Mahakama ya mafisadi kitanzi kwa wanyonge

Feedback

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
7,990
4,507
Kwa mwonekano wa nje hii mahakama inaonekana kama kitanzi kwa mafisadi papa, kinyume chake kitakuwa kilio kwa watu wanyonge wasio na hatia, wasio na majina, wasio na uwezo wa kuhonga majaji.

Litakuwa kaburi kwa watu walioonekana na watakaoonekana kwenda kinyume na wateule, hawa ni pamoja na walio ndani ya CCM. I bet, mbele ya mahakama hii kutakuwa na uonevu wa hali ya juu kwa wafanyabiashara kutaifishwa mali zao kwa vile tu huyu alinihujumu kwenye uchaguzi au huyu sio mwenzetu.

Uonevu kwa wanasiasa 'wa pande zote', uonevu kwa wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu kwa kisingizio cha kutoa maneno ya uchochezi.
Uonevu kwa watumishi wa umma, wakurugenzi wa mashirika kwa kisingizio cha kufisadi miradi kwa dhana ileile ya yule si mwenzetu.

Mahakama hii lazima iangaliwe kwa jicho la tatu. Mwenyewe kasema atawalinda wastaafu, kwanini basi usijiulize hii mahakama imeundwa kwa ajili ya akina nani? Na je kama itathibitika mbele ya mahakama hii mtuhumiwa alitenda kosa kwa maelekezo ya mstaafu aliyeapa kulindwa unategemea haki kutendeka?

Wait and see.
 
Mkuu,wala usijali. Mahakama ikishindwa kuwapeleka wale wakubwa ndani kwa uzembe na wzi waliofanya huku familia za watu wadogo zikiathirika. Usishangae kuokota maiti zao na watoto wa hao wakubwa katika mitaro. Wasifanye haki,haki itatendeka kwa namna nyingine.
Duh huu sasa utakua ni umafia
 
Kuna tetesi majaji wataambiwa kufunga watu harakaharaka ili ionekane ilani inatekelezwa.

Sasa ukutane na mwendesha mashtaka wa serikali na jaji Mwenye maelekezo...!!
Mbona watakoma wananchi
 
Toa maoni ya kuboresha sio kulalamika..kwa mfano ili isiwe mahakama kwa ajili ya wanyonge ungeweza kusema kuwe na kiwango fulani cha ufisadi kilichofanyika ili uhukumiwe kwenye mahakama hii kwa mfano ubadhirifu wa Richmond, Escrow, Epa n.k au tuseme ubadhirifu unaozidi kiasi cha Sh. bilioni moja na kuendelea.

INGAWA KISHERIA SIDHANI KAMA MNYONGE ANAHESABIKA KUWA NI MALAIKA NA HAWEZI KUIBA....Hata yule jamaa alipobanwa na maswali aliishia kusema mnanionea(huu ni unyonge pia)
 
Toa maoni ya kuboresha sio kulalamika..kwa mfano ili isiwe mahakama kwa ajili ya wanyonge ungeweza kusema kuwe na kiwango fulani cha ufisadi kilichofanyika ili uhukumiwe kwenye mahakama hii kwa mfano ubadhirifu wa Richmond Escrow Epa n.k

au tuseme ubadhirifu unaozidi kiasi cha sh bilioni moja na kuendelea.

INGAWA KISHERIA SIDHANI KAMA MNYONGE ANAHESABIKA KUWA NI MALAIKA NA HAWEZI KUIBA....Hata yule jamaa alipobanwa na maswali aliishia kusema mnanionea(huu ni unyonge pia)
Muda ni mwalimu mzuri sana mwezi wa saba siyo mbali, wewe tega sikio KAMA utasikia kesi za Escrow au EPA au Meremeta au Kiwira au kampuni ya mwarabu wa Loliondo au IPTL na Tanesco zinafunguliwa na wahusika wake wanafikishwa mbele ya mahakama hiyo, nijulishe.

Sana sana tutasikia mahakama ya mafisadi imemuachia huru m-Asia aliyetuhumiwa kukwepa kodi, TRA imethibitisha makontena yaliyokamatwa yalikuwa yamelipiwa kodi, ikawa jioni ikawa asubuhi ya tarehe 25/4/2020 kipindi chake kimekwisha niongezeeni miaka mingine mitano walimie ulimi sio meno tena.

Hahahaa Only in Tanzania.
 
Mkuu,wala usijali. Mahakama ikishindwa kuwapeleka wale wakubwa ndani kwa uzembe na wzi waliofanya huku familia za watu wadogo zikiathirika. Usishangae kuokota maiti zao na watoto wa hao wakubwa katika mitaro. Wasifanye haki,haki itatendeka kwa namna nyingine.

Mkuu siyo watoto wao tu , hata wao wenyewe. Maana wamezidi kuongopa.
 
Hiyo mahakama itakuja kuwafunga wenyewe wanao ipigia chapuo.
1466834403451.jpg
 
Leo hii chadema wanaipinga mahakama ya mafisadi... JPM endelea kuwabana mafisadi watajitokeza kote walipojificha kuanzia ufipa.

Orodha ya mwanzo wasipo kuwepo kina Lugumi and co, Kiwira mines, escrow, HSC, nisawa na kujilisha upepo.
 
Kiukwe Raisi alipotamka kuwalinda watangulizi wake nilijua basi tena hakua Mahakama ya Mafisadi,
Maana wahusika wa kupelekwa kule ni walewale kutoka kwenye Mitando ya hao anaowalinda,

Kwahiyo watakuwa wazi kusimamia miradi yao sii kwa kificho tena,
CCM ni ileile na matendo ni yaleyale,
Hakuna wa kupambana na Ufisadi kutokea ndani ya CCM,
 
Kwa mwonekano wa nje hii mahakama inaonekana kama kitanzi kwa mafisadi papa, kinyume chake kitakuwa kilio kwa watu wanyonge wasio na hatia, wasio na majina, wasio na uwezo wa kuhonga majaji.

Litakuwa kaburi kwa watu walioonekana na watakaoonekana kwenda kinyume na wateule, hawa ni pamoja na walio ndani ya CCM.

I bet, mbele ya mahakama hii kutakuwa na uonevu wa hali ya juu kwa wafanyabiashara kutaifishwa mali zao kwa vile tu huyu alinihujumu kwenye uchaguzi au huyu sio mwenzetu.

Uonevu kwa wanasiasa 'wa pande zote', uonevu kwa wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu kwa kisingizio cha kutoa maneno ya uchochezi.

Uonevu kwa watumishi wa umma, wakurugenzi wa mashirika kwa kisingizio cha kufisadi miradi kwa dhana ileile ya yule si mwenzetu.

Mahakama hii lazima iangaliwe kwa jicho la tatu.

Mwenyewe kasema atawalinda wastaafu, kwanini basi usijiulize hii mahakama imeundwa kwa ajili ya akina nani?

Na je kama itathibitika mbele ya mahakama hii mtuhumiwa alitenda kosa kwa maelekezo ya mstaafu aliyeapa kulindwa unategemea haki kutendeka?

Wait and see.
Sasa nyie huwa mnataka nini hasa?? Mbona machadema hamueleweki?
 
Leo hii Chadema wanaipinga mahakama ya mafisadi... JPM endelea kuwabana mafisadi watajitokeza kote walipojificha kuanzia ufipa.
Hakuna anayepinga mahakama hii bali tunatoa angalizo la dhana iliyojificha ndani.

Kama kweli unavyosema Magufuli kaanzisha mahakama hii kwa ajili ya ufisadi ulioko 'ufipa' kwa maana ya makao makuu ya Chadema,

basi either of the two is true, ama wewe akili zako haziko sawa au rais hakuwa serious kuanzisha hii mahakama.
 
Muda ni mwalimu mzuri sana mwezi wa saba siyo mbali, wewe tega sikio KAMA utasikia kesi za Escrow au EPA au Meremeta au Kiwira au kampuni ya mwarabu wa Loliondo au IPTL na Tanesco zinafunguliwa na wahusika wake wanafikishwa mbele ya mahakama hiyo, nijulishe.

Sana sana tutasikia mahakama ya mafisadi imemuachia huru m-Asia aliyetuhumiwa kukwepa kodi, TRA imethibitisha makontena yaliyokamatwa yalikuwa yamelipiwa kodi, ikawa jioni ikawa asubuhi ya tarehe 25/4/2020 kipindi chake kimekwisha niongezeeni miaka mingine mitano walimie ulimi sio meno tena.

Hahahaa Only in Tanzania.
Mara ya kwanza mlisema haitaanzishwa!!
Brother Magu sio mtu wa porojo ni kazi tu.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom