Mahakama ya Kadhi Inaweza Kuwa Kiini Macho Tu

tototundu

Senior Member
Jul 29, 2009
198
40
Mimi sio mshabiki wa siasa asilani, na sijawahi kuwa na muumini mkubwa wa dini (sayansi iliniathiri toka niko mdogo), lakini Ma- great Thinkers mmenisikitisha kwa jinsi mnavyoshabikia hotuba ya Mheshimiwa Rais kwenye Baraza la Idd, na ambavyo mnashindwa kuona jinsi gani mmekuwa twisted kidogo tu, woote mmezolewa.

Mmesahau kuwa mwanzo wa ngoma ni lele, na haba na haba hujaza kibaba. Baada ya kubishana sana na wanaotaka kuanzisha mahakama ya kadhi na nyinyi kuwashinda, wenzenu wamekaa chini na kufikiria njia mpya ya jinsi ya kujipenyeza. Kosa lao ilikuwa na kujaribu kuanzia juu sana, ambako nyinyi nyote mlishtuka. Ni sawa na kwenda kjijini na kutaka kupewa hekari mia za msitu, wanakijiji lazima wakupige mawe. Lakini ukienda leo ukaomba hekari moja kesho ukaomba ya pili, mwezi ujao ukawa na kumi, hawatashtuka mpaka wanajikuta wamekupa ekari mia bila wao kujua.

Na hawataweza kukunyang'anya tena kwa kuwa utakua umezipata kihalali. Wakitaka kukunyang'anya kwa nguvu bila shaka utaanzisha vita, na ukizingatia ukiwa na hekari mia utakuwa na vibarua wengi, vita na kijiji haitakuwa ndogo.

Hivyo hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa mahakama ya kadhi. Itaanza kwa kuruhusiwa na kuendeshwa kwa gharama zao wenyewe. Halafu zitaanza kuwa common, ghafla atatokea mfadhili kutoka Iran au Saudia atazipa fedha za kutosha kujiendesha kwa miaka mitano. Mara kila wilaya itakuwa na mahakama ya kadhi. Hakafu kila mkoa, baadae tutapata kadhi mkuu wa taifa.

Pengine kusiwe na tatizo la setup nzima, ila ni ukweli ulio wazi kuwa bandu banduhumaliza..... Tutaanza na kesi za mirathi, ndoa na talaka. Kidogo kidogo, tutaanza kuingiza na kesi za kuiba kuku, simu, mitumba na zaidi. Kama livyo tamaa, unapozidi kupata kikubwa ndio unazidi kutamani kikubwa zaidi.

Nawasihi watanzania wenzangu, dini na siasa na utawala, si vitu vya kuchanganya hata kidogo. Huwezi kuwa na nchi moja yenye kufuata sheria mbili zinazopingana. Kutakuwa na ugomvi tu.
Mfano, mtu amekamatwa ugoni, kwa sheria za nchi zilizopo sasa, aliyefumaniwa atalipa faini. Kwa sheria za biblia na za kiislamu, mwanamke katika fumanizi hilo (bila kujali nani mwenye kosa), anatakiwa apigwe mawe mpaka afe. Lazima kutakuwa na conflict of interests. Mtajipa moyo kwamba mtaweka mipaka kwa kila sheria, lakini in practice ni huwa haiwezekani. Jambo la namna hii limeleta migogoro mikubwa sana sehemu nyingi hasa hasa Nigeria.

Ingefaa dini ingebaki kwenye imani ya mtu binafsii tu. Iwe kati ya Mungu na mja wake. Kuchanganya dini na siasa na utawala ni suicidal. Mfano hai ni nchi kama Nigeria, sijawahi kuona logic ya watu kuuwana kisa dini. Huwa nahuzunika sana nionapo mauaji ya kidini popote pale hasa hasa Afrika.

Tanzania bado tuna nafasi ya kuzuia majanga kama haya yasitokee huko mbeleni. Ingawa mimi niko kisayansi zaidi, lakini na mimi nina dini yangu niliyokulia nayo. Pamoja na hayo, MIMI NAAMINI KUWA MIMI NI MTANZANIA/MWAFRIKA KWANZA HALAFU NI MWISLAMU/MKRISTO BAADAE. Major reason ni kuwa naweza kubadili dini nitakavyo (ukoo wetu una ndugu wengi wa dini zote, hawajahi kukosana sababu ya dini), lakini siwezi kubadili asili yangu ya uafrika baada ya kuzaliwa.

Nimewahi kwenda UK nikabaguliwa kwa rangi yangu, nimewahi kwenda Saudi nikabaguliwa kwa rangi yangu pia. Nimetembea sehemu nyingi Tanzania sijawahi kushangaliwa (sijui kama ni Kiswahili sahihi) kama ambavyo watu wa nje, wazungu kwa waarabu wanavyoshangaliwa wakienda hasa vijijini.

Ningeshauri sana vijana wa sasa, ambao ndio walio wengi kwa sasa hapa nchini, wafundishwe utaifa, taifa mbele kabla ya kitu kingine chochote. Watu wengi walio maskini ndio huwa wanakuwa waathirika wakubwa wa machafuko ya aina yoyote; viongozi (siasa/dini) na familia zao huwa wanakimbilia safe heaven wakiwaacha nyinyi mtaabike.

Na ni vizuri tiukasambaza elimu ya kufikiria kwa "BIG PICTURE" kwa watu wote Tanzania. Ushahidi upo, waafrika ni wastaarabu sana, waarabu wa Saudia, Dubai au Iran, au wazungu wa kawaida wa Ulaya na Marekani, huwa hawana muda au nia mbaya na watu wa Afrika.

Choko choko zote huku kwetu Afrika hazijawahi kuanzishwa na Waafrika wenyewe (as original source). Choko choko zote huanza mahali pale panapojulikana kuna mali, hasa hasa madini na mafuta. Kwa hili mifano iko mingi tu, Angola vita vimepiganwa wee, wazungu wamefaidika, waafrika wameachwa vilema na masikini, Afrika Kusini wamepewa uhuru baada tu ya kuhakikisha Urusi imeanguka, haitafaidika tena madini yaliyopo kule. Congo DRC kuna vita mpaka leo isiyo na mwisho wala sababu kwa sababu tu kuna mali zilizopo pale.
Angalia sasa, huko kote hakuna dini zilizojikita na zenye nguvu, hakuna udini, lakini vita haiishi.

Si watu wengi wanajua kuwa Nigeria ni moja ya nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi sana duniani, lakini wananchi wa kawaida WAISLAMU KWA WAKRISTO hakuna wanachofaidika na hayo mafuta. Wametiwa ujinga wa kugombanishwa kwa udini, akili zao zimeharibiwa hawafikirii kwa mantiki.
Tusifike huko. Tuwarithishe vijana na watoto wetu ukweli huu.
Libya ni mfano wa karibuni sin haja ya kuusemea.

Nasema tena, na kwa ushahidi kabisa, hakuna vita ya kidini popote ambapo sio Uarabuni halafu waarabu au waislamu/wakristo wakawa ni chanzo. Chanzo cha choko choko zote za kidini hasa hasa Afrika ni CIA. Fikiria Osama alipotokea. Hivyo ndio dunia inavyoendeshwa.

Yote haya tunayoyaona malumbano ya kidini yamepandikizwa kwa sababu tumeaanza kuachia madini yetu pamoja na kugunduliwa mafuta huku Tanzania. Naweza kuwa siko sahiki, lakini nahisi kuna mkono wa CIA. Rekodini maneno yangu. Ikishathibitka kuwa mafuta yapo Tanzania, wakati sisi tutakapokuwa tunapigana kwa tofauti ya dini zetu, wamarekani watakuwa wanajichimbia mafuta pwani yetu kiulaiiini kama Iraq, tena watakuwa wanatupiga mabomu mara kwa mara tukilala sana, watuchonganishe.

Watanzania wenzangu, THINK IN THE BIGGER PICTURE, AND OUTSIDE THE BOX.

Ni hayo tu.
 
Mkuu tototundu umeongea ukweli wote,nataman watu wote wangepokea ushauri huu na kuuelewa.
 
Ni mawazo mazuri

Ila cha msingi ni ndugu zetu waislam wasahau kwamba hili taifa niletu wote, wenye dini na wasiokuwa na dini, mambo yao ya dini ni vema wakayaendesha kwa mujibu wa taratibu zao bila kuwabebesha mzingo watu wengine. Nikiwa kama mlipa kodi sio haki hata kidogo kodi yangu iende kulipa watakao kuwa wanafanya kazi kwenye hizo mahakama za kadhi, Ni vema wajipange wenyewe wazianzishe hizo mahakama na kuziendesha kwa garama zawatakaokuwa wanafaidika nazo

Ni vema wakajifunza wakatoliki wanazo mahakama zao, zinazoshughulikia mamabo yao ya dini, hawajawahi omba serekali kuwasaidia kuziendesha ni vema wakajifunza kwao wanaziendeshaje, itawasaidia kuwapa mwanga zaidi

Na ni vema kwenye mafundisho yao wakawa wanahubiri umoja na mshikaman wa taifa badala ya kila siku kuhubiri chuki na udini. Haya maswala ya udini wasipokemewa naamini soon tutakuwa mahali ambapo ni pabaya saana

Ndugu zetu waislam kumbukeni jamii ya kitanzania kwa sasa imechanganyika mno, wapo wengi wasio waislam wameoa waislam halikadhalika wapo waislam safi kabisa wameoa wasio waislam na wanaishi kwa amani na upendo

Ni vema tukaweka maslahi ya taifa kwanza
 
Ahsantre baba Mchungaji umeandika kuhusu usiloijua lakini hayo ni maoni na mtazamo wako una uhuru. Nigeria wamegawana nchi, Sudani kusini wamejitenga kwa msimamo wako Tanzania hatuko mbali na mfumo wetu ambao sijui utakuwaje
 
mbona wakatoliki wana ubalozi wa vatican hapa na unaendeshwa kwa kodi zetu
 
Nashangaa sana ninyi wenzetu mnapo tusemea dini yetu.....

sisi wenyewe waislam hatutaki mirathi.. na ndoa zitatuliwe na sheria ambazo ambazo hazipo katika dini yetu!.. ndoa iliyofungwa kiislam iweje mirathi.. talaka na matatizo yaliyomo ndani ya ndoa yatatuliwe na mahakama za kawaida...?!!!!

kenya ni miaka KENDA WANA MAHAKAMA ZA KADHI na si hivyo mnavyofikiria ninyi!... mahaka hizi zina deal na ndoa na mirathi tu kama muheshimiwa Rais alivyoweka wazi...!!

bahati nzuri Rais ameona mbali ameliweka hili jambo kwa waislam wenyewe.... now ninyi wa dini nyingine (Wakristo) back Off .. hakuta kuwa na hata na sumni ya kodi zenu itatumika.... waislamu tunapata tabu sana mirathi na matatizo ndani ya ndoa yanapotatuliwa na mjumbe wa nyumba 10


 
Kadhi ni ubinafsi wa hawa ndugu zetu.

I'm signing out!

hatuna udugu na weye ...muislam ndugu yake ni muslam TU ... ubinafsi mnao ninyi mnaolazimisha hukumu za ndoa zitolewe mahakama za kawaida wakati sisi tuna sheria zetu wenyewe.. hamkukatazwa na nyinyi kufanya hivo
 
selfishness is the only theme ya hao watu...na ndo ilipopelekea nchi nyingi kua na machafuko yaan hawaoni shida kufanya machafuko ilimradi tuu watimize watakayo..pole nawapa
 
mimi sio mshabiki wa siasa asilani, na sijawahi kuwa na muumini mkubwa wa dini (sayansi iliniathiri toka niko mdogo), lakini ma- great thinkers mmenisikitisha kwa jinsi mnavyoshabikia hotuba ya mheshimiwa rais kwenye baraza la idd, na ambavyo mnashindwa kuona jinsi gani mmekuwa twisted kidogo tu, woote mmezolewa.

Mmesahau kuwa mwanzo wa ngoma ni lele, na haba na haba hujaza kibaba. Baada ya kubishana sana na wanaotaka kuanzisha mahakama ya kadhi na nyinyi kuwashinda, wenzenu wamekaa chini na kufikiria njia mpya ya jinsi ya kujipenyeza. Kosa lao ilikuwa na kujaribu kuanzia juu sana, ambako nyinyi nyote mlishtuka. Ni sawa na kwenda kjijini na kutaka kupewa hekari mia za msitu, wanakijiji lazima wakupige mawe. Lakini ukienda leo ukaomba hekari moja kesho ukaomba ya pili, mwezi ujao ukawa na kumi, hawatashtuka mpaka wanajikuta wamekupa ekari mia bila wao kujua.

Na hawataweza kukunyang'anya tena kwa kuwa utakua umezipata kihalali. Wakitaka kukunyang'anya kwa nguvu bila shaka utaanzisha vita, na ukizingatia ukiwa na hekari mia utakuwa na vibarua wengi, vita na kijiji haitakuwa ndogo.

Hivyo hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa mahakama ya kadhi. Itaanza kwa kuruhusiwa na kuendeshwa kwa gharama zao wenyewe. Halafu zitaanza kuwa common, ghafla atatokea mfadhili kutoka iran au saudia atazipa fedha za kutosha kujiendesha kwa miaka mitano. Mara kila wilaya itakuwa na mahakama ya kadhi. Hakafu kila mkoa, baadae tutapata kadhi mkuu wa taifa.

Pengine kusiwe na tatizo la setup nzima, ila ni ukweli ulio wazi kuwa bandu banduhumaliza..... Tutaanza na kesi za mirathi, ndoa na talaka. Kidogo kidogo, tutaanza kuingiza na kesi za kuiba kuku, simu, mitumba na zaidi. Kama livyo tamaa, unapozidi kupata kikubwa ndio unazidi kutamani kikubwa zaidi.

Nawasihi watanzania wenzangu, dini na siasa na utawala, si vitu vya kuchanganya hata kidogo. Huwezi kuwa na nchi moja yenye kufuata sheria mbili zinazopingana. Kutakuwa na ugomvi tu.
Mfano, mtu amekamatwa ugoni, kwa sheria za nchi zilizopo sasa, aliyefumaniwa atalipa faini. Kwa sheria za biblia na za kiislamu, mwanamke katika fumanizi hilo (bila kujali nani mwenye kosa), anatakiwa apigwe mawe mpaka afe. Lazima kutakuwa na conflict of interests. Mtajipa moyo kwamba mtaweka mipaka kwa kila sheria, lakini in practice ni huwa haiwezekani. Jambo la namna hii limeleta migogoro mikubwa sana sehemu nyingi hasa hasa nigeria.

Ingefaa dini ingebaki kwenye imani ya mtu binafsii tu. Iwe kati ya mungu na mja wake. Kuchanganya dini na siasa na utawala ni suicidal. Mfano hai ni nchi kama nigeria, sijawahi kuona logic ya watu kuuwana kisa dini. Huwa nahuzunika sana nionapo mauaji ya kidini popote pale hasa hasa afrika.

Tanzania bado tuna nafasi ya kuzuia majanga kama haya yasitokee huko mbeleni. Ingawa mimi niko kisayansi zaidi, lakini na mimi nina dini yangu niliyokulia nayo. Pamoja na hayo, mimi naamini kuwa mimi ni mtanzania/mwafrika kwanza halafu ni mwislamu/mkristo baadae. Major reason ni kuwa naweza kubadili dini nitakavyo (ukoo wetu una ndugu wengi wa dini zote, hawajahi kukosana sababu ya dini), lakini siwezi kubadili asili yangu ya uafrika baada ya kuzaliwa.

Nimewahi kwenda uk nikabaguliwa kwa rangi yangu, nimewahi kwenda saudi nikabaguliwa kwa rangi yangu pia. Nimetembea sehemu nyingi tanzania sijawahi kushangaliwa (sijui kama ni kiswahili sahihi) kama ambavyo watu wa nje, wazungu kwa waarabu wanavyoshangaliwa wakienda hasa vijijini.

Ningeshauri sana vijana wa sasa, ambao ndio walio wengi kwa sasa hapa nchini, wafundishwe utaifa, taifa mbele kabla ya kitu kingine chochote. Watu wengi walio maskini ndio huwa wanakuwa waathirika wakubwa wa machafuko ya aina yoyote; viongozi (siasa/dini) na familia zao huwa wanakimbilia safe heaven wakiwaacha nyinyi mtaabike.

Na ni vizuri tiukasambaza elimu ya kufikiria kwa "big picture" kwa watu wote tanzania. Ushahidi upo, waafrika ni wastaarabu sana, waarabu wa saudia, dubai au iran, au wazungu wa kawaida wa ulaya na marekani, huwa hawana muda au nia mbaya na watu wa afrika.

Choko choko zote huku kwetu afrika hazijawahi kuanzishwa na waafrika wenyewe (as original source). Choko choko zote huanza mahali pale panapojulikana kuna mali, hasa hasa madini na mafuta. Kwa hili mifano iko mingi tu, angola vita vimepiganwa wee, wazungu wamefaidika, waafrika wameachwa vilema na masikini, afrika kusini wamepewa uhuru baada tu ya kuhakikisha urusi imeanguka, haitafaidika tena madini yaliyopo kule. Congo drc kuna vita mpaka leo isiyo na mwisho wala sababu kwa sababu tu kuna mali zilizopo pale.
Angalia sasa, huko kote hakuna dini zilizojikita na zenye nguvu, hakuna udini, lakini vita haiishi.

Si watu wengi wanajua kuwa nigeria ni moja ya nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi sana duniani, lakini wananchi wa kawaida waislamu kwa wakristo hakuna wanachofaidika na hayo mafuta. Wametiwa ujinga wa kugombanishwa kwa udini, akili zao zimeharibiwa hawafikirii kwa mantiki.
Tusifike huko. Tuwarithishe vijana na watoto wetu ukweli huu.
Libya ni mfano wa karibuni sin haja ya kuusemea.

Nasema tena, na kwa ushahidi kabisa, hakuna vita ya kidini popote ambapo sio uarabuni halafu waarabu au waislamu/wakristo wakawa ni chanzo. Chanzo cha choko choko zote za kidini hasa hasa afrika ni cia. Fikiria osama alipotokea. Hivyo ndio dunia inavyoendeshwa.

Yote haya tunayoyaona malumbano ya kidini yamepandikizwa kwa sababu tumeaanza kuachia madini yetu pamoja na kugunduliwa mafuta huku tanzania. Naweza kuwa siko sahiki, lakini nahisi kuna mkono wa cia. rekodini maneno yangu. Ikishathibitka kuwa mafuta yapo tanzania, wakati sisi tutakapokuwa tunapigana kwa tofauti ya dini zetu, wamarekani watakuwa wanajichimbia mafuta pwani yetu kiulaiiini kama iraq, tena watakuwa wanatupiga mabomu mara kwa mara tukilala sana, watuchonganishe.

Watanzania wenzangu, think in the bigger picture, and outside the box.

Ni hayo tu.
kweli sayansi imekuathiri!
 
hapo ndo mnapokoseaga mnaposema muislam ndugu yake muislam ndo maana hata maendeleo yanawaacha nyuma mtabaki kulalamika na kuleta maafa tuu..hamjui kwamba upendo huleta maendeleo badilikeni aisee
 
mbona wakatoliki wana ubalozi wa vatican hapa na unaendeshwa kwa kodi zetu
&lt;br /&gt;<br />
&lt;br /&gt;<br />
partial knowledge ni tatizo kubwa sana. Unamaanisha hata ubalozi wa marekani unaendeshwa kwa kodi za tz? Pls with no research utakuwa weak na mchonganishi. Utaonekana mubabaishaji tu. Jitahidi kutafuta ukweli kabla hujandika au ongea chochote.
 
Back
Top Bottom