Vyama vya Upinzani vyafungua kesi kwenye Mahakama ya Afrika Mashariki kupinga Sheria kandamizi ya vyama vya siasa kutumika

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,395
Serikali imepewa siku 45 na Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) kujibu madai ya vyama vinane vya upinzani vinavyopinga Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya siasa, baada ya vyama hivyo kufungua kesi Februari 12, 2019.

Vyama vinne vya upinzani nchini Tanzania vimeishtaki serikali ya Rais John Pombe Magufuli katika mahakama ya Afrika Mashariki kuhusu haki ya EACJ kufuatia mabadiliko ya hivi majuzi ya sheria ya vyama vya siasa.

Sheria hiyo ambayo ilitiwa saini na Rais John Pombe Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Februari na kuchapishwa katika gazeti la serikali siku 10 baadaye, imezua mjadala mkubwa nchini humo.

Akizungumza jijini Dar es salaam kwa niaba ya vyama vinne vya kisiasa, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe amesema kuwa, malalamishi hayo yamesajiliwa na mahakama ya Afrika Mashariki kuhusu haki ya EACJ.

Hayo yanajiri siku chache tu baada waziri kivuli wa Mashauri ya Kigeni wa Uingereza Liz Mclnnes kuelezea kusikitishwa kwake na kupitishwa kwa sheria ya vyama vya kisiasa nchini Tanzania ambayo anadai inabinya na kukandamiza vyama vya upinzani.

Vyama vya upinzani na asasi za kirai vimekuwa vikilalamikia sheria hiyo vikieleza kwamba, inafanya shughuli za siasa kuwa kosa la jinai.

Bunge lilipasisha muswada huo mwezi Januari mwaka huu na hatimaye kusainiwa kuwa sheria na Rais John Pombe Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Licha ya kupongezwa kwa hatua mbalimbali za maendeleo zilizochukuliwa na serikali yake, zikiwemo za kustawisha miundombinu ya kiuchumi na kupambana na ufisadi, Rais wa Tanzania anakosolewa kuwa anaminya demokrasia sambamba na kuendesha kampeni ya kuua vyama vya upinzani nchini humo

IMG_20190415_193251.png


IMG_20190415_193118.png
IMG_20190415_193142.png
IMG_20190415_193328.png
IMG_20190415_193309.png


IMG_20190415_193118.png
IMG_20190415_193142.png
 
Hashim Rungwe na Salum Mwalimu Kwa niaba ya Vyama vya upinzani vya nchini Tanzania pamoja na wananchi wote wapenda haki , wamefungua kesi dhidi ya Serikali Katili ya Tanzania kwenye Mahakama ya Afrika Mashariki wakipinga Sheria ya kikatili ya vyama vya siasa kutumika.

Mahakama imeombwa kuzuia matumizi ya sheria hiyo hadi pale uamuzi wa kesi ya msingi utakapotolewa.

Taarifa zaidi kuhusiana na kesi hii ambayo kimsingi ni kati ya Mungu dhidi ya Mwovu Shetani , zitaendelea kutolewa kwa kadiri mambo yatakavyokuwa yanatokea .

Mungu wabariki Wapinzani wa Kweli wa Tanzania ambao ndio tegemeo pekee la Wananchi .
 
Hashim Rungwe na Salum Mwalimu Kwa niaba ya Vyama vya upinzani vya nchini Tanzania pamoja na wananchi wote wapenda haki , wamefungua kesi dhidi ya Serikali Katili ya Tanzania kwenye Mahakama ya Afrika Mashariki wakipinga Sheria ya kikatiri ya vyama vya siasa kutumika.
I
Taarifa zaidi kuhusiana na kesi hii ambayo kimsingi ni kati ya Mungu na Shetani , zitaendelea kutolewa kwa kadiri mambo yatakavyokuwa yanatokea .
Tupo kwenye tatizo la Sheria kandamizi,zinapitishwa kwa mabavu na kutumika dhidi ya wapinzani.
Hii dhana Ni mbovu mno,kwamba chama tawala ndiyo Watanzania.Mambo sensitive kama haya huamsha hasira za watawaliwa.
 
I mean what will happen at the end of the day?
Au ni for the record sake...
Maana museven anatafuta mwaka wa 40 madarakani na mahakama i na mahakama ya EA ipo
Pamoja na yote hayo bado Msajili wa vyama wa Uganda hajawahi kupewa nguvu ya kuchagua viongozi wa vyama vya siasa vya nchini humo, wala hajawahi kupewa mamlaka ya kuteuwa wagombea wa vyama vya upinzani nchini humo .

Unajua hii sheria ya vyama vya siasa ya Tanzania hata Makaburu hawakuwahi kuitumia , hii ilitumika na HITLER tu , hatuwezi kukubali unyama huu kutumika Tanzania
 
Mtikila angekuwepo tungelewana tu maana huku ndio uwanja wake,huku mtikila huku Wangwe kule Lissu,tungekuwa kama Kenya tu.Sheria zote kandamizi za kidikteta ni lzm zipingwe.Ilitakiwa kila wafunguliwe kesi nyingi sana mahakamani yaani kila siku wawe wakiburuzwa mahakamani hii itasaidia kuondoa matamko binafsi yasiyo ya katiba
 
Mtikila angekuwepo tungelewana tu maana huku ndio uwanja wake,huku mtikila huku Wangwe kule Lissu,tungekuwa kama Kenya tu.Sheria zote kandamizi za kidikteta ni lzm zipingwe.Ilitakiwa kila wafunguliwe kesi nyingi sana mahakamani yaani kila siku wawe wakiburuzwa mahakamani hii itasaidia kuondoa matamko binafsi yasiyo ya katiba
Kipyenga ndio kimepulizwa mkuu
 
Kumekucha ngoja tuone..maana ile hukumu ya kwanza selikari walisema watakata rufaa ila sijasikia mpaka leo wameishia wapi

Wa sangara
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom