Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imefuta kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili Mbunge wa Ubungo

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeyaondoa mashtaka ya uchochezi yaliyokuwa yakimkabili Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea (46).

Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbroad Mashauri, leo ameyaondoa mashtaka hayo mahakamani hapo kwa sababu hati ya mashtaka ilikuwa na utata na aiendani na kifungu cha 132 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA).

Akitoa uamuzi huo, Hakimu Mashauri alisema kifungu hicho cha sheria kinataka kosa lielezwe kwa uwazi ' kinaga ubaga'.

Alisema katika kesi ya uchochezi iliyokuwa ikimkabili Kubenea ya kusambaza habari ya uongo yenye kichwa cha habari 'yuko wapi atakayeiokoa Zanzibar' ambayo ingeweza kuleta uvunjifu wa amani, Hakimu Mashauri alisema maneno hayo pekee kisheria siyo kosa.

Akiendelea kutoa uamuzi huo, Hakimu Mashauri alisema upande wa mashtaka ulishindwa kueleza maneno yenyewe hasa ya uchochezi yenye lengo la uvunjifu wa amani.

Hivyo, Hakimu Mashauri aliiondoa kesi hiyo mahakamani hapo na mshtakiwa akaachiwa huru na kwamba upande wa mashtaka unaweza kumshtaki upya.

Hata hivyo baada ya Kubenea kuachiwa huru alikamatwa na kupelekwa polisi kati na baadaye akaachiwa kwa dhamana.



IMG_20170125_124556.jpg

IMG_20170125_124800.jpg

[HASHTAG]#Justice[/HASHTAG] For Lema
 
Mkuu unesahau kuweka chama chake kny mabano.

Hivi ni mbunge wa chama gani huyu?
 
Baada ya ushindi wa juzi mkuu ameamini kwamba ccm bado inapendwa hivyo hana sababu ya kuwa na hofu, kesi nyingi za wapinzani zitakufa pengine na mikutano ya hadhara na bunge live itaruhusiwa sasa.
 
Back
Top Bottom