Mahakama ya Kisutu yawahukumu Mawaziri wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona kwenda jela miaka 3

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
1,656
2,250
Nimepigiwa simu kufahamishwa hilo ila sina uhakika.Nasikia wamehukumiwa kifungo cha jela miaka mitatu na faini ya million 5. Ila navyoamini itakuwa jela miaka 3 au faini ya million 5.

Kama kweli wamefungwa japo ni miaka michache ndio watakuwa kafara au arent kwa kina Chenge hata sijui. Ni vigumu kuhukumu kesi za wanasiasa bila kuangalia siasa kwa nchi changa kisiasa

Mwenye taarifa za kina atujuze.



basil-yona.jpg

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo, imewahukumu kifungo cha miaka mitatu jela aliyekuwa Waziri wa Fedha na Uchumi, Bazil Mramba na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona baada ya kuwatia hatiani kwa makosa mawili.

Akizungumzia hukumu hiyo, Wakili wa washtakiwa hao, Peter Swai, ameiambia FikraPevu kwamba hukumu hiyo imetolewa na jopo la majaji watatu ambao ni Jaji Samu Rumanyika, Jaji John Utamwa, pamoja na Hakimu Saul Kinemela, ambapo mtuhumiwa wa tatu wa kesi hiyo ambaye ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja, ambaye amekutwa hana hatia huku mawakili wa washtakiwa wakiazimia kukata rufaa.

"Hatujaridhika na hukumu ila shauri limesikilizwa na Mahakimu wa tatu. Na kwa mujibu wa sheria ytukikata rufaa aidha watakubali wote watatu au mmoja wao atakataa, kwahiyo iwapo mmoja wao atakataa na wawili wakikubaliana hiyo ndiyo hukumu ya Mahakama, na hicho ndicho Mahakama ilichofanya leo, hili ni jambo la kisheria kama tunaamini kwamba uamuzi uliotolewa hauendani na sheria tutakata rufaa kwenye Mahakama ya juu na itatafsiri sheria upya na sisi tutapata majibu" alikaririwa na FikraPevu.

Kwa mujibu wa sheria ya makosa ya jinai, kosa la matumizi mabaya ya madaraka adhabu zake ni kulipa faini ya Sh. milioni 2 au kifungo cha kati ya mwaka mmoja au miaka mitatu jela baada ya mshtakiwa kupatikana na hatia.

Katika mashtaka hayo ilidaiwa kuwa washtakiwa wakiwa watumishi wa serikali, Oktoba 10, mwaka 2003 walikaidi ushauri wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wa kuwataka wasitoe msamaha kwa Kampuni ya Alex Sterwart (Assayers) Government Business Corporation.

Novemba 25, mwaka 2008, washtakiwa hao, walifikishwa katika mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Hezron Mwankenja, na kusomewa mashitaka 13, likiwamo la matumizi mabaya ya madaraka. Kesi hiyo ilipangiwa jopo hilo na kuanza kuisikilizwa mapema mwaka 2009.

Kumbukumbu zinaonyesha kwamba katika mashitaka yaliyokuwa yanawakabili washtakiwa ni pamoja na kudaiwa kati ya Agosti mwaka 2002 na Juni 14 mwaka 2004 Jijini Dar es Salaam, washitakiwa wakiwa watumishi wa umma kama Mawaziri walitumia vibaya madaraka. Mramba na Yona wanadaiwa kuwa kati ya Juni 2003 na Mei 2005, wakiwa na nyadhifa hizo za uwaziri kwa makusudi na kutowajibika waliruhusu mkataba wa kuzuia kulipa kodi ili kuipendelea kampuni hiyo na kuisababishia serikali hasara ya Sh. 11,752,350,148.00.

Washtakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh. Bilioni 11.7 kutokana na kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya kukagua madini ya dhahabu ya Alex Stewart (ASSAYERS) ya Uingereza iliyoingia mkataba wa kudhibiti madini ambapo kwa kupitia kampuni tanzu ya Alex Stewart (ASSAYERS) Government Business Corporation waliingia mkataba na kampuni tanzu kukagua uzalishaji wa madini ya dhahabu, kinyume cha Sheria ya Manunuzi ya Umma.


========

Video ikiwaonyesha Mramba na Yona Mahakamani baada ya kuhukumiwa miaka mitatu jela:



Hisani: MillardAyo.com
 
Last edited by a moderator:
mkuu tulia ,lete habari iliyokamilika
na sio habari mfu kama hivi ulivyoleta
kama huna uhakika ni bora uweke UNCONFIRMED
ili wadau wa mambo wakuwekee sawa
 
hukumu ya kampeni hii na ni maigizo!!

Kesi imechukua 9years,2010 kwenye kampeni Kikwete alijigamba pale Jangwani kuwa kapambana na rushwa kwa kushitakiwa mawaziri Yona na Mramba,2015 kwenye kampeni series itaendelea!!

Siku za hukumu zilisogezwasogezwa,leo hukumu hiyo kwa kuitia hasara 11+ billions na matumizi mabaya ya ofisi,real??!!

Francis Cheka alihukumiwa kwa kupigana miaka mingapi??! jela kuna watu wamefungwa zaidi ya miaka minne kwa wizi wa kuku,ngombe etx
 
Hii ndio adhabu gani,tukiendelea na ujinga kama huu nakwambia wizi hautokwisha serekalini.Ningefurahi na kuipongeza mahakama kama wangelambwa miaka 20 jela,Viboko kumi wakianza kutumikia adhabu zao na viboko vingine kumi wakati wakitoka jela,wafilisiwe malizao zote na kusiwepo na fursa ya kupunguziwa adhabu.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom