ajili ya kuzifurahisha hisia binafsi (Adventure) za watawala au ni kwa faida ya jamii nzima ya watanzania kwa ajili ya kuliondoa tatizo la ufisadi liliota mizizi?

Waendesha mashitaka watakuwa chini ya DPP au watajitegemea, Upelelezi utafanywa na Polisi au kitaundwa chombo maalum cha kufanya kazi hiyo ya kupeleleza? Hao wasafi wa kuendesha mchakato wa Mahakama hiyo ni kina nani hasa.

Hivi mafisadi hawashtakiki kwa kuwa hawana mahakama yao na sheria zinazowabana au tatizo ni nini hasa? Tunamkubuka Sokoine kwa kupambana na Mafisadi enzi za miaka ya 80 yeye alitumia mahakama zipi na sheria zipi? Tunataka kusema kwamba mahakama na sheria zetu ni dhaifu kiasi kwamba haziwezi kuwabana mafisadi itakiwavyo?

Huu ni ufujaji wa fedha zetu usio na sababu!!
Ni wachache sana watakao kuelewa
 
Back
Top Bottom