Mahakama ya kimataifa ya ICC ni kwa ajili ya mataifa gani na kesi zipi?

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,490
46,011
Ni wakati gani ambapo mahakama ya kimataifa ya ICC huwa ina uwezo wa kuingilia taifa lingine na kutoa waranti za watu kukumatwa na kuwafungulia kesi?

Baadhi ya wa Kenya, Congo, Sudan n.k wamewahi kushitakiwa katika mahakama hii
Je, Mahakama hii ina nguvu na mamlaka juu ya mataifa yapi?

Kesi za aina gani huendeshwa na mahakama ya ICC?
 
ni nchi wanachama Tuu na pia kuna makosa kama nakumbuka vizuri yapo manne.. Kuna Genocide, Crimes against humanity, War crimes na Aggression.... haya ndo ICC inashughulika nayo
 
mostly genocide lakini sio watu 15 wameuliwa unafungua kesi, there is a limit sina uhakika ni limit gan
 
Ni wakati gani ambapo mahakama ya kimataifa ya ICC huwa ina uwezo wa kuingilia taifa lingine na kutoa waranti za watu kukumatwa na kuwafungulia kesi?

Baadhi ya wa Kenya, Congo, Sudan n.k wamewahi kushitakiwa katika mahakama hii
Je, Mahakama hii ina nguvu na mamlaka juu ya mataifa yapi?

Kesi za aina gani huendeshwa na mahakama ya ICC?
Icc no kwa ajili ya third world country only.
 
Wakati inatoa waranti ya kukamatwa Omar Al Bashiri Sudan haikuwa mwanachama.
Wakati mwingine hupelekewa kesi na UN Security Council...si lazima uwe Mwanachama... ndio maana unawaona hawa diplomats wanaenda sana huko kwenye kesi ya mbowe... ni kwenda kukusanya taarifa tu ili baadae wafanye kweli hata kama ni kwa style ya Makonda Bashite ..
 
Kuna nchi ambazo zimetia sahihi makubaliano ya Rome statue na ambazo hazijatia sahihi makubaliano hayo. Nchi ambazo zimekubali makubaliano haya moja kwa moja ni members wa ICC. Unaweza kufikiria kwamba nchi nyingi za Afrika zinaonewa kwa kuwa members wa ICC lakini utagundua kwamba mahakama hii haisikilizi kesi zozote tu. ICC inasikiliza kesi za watu ambao hawawezi kutiwa nguvuni na vyombo vya usalama nchini kwao kwasababu ya umaarufu wao, nguvu waliyo nayo na influence yao kwenye kuamua matokeo ya kesi na haki kutolewa. Mfano mkubwa ni hapa Tanzania ambapo rais yeyote yule ana kinga. Aki husika na shutuma zozote zinazo husu yeye kuminya haki za binadamu au kuvunja amani, hawezi kupata fair trial au kuhukumiwa nchini Tanzania. Hapo ndio ICC wanapo ingilia kati
 
Ni wakati gani ambapo mahakama ya kimataifa ya ICC huwa ina uwezo wa kuingilia taifa lingine na kutoa waranti za watu kukumatwa na kuwafungulia kesi?

Baadhi ya wa Kenya, Congo, Sudan n.k wamewahi kushitakiwa katika mahakama hii
Je, Mahakama hii ina nguvu na mamlaka juu ya mataifa yapi?

Kesi za aina gani huendeshwa na mahakama ya ICC?
Ndugu!
Kuna haki za Binadamu na haki za waafrika, halafu kuna haki za bongoland.
Bongoland haki hizo za Binadamu hakuna. Ndiyo maana ukifanya fyoko utaambiwa nenda Burundi!
 
Wakati mwingine hupelekewa kesi na UN Security Council...si lazima uwe Mwanachama... ndio maana unawaona hawa diplomats wanaenda sana huko kwenye kesi ya mbowe... ni kwenda kukusanya taarifa tu ili baadae wafanye kweli hata kama ni kwa style ya Makonda Bashite ..
Natamani nisikie leo Siro na genge lake wako ICC
 
ni nchi wanachama Tuu na pia kuna makosa kama nakumbuka vizuri yapo manne.. Kuna Genocide, Crimes against humanity, War crimes na Aggression.... haya ndo ICC inashughulika nayo
Sio kwa nchi wanachama tu, hata Sudan sio mwanachama lakini kwa idhini ya baraza kuu la usalama la umoja wa mataifa ikiidhinisha basi mtu yeyote anaweza akashtakiwa kwa yale makosa manne yaliyo chini ya mamlaka yake.
 
Back
Top Bottom