Mahakama Tanzania zinakosa nguvu na mvuto kwa wananchi kwa sababu ya Siasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahakama Tanzania zinakosa nguvu na mvuto kwa wananchi kwa sababu ya Siasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamundu, Apr 5, 2012.

 1. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Mimi nashauri Jaji mkuu wa Tanzania sio chaguo zuri na hii ni kama ilivyokuwa Mahita wakati akiwa IGP. Kazi ya jaji mkuu na hata IGP ni kuweka bayana kwa majaji kwamba Mahakama ni Chombo ambacho kinatakiwa kiwe cha kuaminiwa na chenye nguvu kuliko idara yeyote Tanzania. Kama vile Mahita alivyofanya Polisi ishuke hadhi wakati wa Mkapa kwasababu za kujiingiza kwenye siasa ni vilevile Jaji mkuu anafanya Mahakama ianze kutharauliwa na watu kuon akama ni chombo cha kuzuia demokrasia Tanzania. Hakuna mtu au chombo chochote duniani ambacho kina weza kushinda Demokrasia na ndiyo maana Wakoloni walishidwa pamoja na kuwa na nguvu za aina zote. Kwa miaka michache sasa nimesikia Mahakama inaweza kuhongwa kiholela holela tu kama vyombo vingine vya serikali!!!. Kama tulivyoona Mahita alivyoaribu serikali tunataka Jaji mkuu ambaye ana hekina na msafi ambae anaweza kuheshimiwa na majaji wote na ndiyo maana Jaji Mama Munuo ndiye angetakiwa kuwa jaji mkuu Tanzania na sio huyu tuliyenae ambaye hailewi vizuri majaji mikoani wanafanya nini. Kama tulivyomuona IGP mwema anajaribu kuridisha heshima ambayo Mahita aliipoteza badi Raisi anatakiwa kubadilisha Jaji mkuu na kuweka mtu ambaye ataogopeka na kila jaji Tanzania.
  Hao viongozi wanaofikiria kwamba kutengua ubunge wa Lema kutawasaidia CCM anakosea maana sasa kuna mfano mzuri wa wananchi kuona kwa macho yao matusi ya CCM huko Meru wakati hakuna hata video ya matusi ya Lema Arusha bali ni maneno tu. Hata mbunge aliyeshidwa hakwenda mahakamani!!. Demokrasia haiwezi kuchezewa hivi na watu bado wakawa na imani na Mahakama. Hakuna siasa za CCM wala Chadema zisizo na kashifa sasa je CCM wangeshida Arumeru jaji huyo angetengua uchaguzi kwasababu Lusinde katukana! au ni kwa upinzania pekee!
   
Loading...