Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu yafuta mashtaka ya kusafirisha dawa za kulevya kwa Mfanyabiashara Mussa Mohamed

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
8,905
25,176
EbMzZtXWoAIRNyM.jpeg

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemfutia mashtaka Mfanyabiashara Mussa Mohamed aliyefikishwa mahakamani hapo leo Juni 23, 2020 akikabiliwa na mashtaka ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroine.

Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Serikali,Sylvia Mitanto kudai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Yusto Ruboroga kuwa upande wa mashtaka hauna nia ya kuendelea kumshitaki Mohamed kwa kosa hilo.

Aliomba mahakama kufuta shauri hilo chini ya kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai. Mapema akisoma mashitaka dhidi ya mshtakiwa huyo, Mitanto alidai mshitakiwa alitenda kosa hilo Juni 5, mwaka huu maeneo ya kuhifadhi mizigo ya wasafiri jijini Dar es Salaam.

Alidai mshitakiwa alikutwa akisafirishwa dawa za kulevya aina ya heroine zenye gramu 101.71. Hata hivyo mshitakiwa alikana mashitaka na upande wa mashitaka ulidai upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kisha wakawasilisha ombi la kumfutia mashtaka.

Hakimu Ruboroga alikubaliana na maombi ya upande wa mashitaka nakuondoa shauri hilona kumuachia huru mshitakiwa. Hata hivyo, mshitakiwa huyo amekamatwa tena na kupelekwa mahabusu ya mahakamani hapo.
 
Hii ndiyo sababu watu wakifutiwa mashitaka wanatoka mahakamani mbio balaa.
Mkuu wale wanaotoka mbio ni wale ambao mahakama inawafutia shitaka lake chini ya kifungu kidogo cha sheria lakn wanaruhusiwa kukamatwa tena na kufunguliwa upya shitaka lake na state attorney ndiye anayewaambia askar kwamba mtuhumiwa akamatwe upya.. Lakn kama state attorney mwenyew ndiye anayeiomba mahakama kuondoa shitaka mtuhumiwa hawezi kukamatwa tena
 
Sawa mkuu!
 
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemfutia mashtaka Mfanyabiashara Mussa Mohamed aliyefikishwa mahakamani hapo leo Juni 23, 2020 akikabiliwa na mashtaka ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroine.

Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Serikali,Sylvia Mitanto kudai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Yusto Ruboroga kuwa upande wa mashtaka hauna nia ya kuendelea kumshitaki Mohamed kwa kosa hilo.

Aliomba mahakama kufuta shauri hilo chini ya kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai. Mapema akisoma mashitaka dhidi ya mshtakiwa huyo, Mitanto alidai mshitakiwa alitenda kosa hilo Juni 5, mwaka huu maeneo ya kuhifadhi mizigo ya wasafiri jijini Dar es Salaam.

Alidai mshitakiwa alikutwa akisafirishwa dawa za kulevya aina ya heroine zenye gramu 101.71. Hata hivyo mshitakiwa alikana mashitaka na upande wa mashitaka ulidai upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kisha wakawasilisha ombi la kumfutia mashtaka.

Hakimu Ruboroga alikubaliana na maombi ya upande wa mashitaka nakuondoa shauri hilona kumuachia huru mshitakiwa. Hata hivyo, mshitakiwa huyo amekamatwa tena na kupelekwa mahabusu ya mahakamani hapo.
Huo ni mtindo wa kubadirisha shitaka, aliposikia hakimu amekubali kufuta kesi angetimua mbio kutoka dirishani.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom