MANI
Platinum Member
- Feb 22, 2010
- 7,320
- 6,376
Tuache kuchangia kwa ushabiki hoja za msingi zinapoletwa jukwaani. Tutumie fursa kujifunza.
Leo ni viongozi wa chadema huwezi kujua kesho nani atakuwa kwenye tatizo kama hili.
Kisheria kama mshtakiwa hajafika mahakamani na yuko nje kwa dhamana hakimu anatakiwa amwite mdhamini na kumuamuru amlete mshtakiwa katika siku itakayopangwa.
Mdhamini akishindwa kumleta mshtakiwa hatua inayofuata ni kuforfeit bond aliyoweka na baada ya hapo ndipo arrest warrant hutolewa. Kwa misingi hiyo ni dhahiri hakimu karuka vihunzi viwili.
Swali la kujiuliza ni, je hakimu amefanya hivyo by design or accidentally? Kama ni accident should it be taken in isolation with dhamana ya Mheshimiwa Lissu. Makosa hayo ya mahakimu kukosea katika misingi ya sheria ya dhamana yakichukuliwa kwa pamoja mtu wa kawaida anapata hisia gani??
Je kama mahakama kuu haitaingilia kurekebisha makosa hayo jamii itaathirika vipi????
Well said !