Mahakama ya Afrika: Nchi wanachama hazitekelezi hukumu zinazotolewa na mahakama, why?

Ikoko

JF-Expert Member
Jul 15, 2022
2,101
3,034
Nafuatilia taarifa ya Habari UTV Azam.

Jaji wa mahakama ya Afrika anaeleza kwamba leo wametoa hukumu zaidi ya kumi zinazohusu mashauri ya nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania.

Hata hivyo jaji anasema, tena kwa unyonge kabisa, kwamba changamoto kubwa ya mahakama hiyo ni nchi wanachama kugomea utekelezaji wa hukumu wanazozitoa.

Sasa mimi najiuliza hii mahakama ina faida gani ikiwa inatoa hukumu na hazitekelezwi? Je hii si ni hasara kwa nchi wanachama kuendelea kuendesha hii mahakama wakati ikitoa hukumu hawatekelezi?

Kingine cha kushangaza ni kwamba Tanzania imejitoa kwenye hiyo mahakama daaah.
 
Back
Top Bottom