Mahakama Tanzania Mnajidhalilisha

a.9784

Senior Member
Feb 19, 2008
145
4
Hivi wewe Jaji Kaijage na wewe ni fisadi au umelogwa,sasa ulichokifanya kumuachia mtoto wa Keenja ndio nini.Jamani mambo mengine ukisimuliwa katika mazingira ya kawaida huwezi kuamini kama binadamu wa kawaida anaweza akafanya hivyo.Sema huo ujaji ulipewa na mwenyekiti wa sisiem kwa hiyo unalipa fadhila,hivi kwa akili yako huoni kama umemdhalilisha hakimu wako kwa mambo ya kijinga,You know how our Criminal Procedure is au ulikua kilaza katika somo hili.Ulichofanya ni aibu na fedheha kwa watendaji wako wa chini.

Hapa kuna mazingira ya jaji kula rushwa.Nasema ni mazingira ya rushwa kwa sababu Kaijage anazo ndoto za kuupata Ujaji mkuu ndio maana anawapendelea wadhambi ili baadae wamuone,hii ni rushwa.Kweli ukatengue uamuzi after two hours,Kaijage hata taaluma ya sheria hujatendea haki.Hivi huoni hata aibu?Hakimu wako amejikunja lakini wewe umeona upuuzi mtupu unatoa amri eti Keenja achiliwe huru mara moja.

Benadetha nakupongeza kwa kuisusia hiyo kesi na kama Kaijage hajipendi akuwajibishe aone cha moto.

Halafu mnatuambia kwamba hakuna aliye juu ya sheria kama sio kutudanganya.Wadau naomba mnisaidie kwa hili.

Source NIPASHE ya tar.27 March,2008 page 16(Na Hellen Mwango)
 
NAJIULIZA HV HAWA MAJAJI WA TZ WANAFANYIWAGA "VETTING"? maana maamuzi yao ya ajabu ajabu mno hebu angalia kesi ya ZOMBE, hii ya KEENJA, LULU, etc
 
Kwanza napenda kutoa pongezi za dhati kwa hakimu aliyeamua kujitoa katika hiyo kesi, alionyesha dhamira ya kutenda haki, kwa kuanza kabisa na sheria ya kumnyima mtoto wa Fisadi dhamana, kisheria, pili na kwa ujasili aliochukua kuona kuwa inawezekana yeye awezi kufanya hiyo kazi, na kujitoa

Hongera sana mama.

Pili niombe kuelewa, hawa mahakimu wana nguvu kabisa ya kufanya maamuzi kisheria na yakafuatwa?? hii sio siasa, sasa iweze hawa najaji kila siku wao wanatengua mambo tuuuuuuu

Huu ni mwelekeo wa Rushwa, cha jabu hata wahusika wakuu, hawasemi lolote
Tumeona juzi juzi, eti kuna jaji kamuachia padre mlawiti, jamani hili nalo liliitaji tena kuangaliwa, wakati kesi ilishasomewa hukumu na ushahidi wote ukaoneka, leo mnatueleza eti ushahidi haujitoshelezi
Haya leo mnatengua maagizo ya Hakimu mwadilifu kwa sababu tu huyo ni mtoto wa Keenja, tena agizo linatoka mahakama kuu, vipi mtaendelea kutoa maagizo kama haya kwa watanzania wote watakao kuja na sababu za uongo?????

Hivi hii serikali jamani vipi? mimi naona hapa ni kuanzisha mauaji ya Mafisadi wote na viongozi ambao ni wala rushwa. Hii itasaidia sana kuwaweka sawa

Vipi mpo tayari tuingie mstuni wazee, vita hii ni watanzania walipa kodi na Viongozi mafisadi wanaotunyonya jamani, twendeni la sivyo tutabaki kulalamika tu
Tahadhari..., unaweza kufunguliwa kesi ya ugaidi. Huu uzi unaweza kuwekwa u-tube.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom