Mahakama ya Kadhi: Masheikh wakutana na JK

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
PRESIDENT'S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, usiku wa jana, Jumatatu, Septemba 5, 2011, amekutana na kufanya mazungumzo na Masheikh wa Dini ya Kiislam kuhusu mchakato wa kuundwa kwa Mahakama ya Kadhi nchini.

Katika mkutano huo, pande hizo mbili zimezungumzia kwa undani hali ya majadiliano ya suala zima la kuanzishwa kwa Mahakama hiyo ya Kadhi.

Mheshimiwa Rais na Masheikh wamekubaliana kuwa Kamati ya Pamoja ya Serikali na Masheikh ikutane mapema iwezekanavyo na iongeze kasi ya majadiliano ili shughuli hiyo iweze kumalizika mapema iwezekanavyo.

(Habari hii imeambatana na picha ya Mheshimiwa Rais na Masheikh katika kikao hicho cha jana lkn nipo via mobile siwezi kuiweka).

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

06 Septemba, 2011
 
hakuna jipya,ni ngonjera zilezile,labda useme kama this time serikali imekubali kui fund mahakama ya kadhi
 
Baada ya mahakama ya kadhi kushindikana, sasa wanataka kuomba Tanzania ijiunge na OIC. Hizo ni hatua muhimu za kujenga taifa la wazee wa ubw....
 
wanajadiliana nini? Si alishawaambia kwamba waanzishe mahakama yao wenyewe?
Na hiyo kamati itagharamiwa na nani?
 
serikali ianzishe hiyo mahakama watu wakatwe mikono bana.. Uhalifu mwingi utapungua aisee...kwa nn wakristo hawaitaki hii mahakama? Hii ni pilipili isiyoila sasa inawawashia nini?
 
Wakristu wanataka mahakama ya kadhi iwepo <b>ila tu</b> iendeshwe na waislam wenyewe. kuna tatizo hapo mkuu wangu?
tatizo lipo tena kubwa..kwani hiyo pesa ya serikali wakristo ndio wanachangia hio kodi wenyewe? This is distribution of nation cake....tatizo liko wapo? Kwani mahakimu wa hio mahakama watatoka uarabuni? Nope ..watakuwa ni watanzania wenzetu tena....kuna tatizo hapo?....au hujawahi kwenda kwenye migodi ya madini na makampuni makubwa ukaona jinsi wageni wanavyotumbua pesa yetu kwa kupewa mishahara mikubwa?
 
Mkuu wangu ....uamuzi mbona umeshatolewa! Mtaiendesha mahakama ya kadhi kwa hela zenu wenyewe. hakuna jinsi!
 
wakristo kuipinga mahakama ya kadhi ni kueneza udini...
kama tumepinga mbona kikwete amekaa na mashehe na wamekubaliana kuunda kamati haraka ili kufanikisha mahakama ya kadhi? au wanataka kuunda mahakama ya kitu gani?? kaka , mbona mna tabia ya kulalamika sana? mimi sijawahi kuona watu wanadai kitu halafu wakipewa wanaanza tena kulalamika. Ninyi ni watu wa aina ya pekee kabisa hapa duniani.
 
tatizo lipo tena kubwa..kwani hiyo pesa ya serikali wakristo ndio wanachangia hio kodi wenyewe? This is distribution of nation cake....tatizo liko wapo? Kwani mahakimu wa hio mahakama watatoka uarabuni? Nope ..watakuwa ni watanzania wenzetu tena....kuna tatizo hapo?....au hujawahi kwenda kwenye migodi ya madini na makampuni makubwa ukaona jinsi wageni wanavyotumbua pesa yetu kwa kupewa mishahara mikubwa?
ahaa! Hapo mkuu umeteleza. Serikali haina dini na tena serikali siyo charity organization. Tuiache ifanye mambo yake tusiipe majukumu ambayo siyo yake. Tuiache itupe miundo mbinu na mambo ya namna hiyo
 
kama haina dini kwa nini -Katoliki wanapewa fungu na serikali? Kwa nini kama wanatoa huduma za jamii wasitoe tu kama kanisa? Kwa nini wameingia gentlemen mkataba na serikali ambayo haina dini? Serikali na maaskofu hapa wameteleza kuwanyima waislamu mahakama ya kadhi kama walivyotaka na huu udini wakristo ndio wanauanzisha wenyewe
 
Mkubwa... Sorry if I'll be offending you... But I think and believe the opposite is true... Kutumia pesa za Serikali kuanzisha na kuendesha Taasisi za kidini ndiyo UDINI!!!
unajua kuwa serikali inalipa kanisa fungu kila mwaka? Huu sio udini?
Wake up!!! Hapa serikali imeteleza sana isifikiri kuwa waislamu ni wajinga
 
kama haina dini kwa nini -Katoliki wanapewa fungu na serikali? Kwa nini kama wanatoa huduma za jamii wasitoe tu kama kanisa? Kwa nini wameingia gentlemen mkataba na serikali ambayo haina dini? Serikali na maaskofu hapa wameteleza kuwanyima waislamu mahakama ya kadhi kama walivyotaka na huu udini wakristo ndio wanauanzisha wenyewe

Mkubwa hiyo "genlement mikataba" inahusu nini?? Je inahusu kuimarisha utekelezaji wa sheria na taratibu za kikristo au??
 
wakristo kuipinga mahakama ya kadhi ni kueneza udini...
Hivi wewe wakristo wanakunyima usingizi? Jitahidi uwabadilishe wawe waislam. Ukishindwa ungana nao.

Madhehebu gani ya kiislam yatakayoendesha mahakama hiyo. Bakwata mwaikataa!!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom