Kunguru Mjanja
JF-Expert Member
- Aug 22, 2012
- 2,036
- 3,929
Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki(EACJ) jana Septemba 19, 2018 imetupilia mbali kesi ya Rashid Salum Adiy na wenzake 39,999 dhidi ya Serikali ya Tanzania
Walifungua kesi hiyo mnamo Februari 13 mwaka huu wakipinga uhalali wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Kwa mujibu wa Msemaji wa Serikali amesema sababu za kina za uamuzi huo zitatolewa baadae lakini Majaji wamewashauri walalamikaji kuwa wanaweza kuwasilisha madai yao upya katika Mahakama za Zanzibar
Katika shauri hilo, Serikali ilitetewa Mawakili waliongozwa na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Ally Possi
=======
Mahakama ya Afrika Mashariki imetupilia mbali ombi lililowasilishwa na raia wa Zanzibar kupinga uwepo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutaka kesi hiyo isikiliziwe Zanzibar.
Rashid Salum Adiy na wenzake 39,999 kutoka Zanzibar wamewasilisha kesi dhidi ya Serikali ya Tanzania wakisema muungano huo ni haramu.
Walalamishi walikuwa wamejitetea kwamba wengi wao ni wakazi wa Zanzibar na huenda ikawa vigumu kwao kuhudhuria vikao vya kusikilizwa kwa kesi hiyo iwapo itaendelea kusikiliziwa Zanzibar.
Ombi hilo limetupiliwa mbali na majaji katika mahakama hiyo mjini Arusha, ingawa hawakutoa maelezo kuhusu sababu zilizowaongoza kutoa uamuzi huo.
Katika uamuzi wake, majaji walisema hakuna haja na wala haifai kwa mahakama hiyo kuagiza kwamba vikao vya kesi hiyo viandaliwe Zanzibar.
Kifungu 68 cha sheria za mahakama hiyo kinawaruhusu kutoa uamuzi kwanza na kisha kutoa maelezo ya kina baadaye.
Wameahidi kutoa maelezo ya kina baadaye.
Katika kesi hiyo, Salum na wenzake wawawameshtaki miongoni mwa wengine Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwezi Machi, mahakama hiyo ilikuwa imetupilia mbali ombi la walalamishi la kutaka kumteua Japheth Kiziba kuwa mwakilishi mpya mahakamani.
Majaji wakiongozwa na Jaji Monica Mugenyi walilalamikia walichosema ni ishara za walalamishi kutochukulia kwa uzito kesi waliyokuwa wameiwasilisha, wakizungumzia moja ya maombi yaliyokuwa yamewasilishwa.
"Hii ni kama kuipotezea muda mahakama hii na ni hatua ambayo imesababisha kuchelewa kusikizwa kwa kesi hii, na pia ni kutumia vibaya mchakato wa mahakama," walisema majaji.
Wakati mmoja, walalamishi walijaribu kutumia lugha ya Kiswahili, jambo ambalo mahakama hiyo mwezi Machi ilisema linaenda kinyume na mkataba wa kuundwa kwa mahakama hiyo Kifungu 46 ambacho kinasema lugha ya Kiingereza ndiyo lugha pekee ya jumuiya hiyo.
-----
KUMRADHI: MAHAKAMA 'HAIJATUPILIA MBALI' KESI YA KUPINGA MUUNGANO BALI IMEKATAA OMBI MOJA KATIKA KESI HIYO
Mahakama ya Haki ya Afrika ya Mashariki imekataa ombi namba 7 la Walalamikaji 40,000 Waliotaka Kesi ya kupinga uhalali wa Muungano wa Tanzania ikasikilizwe Zanzibar
Kwenye uamuzi huo, Mahakama haikutajwa kuwa kesi yenyewe ya kuupinga uhalali wa Muungano imetupiliwa mbali
Walalamikaji hao wanaoongozwa na Rashid Salum Adiy Walifungua kesi hiyo mnamo Februari 13 mwaka huu
Hata hivyo, Msemaji wa Serikali kupitia akaunti yake katika Mtandao wa Twitter ameandika kuwa Mahakama hiyo imetupilia mbali kesi hiyo
Soma zaidi.....Mahakama ya Afrika Mashariki Arusha: Muendelezo wa kesi ya kuhoji uhalali wa muungano - JamiiForums