Mahakama ya Katiba ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza kuwa haina uwezo wa kumhukumu aliyekuwa Waziri Mkuu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Mahakama ya juu zaidi nchini DRC imeamua Jumatatu (Novemba 15) kwamba haina uwezo wa kumhukumu aliyekuwa waziri mkuu Seneta Augustin Matata Ponyo. Seneta mteule wa bunge la sasa, Augustin Matata Ponyo anashutumiwa kwa ubadhirifu wa mamia ya mamilioni ya dola zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa bustani ya kilimo ya Bukanga-Lonzo.

Katika kesi hiyo, watu wengine wawili pia wanashitakiwa: Patrice Kitebi, Waziri wa zamani wa Fedha, na Kristo Groblert, meneja wa kampuni ya Africom ya Afrika Kusini.

Wiki moja iliyopita, upande wa utetezi wa Matata Ponyo ulionyesha kwa jinsi gani Mahakama ya Kikatiba haina uwezo wa kumhukumu.

Kinachobaki sasa ni upande wa serikali kufahamu itafanya nini na inakusudia vipi kupata suluhu na ni mahakama gani itakayopewa mamlaka ya kuwahukumu washtakiwa.
 
Back
Top Bottom