Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,813
- 4,544
Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) ilitangaza Jumatano wiki hii kwamba dola Milioni 325 ndio kiasi cha fidia ambacho Uganda inapaswa kuilipa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambayo ilikuwa ikidai zaidi ya dola bilioni 11 kwa uvamizi wa Uganda mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa vita vya miaka ya 1998-2003.
ICJ, mahakama ya juu zaidi ya Umoja wa Mataifa, ilibaini kwamba Uganda inapaswa kulipa DRC dola milioni 225 kwa kusababisha vifo vya raia wa nchi hiyo, dola Milioni 40 kwa uharibifu wa mali na dola milioni 60 kwa uharibifu wa maliasili, alisema jaji kiongozi wa mahakama hiyo, Joan Donoghue.
Kesi hii ilianza mwaka wa 2005, ikiwa ni pamoja na malalamiko ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo dhidi ya majirani zake wawili, Uganda na Rwanda, ambazo ziliendesha vita katika eneo hilo wakati huo.
Kigali ilijiondoa haraka katika kesi hii, kwa sababu Mahakama ilijikuta kuwa haina uwezo wa kuhukumu Rwanda. Imesalia Uganda, ambayo imepatikana na hatia ya kuingilia masuala ya DRC. Imetakiwa kurekebisha uharibifu iliyosababisha wakati wa uvamizi kati ya mwaka wa 1998 na 2003 na jeshi lake katika mkoa wa Ituri hasa.