Mahakama ya Hakimu wilaya ya Arusha imemwachia huru diwani wa Sombetini Ally Bananga

Yaani umen
BANANGA ASHINDA KESI YA UCHOCHEZI.

Mahakama ya Wilaya ya Arusha imemuachia huru diwani wa Sombetini na Mwanaharakati mashuhuri nchini, Ally Bananga, katika kesi ya uchochezi iliyokua inamkabili baada ya upande wa mashtaka (Jamhuri) kushindwa kudhibitisha mashtaka yaliyokua yanamkabili.

Bananga alishtakiwa kwa kutoa maneno ya uchochezi, mwezi August mwaka jana akiwa wilayani Monduli akidai kuwa ATAWASHIKISHA UKUTA VIONGOZI WA CCM NA SERIKALI ifikapo September 1 mwaka jana ambapo ilikua siku ya kuzindua operesheni UKUTA nchi nzima.

Upande wa Jamhuri uliieleza mahakama kuwa maneno ya Bananga kwamba atawashikisha ukuta viongozi serikali ni udhalilishaji na ni uchochezi maana yanahamasisha wengine kufanya hivyo.

Awali Wakili wa upande wa utetezi, Shecky Mfinanga alimuuliza askari polisi aliyekua anatoa ushahidi kama anafahamu ukuta. Askari huyo alisema anaufamu. Wakili Mfinanga alimtaka askari huyo ashike ukuta wowote katika mahakama hiyo ili kudhibitisha kama anaujua. Askari huyo akashika.

Mfinanga akamuuliza kama amedhalilika. Askari huyo akasema hajadhalilika. Mfinanga akamuuliza ikiwa yeye ameshika ukuta na hajadhalilika, iweje Bananga kuwashikisha ukuta viongozi wa serikali na wa CCM iwe udhalilishaji? Askari huyo alishindwa kujibu.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Devotha Msofe amesema kuwa upande wa Jamhuri umefanya kosa kumfungulia Bananga kesi wilayani Arusha kwa kosa analodaiwa kufanyia wilayani Karatu

Hivyo basi Mahakama hiyo imemuachia huru Bananga baada ya kukosa ushahidi wa kutosha kumtia hatiani.!
View attachment 517436
Yaani umenichekesha kweli kweli. kaambiwa ashike ukuta akashika. Umedhalilishwa? jibu- hapana. Yaani hii kali kuliko. Hawa mawakili vichwa vyao hatari.
 
Back
Top Bottom