Mahakama sasa kutopokea kesi zisizokamilisha upelelezi

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
MAHAKIMU wa Mahakama ya Hakimu Mkazi na Wilaya nchini, wameagizwa kuzingatia maelekezo ya tangazo la serikali namba 296 la mwaka 2002 linaloeleza kesi zote zilizokamilika upelelezi zipokelewe mahakamani na kuanza kusikilizwa mara moja.

Kadhalika, kesi ambazo upelelezi wake haujakamilika wasizipokee wazingatie tangazo hilo kufuatia agizo la serikali kuzuia mkusanyiko kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa corona.

Rai hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania, Dk. Eliezer Feleshi, katika mkutano wake na waandishi wa habari, kuhusu mhimili huo unavyounga mkono juhudi za serikali.

"Imefika wakati sasa mahakimu wafawidhi wa Mahakama za Hakimu Mkazi na Wilaya wafanye kazi kwa kuzingatia tangazo hilo na kama kesi upelelezi haujakamilika, basi ziishie hukohuko na si kupelekwa mahakamani kufuatia agizo la serikali kutoka kwa Rais Dk. John Magufuli, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Afya, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu," alisema Jaji Kiongozi.

Alisema mahakama imeongeza kasi ya matumizi ya mifumo hiyo kwa kanda ya Dar es Salaam kwa kesi zote za jinai zinazoahirishwa kutokana na sababu mbalimbali, watuhumiwa waliopo katika Gereza la Keko na Segerea watasikiliza, yataendelea kuahirishwa kwa njia ya Mahakama Mtandao (Video Conference) ili kuepuka msongamano na mkusanyiko wa mahabusu na wafungwa mahakamani.

Pia, alisema Kanda ya Mbeya na Bukoba zina vifaa vya mahakama mtandao, utaratibu unakamilishwa kwa uwekaji wa vifaa hivyo katika Magereza yaliyopo katika kanda hizo ili huduma hiyo ianze mara moja.

"Juhudi za kuweka vifaa hivyo kwa kanda zingine zilizosalia zinaendelea na baada ya muda mfupi huduma kama hizo zitatolewa, utumiaji wa mfumo wa usajili wa kesi kwa njia ‘E-Filing’ (kielektroniki). Mahakama inaimarisha na kuwasisitiza wadau wote (wananchi, mawakili wa serikali na mawakili wa kujitegemea) kusajili kesi kwa njia hii ya mitandao ili kupunguza msongamano na mchanganyiko wa watu katika maeneo ya mahakama," alisema Jaji Kiongozi, Dk. Feleshi.

Alisema muhimili huo utaongeza wigo wa matumizi ya Tehama kwa njia ya barua pepe na simu za mkononi kwa kutumia mfumo wa 'SMS notification' na 'USSD' katika usambazaji na upatikanaji wa taarifa za mashauri ambao hautawalazimu wadaiwa kufika mahakamani kupata taarifa hizo.

Mahakama itakuwa ikiendesha programu ya elimu ya namna ya kusajili mashauri, kupata taarifa pamoja na kutoa msaada wa usajili wa kesi kwa njia ya kielektroniki kwa kuanza na mahakama zenye kesi nyingi ambazo zinaweza kusababisha mkusanyiko wa watu wengi.

Naye Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Dar es Salaam, Lameck Mlacha, alisema wanatumia Mahakama Mtandao kwa lengo la kupunguza maambukizi ya corona.

Vile vile, ameshawaagiza mahakimu kupunguza idadi ya watu wakati wa usikilizwaji kesi katika vyumba vya mahakama na badala yake zitumike kumbi za wazi.

Chanzo: Nipashe
 
Hata kwa wapinzani na money laundering case au sijasoma mpaka mwisho.
 
Iwe hivi.
  1. Marufuku kukamata kama upelelezi. haujakamilika.
  2. Marufuku kuweka mtu mahabusu. kama upelelezi haujafanyika.
Hayo yafanyike kipindi chote sio wakati huu tu Corona, ikigundulika makosa yamefanyika na akakaa mahabusu au kwenda mahakamani basi fidia kubwa ilipwe kwa mhusika na waliotenda ujinga huo wawajibishwe.
 
Mbona kina Rugemalila huu ni mwaka wa nne upelelezi bado mpaka sasa, kama kweli mahakama ina meno iwaachie tuone.
 
Iwe hivi.
  1. Marufuku kukamata kama upelelezi. haujakamilika.
  2. Marufuku kuweka mtu mahabusu. kama upelelezi haujafanyika.
Hayo yafanyike kipindi chote sio wakati huu tu Corona, ikigundulika makosa yamefanyika na akakaa mahabusu au kwenda mahakamani basi fidia kubwa ilipwe kwa mhusika na waliotenda ujinga huo wawajibishwe..
Hawawezi kukubali kufanya hivyo maana itakuwa ni mwisho wa kuwabambikizia watu kesi!
 
Iwe hivi.
  1. Marufuku kukamata kama upelelezi. haujakamilika.
  2. Marufuku kuweka mtu mahabusu. kama upelelezi haujafanyika.
Hayo yafanyike kipindi chote sio wakati huu tu Corona, ikigundulika makosa yamefanyika na akakaa mahabusu au kwenda mahakamani basi fidia kubwa ilipwe kwa mhusika na waliotenda ujinga huo wawajibishwe..
1. Mtuhumiwa kukamatwa ni sehemu ya upelelezi. Kwani maelezo yake yanahitajika.

2. Kukaa mahabusu pia hakukwepeki kwani ukishakamatwa unaweza kuwekwa mahabusu ukisubiri kuhojiwa.

Jambo la msingi ni kuepuka kuwapeleka mahakamani watu bila kukamilisha upelelezi Nadhani umeelewa.
 
  1. Unashindwaje kufanya upepelezi mtuhumiwa akiwa nje? na wewe ukakusanya ushahidi wote na ukikamilika ndio unampeleka mahabusu tayari kwa kesi mahakamani ambayo nayo haitakiwi kuchukua muda.
  2. Unawezaje kumuweka mahabusu mtuhumiwa ambaye unamtuhumu na mahakama haijathibitisha.
  3. Ikigundulika mahakamani huyu uliyemuweka mahabusu si mhusika - atafidiwi gharama na muda wake?
La msingi pia tujitahidi kuharakisha muda wa kukamata, kupeleka mahakamani na kuhukumu.
Tujitahidi kurahisisha suala la dhamana kwa walio mahabusu vituoni ili watokee makwao kuja mahakamani.
 
MAHAKIMU wa Mahakama ya Hakimu Mkazi na Wilaya nchini, wameagizwa kuzingatia maelekezo ya tangazo la serikali namba 296 la mwaka 2002 linaloeleza kesi zote zilizokamilika upelelezi zipokelewe mahakamani na kuanza kusikilizwa mara moja.

Kadhalika, kesi ambazo upelelezi wake haujakamilika wasizipokee wazingatie tangazo hilo kufuatia agizo la serikali kuzuia mkusanyiko kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa corona.

Rai hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania, Dk. Eliezer Feleshi, katika mkutano wake na waandishi wa habari, kuhusu mhimili huo unavyounga mkono juhudi za serikali.

"Imefika wakati sasa mahakimu wafawidhi wa Mahakama za Hakimu Mkazi na Wilaya wafanye kazi kwa kuzingatia tangazo hilo na kama kesi upelelezi haujakamilika, basi ziishie hukohuko na si kupelekwa mahakamani kufuatia agizo la serikali kutoka kwa Rais Dk. John Magufuli, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Afya, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu," alisema Jaji Kiongozi.

Alisema mahakama imeongeza kasi ya matumizi ya mifumo hiyo kwa kanda ya Dar es Salaam kwa kesi zote za jinai zinazoahirishwa kutokana na sababu mbalimbali, watuhumiwa waliopo katika Gereza la Keko na Segerea watasikiliza, yataendelea kuahirishwa kwa njia ya Mahakama Mtandao (Video Conference) ili kuepuka msongamano na mkusanyiko wa mahabusu na wafungwa mahakamani.

Pia, alisema Kanda ya Mbeya na Bukoba zina vifaa vya mahakama mtandao, utaratibu unakamilishwa kwa uwekaji wa vifaa hivyo katika Magereza yaliyopo katika kanda hizo ili huduma hiyo ianze mara moja.

"Juhudi za kuweka vifaa hivyo kwa kanda zingine zilizosalia zinaendelea na baada ya muda mfupi huduma kama hizo zitatolewa, utumiaji wa mfumo wa usajili wa kesi kwa njia ‘E-Filing’ (kielektroniki). Mahakama inaimarisha na kuwasisitiza wadau wote (wananchi, mawakili wa serikali na mawakili wa kujitegemea) kusajili kesi kwa njia hii ya mitandao ili kupunguza msongamano na mchanganyiko wa watu katika maeneo ya mahakama," alisema Jaji Kiongozi, Dk. Feleshi.

Alisema muhimili huo utaongeza wigo wa matumizi ya Tehama kwa njia ya barua pepe na simu za mkononi kwa kutumia mfumo wa 'SMS notification' na 'USSD' katika usambazaji na upatikanaji wa taarifa za mashauri ambao hautawalazimu wadaiwa kufika mahakamani kupata taarifa hizo.

Mahakama itakuwa ikiendesha programu ya elimu ya namna ya kusajili mashauri, kupata taarifa pamoja na kutoa msaada wa usajili wa kesi kwa njia ya kielektroniki kwa kuanza na mahakama zenye kesi nyingi ambazo zinaweza kusababisha mkusanyiko wa watu wengi.

Naye Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Dar es Salaam, Lameck Mlacha, alisema wanatumia Mahakama Mtandao kwa lengo la kupunguza maambukizi ya corona.

Vile vile, ameshawaagiza mahakimu kupunguza idadi ya watu wakati wa usikilizwaji kesi katika vyumba vya mahakama na badala yake zitumike kumbi za wazi.

Chanzo: Nipashe
Kumbe tangu 2002 kuna takwa hilo. Je walioluwa walikiuka ,(ambao wengine ni majaji sasa) wachukuliwe hatua gani? Tuna kauli.mbiu ya 'kutii sheria bila shuruti'. Kuna watu haeakutii hii kauli mbiu...tunataka kujua shuruti gani itachukuliwa kwao.
 
  1. Unashindwaje kufanya upepelezi mtuhumiwa akiwa nje? na wewe ukakusanya ushahidi wote na ukikamilika ndio unampeleka mahabusu tayari kwa kesi mahakamani ambayo nayo haitakiwi kuchukua muda.
  2. Unawezaje kumuweka mahabusu mtuhumiwa ambaye unamtuhumu na mahakama haijathibitisha.
  3. Ikigundulika mahakamani huyu uliyemuweka mahabusu si mhusika - atafidiwi gharama na muda wake?
La msingi pia tujitahidi kuharakisha muda wa kukamata, kupeleka mahakamani na kuhukumu.
Tujitahidi kurahisisha suala la dhamana kwa walio mahabusu vituoni ili watokee makwao kuja mahakamani.
Kweli hii elimu inahitajika kutolewa;

1. Upelelezi hauwezi kukamilika bila maelezo ya mtuhumiwa kupatikana.

2. Kuna mazingira ya kesi ambayo mtuhumiwa huwekwa mahabusu kwanza kabla ya kuanza kutoa maelezo. ( Kwa mfano mtu kafanya mauaji, huwezi sema umuahe akiranda randa huko mtaani wakati unasubiri kukamilisha upepelezi wako) Mtu kama huyo lazima utamuweka mahabusu kwa ajili ya usalama wake, kwani kuna wanaoweza mdhuru na ama akawadhuru na wengine pia ambao wameona tukio na wanaweza saidia katika kutoa ushahidi)

Kukaa mahabusu sio kifungo.

3. Fidia hupatikana endapo itaonekana kesi ilifunguliwa kwa lengo la kumkomoa mtuhumiwa na sio kwamba kutokutwa na hatia pekee ni tiketi ya kupata fidia.
 
Atoe na kalipio kwa askari magereza waliowapiga viongozi wa CHADEMA bila kosa.
 
Kweli hii elimu inahitajika kutolewa;

1. Upelelezi hauwezi kukamilika bila maelezo ya mtuhumiwa kupatikana.

2. Kuna mazingira ya kesi ambayo mtuhumiwa huwekwa mahabusu kwanza kabla ya kuanza kutoa maelezo. ( Kwa mfano mtu kafanya mauaji, huwezi sema umuahe akiranda randa huko mtaani wakati unasubiri kukamilisha upepelezi wako) Mtu kama huyo lazima utamuweka mahabusu kwa ajili ya usalama wake, kwani kuna wanaoweza mdhuru na ama akawadhuru na wengine pia ambao wameona tukio na wanaweza saidia katika kutoa ushahidi)

Kukaa mahabusu sio kifungo.

3. Fidia hupatikana endapo itaonekana kesi ilifunguliwa kwa lengo la kumkomoa mtuhumiwa na sio kwamba kutokutwa na hatia pekee ni tiketi ya kupata fidia.

  1. Haiwezekani mtuhumiwa kuhojiwa halafu akaachwa aendelee na hamsini zake mpaka pale ushahidi wakutosha utakapopatikana na upepelezi kukamilika ndio akamatwe?
  2. Mahakama pekee ndio yenye uwezo wa kusema fulani ana makosa, kabla ya kumpeleka mtu mahakamani na kuhukumiwa huko kote nyuma hubaki kuwa mtuhumiwa. Mkuu kila mtu ana haki zake haijalishi ana makosa kiasi gani, muuaji hawezi kuwa muuaji kabla mahakama haijasema mtu A ana kesi ya kujibu, Aliyeua anapaswa kulindwa hata akiwa mtaani mpaka pale ushahidi utakapokamilika ndio akamatwe na kushitakiwa kwa mauaji yake..
  3. Ni makosa kumuweka mtu mahabusu miaka 3 halafu unamuachia unasema hana hatia haijalishi kwa kosa lipi na hapa lazima fidia ilipwe na kama hatuna sheria hiyo basi tunakiuka haki za binadamu na kunyanyasa raia.
Tujitahidi kuwekeza kwenye elimu ya uchunguzi na upepelezi wa kisasa ili tupunguze au kuondoa mambo haya ya kukamatana halafu kwa miaka mitatu unasema upepelezi haujakamiliki.
Tusomeshe vijana wetu wapate elimu nzuri ili waifan kazi yao kiufanisi.
Tuwekeze kwenye teknolojia ili upelelezi ufanyike ipasavyo na kwa wakati..

Haya yote tunayobishana hapa sio mageni duniani na nchi zote zilizoendelea na kujali haki za raia wake hujitahidi kwenye hilo..

Kipo kis cha kijana wa kitanzania aliyemuua binamu yake pale USA, hakukamatwa na alihojiwa mara nyingi na vyombo vya usalama na akaachwa anaendelea na maisha mpaka pale vilipojidhihirisha na ushahidi wa kutosha ndipo walipomkamata.
 
Hata huko Ulaya kwenye weledi mkubwa ni very rare kukuta mtuhumiwa wa mauaji yupo ana randa randa tu huko mtaani kusubiri hukumu isema kuwa ni kweli kaua. Mkuu nadhani unazungumza tu for purpose of argument ila kiuhalisia ni jambo gumu kutekelezeka.

kwa baadhi ya makosa utakua ni uzembe kumuaha mtuhumiwa nje ya uangalizi wakati akisubiri hukumu. Anaweza kimbia kudhurika au kudhuru. Mfano mwingine mdogo ni kwa yule jamaa aliharibu korani, kumuaha arande rande inaweza kuleta taharuki isiyokuwa ya lazima hivyo kumpumzisha mahali salama ni kwa usalama wake na kuepusha kutendeka kwa makosa mengine.

Hili swala sio rahisi kama tunavyofikiri, watu wanateseka ila kuna umuhimu wa kulifanyia kazi kwa umakini mno ama la, kuna haki za watu zinawezapotea, kumbuka kwamba haki sio kwa mtuhumiwa pekee, ila pia hata kwa mhanga.

Ni jambo la kawaida tu kwa asili ya binadamu, mfano ukaona mtu kamdhuru ndugu yako halafu anarandaranda tu huko barabarani, nadhani utakuwa na fikra kwamba, ama katoa rushwa, ama mamlaka haziupi uzito tukio lako, ikakufanya uhukue hatua mwenyewe, hivyo kuwekwa mahabusu inaweza ikawa pia kwa faida ya mtuhumiwa.
 
Back
Top Bottom