Mahakama Nigeria yakataa uchaguzi kurudiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahakama Nigeria yakataa uchaguzi kurudiwa

Discussion in 'International Forum' started by Ladslaus Modest, Dec 12, 2008.

 1. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #1
  Dec 12, 2008
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mahakama Nigeria yakataa uchaguzi kurudiwa

  Imeandikwa na mwandishi wa BBC

  Uchaguzi wa Nigeria ulikuwa halali

  Mahakama Kuu ya Nigeria imekataa pingamizi la mwisho kuhusiana na uchaguzi mkuu wa rais wa mwaka jana uliompa ushindi rais wa sasa Umaru Yar'Adua.

  Viongozi wa upinzani wameitaka mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi kwa maelezo uchaguzi huo ulitawaliwa na ghasia na wizi wa kura.

  Waangalizi wa ndani na wa kimataifa walioshuhudia uchaguzi huo pia walishutumu namna uchaguzi huo wa mwezi wa Aprili mwaka jana ulivyoendeshwa.

  Lakini Mahakama Kuu imekataa pingamizi hilo lililokubaliwa na mahakama za chini kwa madai kuwa mawakili hawakutoa ushahidi wa kutosha kuweza kutengua matokeo hayo.

  Kwa maana hiyo kwa mujibu wa Jaji Niki Tobi wa mahakama kuu, mahakama hiyo imemthibitisha, Umaru Yar'Adua ndie rais na Dr Goodluck Jonathan ni makamu halali wa rais wa Nigeria.

  Mwandishi wa BBC Alex Last aliye katika mji mkuu, Abuja, amesema mvutano wa kisheria kuhusiana na uchaguzi huo, umezorotesha uwezo wa kufanya kazi wa Rais Yar'Adua kwa miezi 18 aliyokuwepo madarakani.

  Nigeria kwa sasa inakabiliwa na matatizo makubwa ya kiuchumi kwa sababu ya kuanguka bei ya mafuta, chanzo kikuu cha mapato ya Nigeria.


  Chanzo: BBCSwahili.com | Habari | Mahakama Nigeria yakataa uchaguzi kurudiwa
   
Loading...