Civilian Coin
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 2,305
- 4,334
TUIFUNDISHE KAZI MAHAKAMA YA ARDHI na IDARA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA(NIDA) KATIKA MABADILIKO YA MAJINA KISHERIA
Ndugu zangu na Mashabiki wangu, habari za asubuhi!
Naandika hotuba hii nikiwa ofisini Mkolani Sekondari nimekaa kwenye kiti na kunywa uji wa ulezi, naitwa DON NALIMISON, Mwanamziki, Mtetezi wa Haki za Binadamu na Maswala ya Ushauri ya Usalama. Leo tufahamu iwapo mtu amekula kiapo kisheria au kaenda kwa wakili kubadili jina, je Idara ya Mahakama ya Ardhi na NIDA wanawajibika kufanya nini?
Nchi inaongozwa na Sheria, na Sheria zimetungwa na Bunge na sisi ni watekelezaji wa Sheria, tunapoenda kinyume na Sheria hizo ni ishara Taifa linaongozwa na VICHAA wasiofata walichokitunga.
Leo DON NALIMISON nimeenda kwa Wakili nimefata Utaratibu wa Kisheria wa Kubadili Majina ambao unakubalika nchi nzima na dunia nzima. Lakini naenda Mahakama ya Ardhi ili kunihalalishia napewa Masharti ambayo hayana msingi wowote. Mtu kaleta viapo vyake na ameamua mwenyewe kwa mapenzi yàke. Sasa inakuwaje mnataka vielelezo vingine wakati Wakili au Mahakama au Jaji au Hakimu Kisha mdhibitisha kuwa kabadili jina.
Mahakama ya Ardhi inatakiwa kutoa hati bila kutaka vielelezo vingine bali vielelezo vya majina yaliyoachwa tu. Taifa hili halijui Sheria Ila linaigiza Sheria. Nao NIDA mtu anapokuja kubadilishiwa kitambulisho na anakielelezo cha kisheria iwe kwa Wakili au Mahakama wanatakiwa kumbadilishia jina muombaji kutokana na vielelezo vyake vya kisheria na sio kumshauri aendelee na jina la kwanza, Sheria imesha thibitisha kubadilika kwa jina na sahihi na hivyo, lazima mabadiliko ya jina lazima yafanyike ili pia DON NALIMISON aweze kupata Passport ya kusafiria akafanye show Marekani, Afrika Kusini na Uingereza na Australia.
Pia, ili aweze kufanya Mambo mengine katika jamii kwa jina alilochagua kisheria. Lakini ubumbumbu wa Sheria tunajikuta tunawekeana vikwazo vya kijinga visivyo na tija kwa Taifa.
Iweje Baraza la Mtihani linaruhusu mabadiliko ya majina ila nyinyi mkatae? Kuna haja ya wanasheria wafundwe upya maana ya utekelezaji wa Sheria, unajua kusoma Sheria sio KUJUA utekelezaji wa Sheria. Lazima Sheria ziheshimiwe nasio kusikiliza Mkuu wa Wilaya au Mkuu wa Mkoa au DAS/RAS au Waziri, Bali sikiliza Sheria inataka Nini?
Na je mhusika amefata Utaratibu wa Kisheria au lah, Kama amefata Utaratibu wa Kisheria Basi arekebishiwe haraka NIDA yake na Mahakama ya Ardhi impe hati yake bila pingamizi maana yeye ndiye aliyeamua kubadili jina nasio Mahakama Bali ni Sheria imemthibitisha. Zaidi utazipata zote kwa Lugha ya kiingereza kwenye Kitabu Cha "CONVICTION SHAPED MY KNOWLEDGE" kinachoandaliwa na DON NALIMISON mwenyewe.
DON NALIMISON.
O'CLOCK MUSIC PRESS.
20 JULAI 2020.
Simu: +255 682 94 29 01