tototundu
Senior Member
- Jul 29, 2009
- 198
- 40
Mimi sio mshabiki wa siasa asilani, na sijawahi kuwa na muumini mkubwa wa dini (sayansi iliniathiri toka niko mdogo), lakini Ma- great Thinkers mmenisikitisha kwa jinsi mnavyoshabikia hotuba ya Mheshimiwa Rais kwenye Baraza la Idd, na ambavyo mnashindwa kuona jinsi gani mmekuwa twisted kidogo tu, woote mmezolewa.
Mmesahau kuwa mwanzo wa ngoma ni lele, na haba na haba hujaza kibaba. Baada ya kubishana sana na wanaotaka kuanzisha mahakama ya kadhi na nyinyi kuwashinda, wenzenu wamekaa chini na kufikiria njia mpya ya jinsi ya kujipenyeza. Kosa lao ilikuwa na kujaribu kuanzia juu sana, ambako nyinyi nyote mlishtuka. Ni sawa na kwenda kjijini na kutaka kupewa hekari mia za msitu, wanakijiji lazima wakupige mawe. Lakini ukienda leo ukaomba hekari moja kesho ukaomba ya pili, mwezi ujao ukawa na kumi, hawatashtuka mpaka wanajikuta wamekupa ekari mia bila wao kujua.
Na hawataweza kukunyang'anya tena kwa kuwa utakua umezipata kihalali. Wakitaka kukunyang'anya kwa nguvu bila shaka utaanzisha vita, na ukizingatia ukiwa na hekari mia utakuwa na vibarua wengi, vita na kijiji haitakuwa ndogo.
Hivyo hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa mahakama ya kadhi. Itaanza kwa kuruhusiwa na kuendeshwa kwa gharama zao wenyewe. Halafu zitaanza kuwa common, ghafla atatokea mfadhili kutoka Iran au Saudia atazipa fedha za kutosha kujiendesha kwa miaka mitano. Mara kila wilaya itakuwa na mahakama ya kadhi. Hakafu kila mkoa, baadae tutapata kadhi mkuu wa taifa.
Pengine kusiwe na tatizo la setup nzima, ila ni ukweli ulio wazi kuwa bandu banduhumaliza..... Tutaanza na kesi za mirathi, ndoa na talaka. Kidogo kidogo, tutaanza kuingiza na kesi za kuiba kuku, simu, mitumba na zaidi. Kama livyo tamaa, unapozidi kupata kikubwa ndio unazidi kutamani kikubwa zaidi.
Nawasihi watanzania wenzangu, dini na siasa na utawala, si vitu vya kuchanganya hata kidogo. Huwezi kuwa na nchi moja yenye kufuata sheria mbili zinazopingana. Kutakuwa na ugomvi tu.
Mfano, mtu amekamatwa ugoni, kwa sheria za nchi zilizopo sasa, aliyefumaniwa atalipa faini. Kwa sheria za biblia na za kiislamu, mwanamke katika fumanizi hilo (bila kujali nani mwenye kosa), anatakiwa apigwe mawe mpaka afe. Lazima kutakuwa na conflict of interests. Mtajipa moyo kwamba mtaweka mipaka kwa kila sheria, lakini in practice ni huwa haiwezekani. Jambo la namna hii limeleta migogoro mikubwa sana sehemu nyingi hasa hasa Nigeria.
Ingefaa dini ingebaki kwenye imani ya mtu binafsii tu. Iwe kati ya Mungu na mja wake. Kuchanganya dini na siasa na utawala ni suicidal. Mfano hai ni nchi kama Nigeria, sijawahi kuona logic ya watu kuuwana kisa dini. Huwa nahuzunika sana nionapo mauaji ya kidini popote pale hasa hasa Afrika.
Tanzania bado tuna nafasi ya kuzuia majanga kama haya yasitokee huko mbeleni. Ingawa mimi niko kisayansi zaidi, lakini na mimi nina dini yangu niliyokulia nayo. Pamoja na hayo, MIMI NAAMINI KUWA MIMI NI MTANZANIA/MWAFRIKA KWANZA HALAFU NI MWISLAMU/MKRISTO BAADAE. Major reason ni kuwa naweza kubadili dini nitakavyo (ukoo wetu una ndugu wengi wa dini zote, hawajahi kukosana sababu ya dini), lakini siwezi kubadili asili yangu ya uafrika baada ya kuzaliwa.
Nimewahi kwenda UK nikabaguliwa kwa rangi yangu, nimewahi kwenda Saudi nikabaguliwa kwa rangi yangu pia. Nimetembea sehemu nyingi Tanzania sijawahi kushangaliwa (sijui kama ni Kiswahili sahihi) kama ambavyo watu wa nje, wazungu kwa waarabu wanavyoshangaliwa wakienda hasa vijijini.
Ningeshauri sana vijana wa sasa, ambao ndio walio wengi kwa sasa hapa nchini, wafundishwe utaifa, taifa mbele kabla ya kitu kingine chochote. Watu wengi walio maskini ndio huwa wanakuwa waathirika wakubwa wa machafuko ya aina yoyote; viongozi (siasa/dini) na familia zao huwa wanakimbilia safe heaven wakiwaacha nyinyi mtaabike.
Na ni vizuri tiukasambaza elimu ya kufikiria kwa "BIG PICTURE" kwa watu wote Tanzania. Ushahidi upo, waafrika ni wastaarabu sana, waarabu wa Saudia, Dubai au Iran, au wazungu wa kawaida wa Ulaya na Marekani, huwa hawana muda au nia mbaya na watu wa Afrika.
Choko choko zote huku kwetu Afrika hazijawahi kuanzishwa na Waafrika wenyewe (as original source). Choko choko zote huanza mahali pale panapojulikana kuna mali, hasa hasa madini na mafuta. Kwa hili mifano iko mingi tu, Angola vita vimepiganwa wee, wazungu wamefaidika, waafrika wameachwa vilema na masikini, Afrika Kusini wamepewa uhuru baada tu ya kuhakikisha Urusi imeanguka, haitafaidika tena madini yaliyopo kule. Congo DRC kuna vita mpaka leo isiyo na mwisho wala sababu kwa sababu tu kuna mali zilizopo pale.
Angalia sasa, huko kote hakuna dini zilizojikita na zenye nguvu, hakuna udini, lakini vita haiishi.
Si watu wengi wanajua kuwa Nigeria ni moja ya nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi sana duniani, lakini wananchi wa kawaida WAISLAMU KWA WAKRISTO hakuna wanachofaidika na hayo mafuta. Wametiwa ujinga wa kugombanishwa kwa udini, akili zao zimeharibiwa hawafikirii kwa mantiki.
Tusifike huko. Tuwarithishe vijana na watoto wetu ukweli huu.
Libya ni mfano wa karibuni sin haja ya kuusemea.
Nasema tena, na kwa ushahidi kabisa, hakuna vita ya kidini popote ambapo sio Uarabuni halafu waarabu au waislamu/wakristo wakawa ni chanzo. Chanzo cha choko choko zote za kidini hasa hasa Afrika ni CIA. Fikiria Osama alipotokea. Hivyo ndio dunia inavyoendeshwa.
Yote haya tunayoyaona malumbano ya kidini yamepandikizwa kwa sababu tumeaanza kuachia madini yetu pamoja na kugunduliwa mafuta huku Tanzania. Naweza kuwa siko sahiki, lakini nahisi kuna mkono wa CIA. Rekodini maneno yangu. Ikishathibitka kuwa mafuta yapo Tanzania, wakati sisi tutakapokuwa tunapigana kwa tofauti ya dini zetu, wamarekani watakuwa wanajichimbia mafuta pwani yetu kiulaiiini kama Iraq, tena watakuwa wanatupiga mabomu mara kwa mara tukilala sana, watuchonganishe.
Watanzania wenzangu, THINK IN THE BIGGER PICTURE, AND OUTSIDE THE BOX.
Ni hayo tu.