Mahakama ya Kadhi yawakoroga Waislamu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahakama ya Kadhi yawakoroga Waislamu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Babuyao, Sep 22, 2009.

 1. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  • Shura ya Maimamu yapinga serikali kujitoa

  SUALA la uanzishaji wa Mahakama ya Kadhi bila kuishirikisha serikali limewasha moto upya na sasa limeonekana kuwavuruga waumini wa dini hiyo, kutokana na kauli tofauti zinazotolewa na viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu nchini (BAKWATA) na viongozi wa taasisi nyingine za dini hiyo.

  Mwenendo wa mihadhara iliyofanyika katika misikiti mbalimbali baada ya swala ya Idd el Fitr juzi, imeonyesha dhahiri kwamba kumekuwa na mawazo na msimamo tofauti miongoni mwa Waislamu nchini juu ya suala la muundo wa uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi.

  Wakati BAKWATA ikiwa imetoa taarifa juzi mbele ya Rais Jakaya Kikwete kwamba mchakato wa kuanzisha mahakama hiyo umeshaanza na upo kwenye kasi nzuri, baadhi ya Waislamu katika misikiti mbalimbali wamepinga hatua hiyo kwa sababu ya kile wanachokielezea kuwa haitakuwa na nguvu ya kufanya kazi, kwani tayari serikali iliyopaswa kuianzisha na kuipa nguvu kisheria imeshatangaza kujitoa.

  Katika swala ya sikukuu ya Idd juzi iliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi mmoja Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa BAKWATA, Sheikh Suleiman Said Lolila, alisema mchakato wa kuanzishwa kwa mahakama hiyo unakwenda vizuri na kuwataka Waislamu kuvuta subira.

  Alisema mchakato huo, unawashashirikisha masheikh, na wanasharia wa dini hiyo yenye wafuasi wengi nchini.

  Hata hivyo, katika mhadhara kama huo uliofanyika kwenye baadhi ya misikiti jijini Dar es Salaam jana, watoa mada walisikika wakipinga vikali hatua ya serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kukwepa kile walichokiita ahadi yake ya kuanzisha Mahakama ya Kadhi na kuwataka Waislamu wajianzishie wenyewe, huku wakijua fika kuwa ikianzishwa kwa muundo huo, haitakuwa na nguvu ya kufanya kazi.

  “Wapendwa Waislamu, tumekuwa tukifanywa daraja la kuwavusha watu kuingia madarakani kwa kutupa ahadi mbalimbali. Serikali hii katika ilani yake ya uchaguzi mwaka 2005, iliahidi kutuanzishia Mahakama ya Kadhi, leo serikali ile ile inajitoa inasema Waislamu tuanzishe wenyewe.

  “Hatuwezi kuanzisha mahakama wenyewe bila mahakama hiyo kuwa na nafasi katika mfumo wa kiserikali, vinginevyo mahakama hiyo haitakuwa na nguvu, haitakuwa na meno kama ile iliyovunjwa.

  “Wanasiasa wengi serikalini ambao hawautakii mema Uislamu, ndio wameshashinikiza msimamo huo wa serikali, wakijua fika kuwa haiwezekani kwa Mahakama ya Kadhi kuanzishwa nje ya taratibu za kiserikali, halafu kadhi huyo akafanya kazi zake sawasawa.

  “Haitawezekana kwa sababu bado mahakama za kidunia zitakuwa na nguvu kubwa kuliko kadhi, zenyewe zina nguvu katika sheria. Leo mtu akikamatwa anashitakiwa katika mahakama hizi kwa kuwa sheria ya nchi inasema hivyo, sasa Waislamu hatuwezi tukaanzisha Mahakama ya Kadhi wenyewe bila kupewa nafasi katika sheria za nchi, halafu mahakama ikafanya kazi, haitawezekana, itapuuzwa badala ya kupewa hadhi yake vile inavyostahili.

  “Kadhi ni haki yetu, tusikubali kurubuniwa eti tuanzishe wenyewe, tupiganie haki hii hadi iilazimu serikali kuianzisha,” alisema sheikh mmoja aliyekuwa akitoa mhadhara katika swala ya Sikukuu ya Idd kwenye msikiti mmoja wa maeneo ya Tandale, huku waumini wakimuunga mkono kwa kuitikia ‘Takibir’, kila alipomaliza kusoma aya moja.

  Mbali ya mhadhara huo ambao Tanzania Daima iliushuhudia, uongozi wa Shura ya Maimamu umepinga hotuba ya mgeni rasmi katika Baraza la Idd jana, Dk. Ali Mohammed Shein, kwamba hotuba yake ni ya kisiasa mno na haielekei kutafuta ufumbuzi wa tatizo la Mahakama ya Kadhi.

  Pia Shura ya Maimamu, wamepinga hatua ya BAKWATA kukiuka makubaliano ya pamoja waliyowekeana na kuunga mkono mpango wa serikali wa kutaka ianzishwe Mahakama ya Kadhi isiyoihusisha serikali.

  Akizungumza na Tanzania Daima, jana Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu, na Katibu wa kamati ya kuokoa mali za Waislamu, Sheikh Issa Ponda, alisema kauli hiyo ni ya kisiasa na mahakama inayoelezwa na serikali kuwa inaletwa si inayotakiwa.

  “Kauli ya Makamu wa Rais ni ya kisiasa, hatuiungi mkono, kwa sababu, Mahakama ya Kadhi wanayotaka kuirejesha si ile ambayo Waislamu wanaitaka. Tunaitaka ile iliyofutwa, iliyokuwa ikisimamiwa na serikali,” alisema Sheikh Ponda.

  Alisema kauli ya serikali kuhusu Mahakama ya Kadhi ni ya kisiasa, inayoonyesha kutaka kuwapoza Waislamu na imeonyesha wazi kuwa serikali hailitaki jambo hilo.

  “Bado msimamo wetu ni kuipinga mahakama hiyo wanayotaka kuirejesha, huo ni mpango wao na BAKWATA kutaka kuturubuni Waislamu,” aliongeza Sheikh Ponda.

  Akizungumzia kuhusu kupunguzwa kwa idadi ya wajumbe 25, waliokuwa wakiwakilisha Waislamu katika mazungumzo hayo ya uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi na serikali, hadi wajumbe watano, alisema huo ulikuwa ni ujanja wa BAKWATA na serikali kutaka kuwapunguza nguvu ya mjadala huo.

  “Wamepunguza idadi kutoka wajumbe 25 wa awali hadi watano, hii ilikuwa ni kutuzunguka, kwani wale watu wa msingi, wote waliondolewa na hakuna sababu za msingi zilizotolewa,” alisema.

  Naye Amiri wa Shura ya Maimamu, Sheikh Mussa Kundecha, alisema chombo hicho kamwe hakitaisujudia BAKWATA, katika kufanya maamuzi yenye tija kwa Waislamu.

  Sheikh Kundecha, aliilaumu BAKWATA kwa kupuuza makubaliano yao juu ya suala la Mahakama ya Kadhi, ikiwa ni pamoja na kukubali idadi ya wajumbe kupunguzwa.

  Alieleza kuwa baada ya kuteuliwa, viongozi hao ambao walikuwa wakitoka katika jumuiya na taasisi mbalimbali za Kiislamu, walikubaliana kutofanya maamuzi yoyote hadi viongozi hao wakubaliane kwa pamoja, lakini kwa makusdi BAKWATA imekiuka makubaliano hayo.

  “Nataka kuwapa taarifa, kuna mambo mawili yamefanywa na BAKWATA, kinyume na makubaliano yetu, BAKWATA wasifikirie kuwa tunaweza kuchezewa na hili,” alisema Sheikh Kundecha.

  Aliongeza kuwa kitu kilichowashangaza ni uamuzi wa BAKWATA kuteua watu watano kati yao na kudai kuwa wao ndio wawakilishi katika mazungumzo na serikali bila kushirikisha viongozi wote 25.

  Wiki iliyopita serikali iliitaka BAKWATA kupunguza idadi ya wawakilishi wao katika mazunguzo hayo kutoka 25 hadi watano na tayari walishakutana Jumatatu ya wiki iliyopita na kuanza mazungumzo.

  Mazungumzo ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi yanafanyika kati ya viongozi wa BAKWATA na serikali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, ambapo serikali ilikwisha kutangaza kuwa mahakama hiyo itaundwa lakini isiihusishe serikali.

  Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), nayo ilitoa msimamo wa kutaka mahakama hiyo ianzishwe bila kuishirikisha serikali, kwani kufanya hivyo kunaweza kuibua hasira kutoka kwa madhehebu mengine.

  Chanzo: TANZANIA DAIMA
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Sep 22, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hawa waislamu kwa kulalamika kama watoto wadogo ndio jadi yao! Serikali imeshawapa go ahead lakini wanataka watafuniwe kila kitu huku wakijua kwamba Mahakama za Kadhi ni ibada ya Waislamu tu na wengine haziwahusu! Wanafikiri kwa sababu JK ni mwislamu basi serikali nayo ni ya kiislamu! Wakae misikitini wafanye mambo yao hakuna atakayewaingilia!
   
 3. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Tatizo BAKWATA si chombo cha waislamu huko Tanzania. Ni Chombo cha Serikali ya Tanganyika kilichoundwa na JKN kwa maslahi ya serikali ili kuwadhibiti waislamu. Sasa waislamu wanataka vyombo huru na sio Bakwata.

  Nachelea kujiuliza Kwanini Serikali ya Tanganyika inakumbatia BAKWATA? kunani?
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Sep 23, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Unaposema chombo cha serikali unamaanisha katiba ya BAKWATA imetungwa na serikali au vipi ndugu yangu tufahamishe maana madai haya nimeyasikia mara kwa mara! Na kama BAKWATA ni ya serikali mbona wanataka Mahakama ya Kadhi nayo iwe chini ya Serikali hiyo hiyo badala ya kuwa huru? Si wataanza tena kulalamikia kitu hichohicho kwamba hawako huru (Mahakama ya Kadhi) na mnaingiliwa na Serikali?
   
 5. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #5
  Sep 23, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  weeeee ukimwacha muislamu huru hachelewi kujilipua kwake maisha si kitu cha thamani bora afe ndo thamani na thwabu kweke,bravo tz govt kama kweli BAKWATA ni kwa ajili hiyo.hatutaki kina Kaduna,Muktada al kadri, bokoharam katika tanzania yetu,na mipango itafanywa tu wawe down unless waislamu nao wajue umuhimu wa elimu na kuwa wastaarabu.nilitarajia wadai vyuo na vifaa vya elimu kwa kasi kubwa but eti mahakama,ili kumhukumu nanai?au wahalifu wengi sana,kwa muslims?
   
 6. P

  Preacher JF-Expert Member

  #6
  Sep 23, 2009
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  serikali ilikwisha kutangaza kuwa mahakama hiyo itaundwa lakini isiihusishe serikali

  1. Nihabarisheni - kutakuwa na magereza pia? au wahalifu/wakosaji watakaonekana wana hatia watapewa adhabu za kidini au hata kufungwa?

  2. Wakosaji wa-kiislamu watakaposhitakiwa, wataenda kukamatwa na nani - police waliojiriwa na serikali au mahakama hiyo inaajiri pia police wao?

  3. Mahakama hiyo itatumia sheria za Dini ya Kiislamu kuadhibu wakosaji - kama Mwislamu ataona hakutendewa haki - je - kuna mahakama ya kadhi ya rufaa - maybe toka nchi nyingine au??

  Naomba anayejua anieleze zaidi kwani sielewi vizuri -ili nipate ufahamu kwani nina ndugu zangu na marafiki Waislamu -nijuie yatakayowasibu mahakama hiyo ikianzishwa/na pia just to broaden my knowledge in this issue - asanteni.
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Sep 23, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Ukitaka kusomea digrii ya kuwaelewa Waislamu hutaipata hiyo digrii maana hutawaelewa! Leo watasema hapana, kesho watasema ndio kwa jambo lilelile!
   
 8. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #8
  Sep 23, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Mahakama ya Kadhi itahusu ndoa, talaka na mirathi. Katika mambo haya matatu sina hakika kama mahabusu zinahitajika. Sina hakika vilevile kama ile adhabu ya kupiga wazinzi mawe itafanya kazi kwenye mambo ya ndoa au la kwa kuwa serikali ilishawaambia kwamba Mahakama ya Kadhi isijihusishe na mambo ya Jinai na madai!
   
 9. K

  K4jolly JF-Expert Member

  #9
  Sep 23, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 366
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JKN unamaanisha Nyerere?? sasa kama BAKWATA ilianzishwa na JKN mbona alikuja Rais Mwinyi tena Muislam kwanini asibadilishe? akaja Mkapa? akaja JK kwanini hawa wote wasibadilishe hiki chombo??

  Mimi nadhani nyie wenyewe kwa wenyewe ndo kuna tatizo! jipangeni mkae wote mtoe msimamo mmoja. Lakini leo Bakwata, kesho shura ya maimamu, keshokutwa wale wanaotetea mali za waislam? kweli hapo utapata jibu la kueleweka?

  Pia nyie wenyewe mnamdharau Mkuu wenu Shehe Mkuu, kitu ambacho ni kibaya zaidi na haipendezi.
   
 10. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #10
  Sep 23, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Muda si mrefu wataomba kuwe na Mahakama ya Kadhi ya BAKWATA na pia Mahakama ya Kadhi ya Shura ya Maimamu!
   
Loading...